Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Na wale wanaoota vitu ambayo hawajawahi hata kuviona au kuvifahamu halafu baadae inatokea kweli inakuwaje?
Na msingi wa mada yangu uko hapa yaan ni kitu gani hua kinafanyika mpka mtu ajue jambo kama hilo
 
Ukienda mbugani kutalii ambapo akili inajua na imeshajiwekea kwamba mazingira ya mbugani (porini) huwa kuna wanyama na wadudu hatari.

Halafu ukiwa Vacation mbugani, ukaota nyoka anakung'ata, lakini kiuhalisia hajakung'ata ni ndoto tu.

Ukaendelea kutalii mbugani hapo kwa siku kadhaa, Halafu ghafla Nyoka akakung'ata.

Utasema ndoto yako uliyoota kabla imetimia kiroho kwa mambo yajayo?

Au akili yako imesha jijenga kwamba kiuhalisia mazingira ya mbugani huwa wanaishi wadudu hatari kama nyoka ndio maana ukaota ndoto kabla ya kung'atwa?
Mkuu kuna watu wana maono kupitia ndoto.

1.Kuna mtu usiku aliota ndugu yake kapata ajali na amepata majeraha na damu zinamchuruzika ,asubuhi akapewa taarifa ndugu yake kapata ajali na aliumia sana.

2.Kuna siku aliota msiba wa mtu wake wa karibu upande wa ushemejini na huyo mtu alikuwa haumwi wala nini lakini baada ya siku kadhaa week 3 -4 akasikia huyo mtu amekata MOTO.

Baada ya hayo matukio wazee ikabidi wamuweke chini kwamba akiota kitu kibaya basi aamke na akemee.

Zipo kweli ndoto zinazotokana na kuwaza kitu kwa sana ila kuna nyingine ni ufunuo(maono).
 
Kuna mtu anaota kuna mtu kafa hata kabla kifo hakijatokea na hata kama hana taarifa kuna family member mgonjwa. Hii inaletwa na nini?
Akili ya mwanadamu yeyote automatically inajua kwamba kuna kufa.

Na inajua kifo kipo.

Kwa hiyo akili yako, inaweza kuota mtu yeyote amekufa kwa sababu tukio la kifo, Si tukio geni kwenye akili ya mwanadamu.
 
Mkuu kuna watu wana maono kupitia ndoto.

1.Kuna mtu usiku aliota ndugu yake kapata ajali na amepata majeraha na damu zinamchuruzika ,asubuhi akapewa taarifa ndugu yake kapata ajali na aliumia sana.

2.Kuna siku aliota msiba wa mtu wake wa karibu upande wa ushemejini na huyo mtu alikuwa haumwi wala nini lakini baada ya siku kadhaa week 3 -4 akasikia huyo mtu amekata MOTO.

Baada ya hayo matukio wazee ikabidi wamuweke chini kwamba akiota kitu kibaya basi aamke na akemee.

Zipo kweli ndoto zinazotokana na kuwaza kitu kwa sana ila kuna nyingine ni ufunuo(maono).
Je Kiranga una maoni gani hapa?
 
Na msingi wa mada yangu uko hapa yaan ni kitu gani hua kinafanyika mpka mtu ajue jambo kama hilo
Kwenye kumbukumbu ya MV Bukoba mwaka huu kuna member alisema dada yake aliota kuhusu ajali ile kabla na akaandika kwenye diary. Ile diary baba yake alivyoenda kwenye graduation yake Rugambwa Girls alirudi nayo pamoja na mizigo iliyotangulia. Bahati mbaya yule dada alifariki kwenye ile ajali,baadae kuangalia kwenye vitu vyake ndo wanakutana na ile diary inaelezea ajali. Kama hapo chanzo cha huyo dada kuota kuhusu ajali ni nini ndo swali gumu.
 
Mkuu kuna watu wana maono kupitia ndoto.

1.Kuna mtu usiku aliota ndugu yake kapata ajali na amepata majeraha na damu zinamchuruzika ,asubuhi akapewa taarifa ndugu yake kapata ajali na aliumia sana.

2.Kuna siku aliota msiba wa mtu wake wa karibu upande wa ushemejini na huyo mtu alikuwa haumwi wala nini lakini baada ya siku kadhaa week 3 -4 akasikia huyo mtu amekata MOTO.

Baada ya hayo matukio wazee ikabidi wamuweke chini kwamba akiota kitu kibaya basi aamke na akemee.

Zipo kweli ndoto zinazotokana na kuwaza kitu kwa sana ila kuna nyingine ni ufunuo(maono).
Atakupa majibu yale yale kama aliyotoa kule na juu ni mepesi mnoo hayajitosherezi mifano anayotoa haina hoja kabisa kulingana na mada husika
 
Mkuu nadhani kuna kitu haujakielewa hapo, yeye ameelezea namna ubongo unavyo fanya kitu kinaitwa constant risk assessment.

Iko hivi, ndoto ambazo wengi huwa wanaziona kama ni maono, yale huwa ni matokeo ya kile wanacho kutana nacho kwenye maisha yao ya kila siku (matukio ya siku zote, kuanzia unayoyaona mtandaoni mpaka yale mnayoyaishi mtaani).
Huo ni upande mmoja wa ndoto, na hayo sio maono. Ndoto zenye sura za watu unaowajua, na mambo uliyofanya au kuwaza mchana, sio maono. Hizo ni ndoto za dhamiri na nyingine ndo huitwa nightmare

Ndoto za maono, ni ndoto za hatma. Hizi mara nyingi huwa metaphoric, haziji na sura za watu unaofahamu na mara nyingi kama sio mara zote, haziji na tafsiri ya moja kwa moja.
 
Akili ya mwanadamu yeyote automatically inajua kwamba kuna kufa.

Na inajua kifo kipo.

Kwa hiyo akili yako, inaweza kuota mtu yeyote amekufa kwa sababu tukio la kifo, Si tukio geni kwenye akili ya mwanadamu.
Haya majibu ni mepesi jamani hivi huoni tofauti wa mifano yako na mada yenyewe?
 
Kwenye kumbukumbu ya MV Bukoba mwaka huu kuna member alisema dada yake aliota kuhusu ajali ile kabla na akaandika kwenye diary. Ile diary baba yake alivyoenda kwenye graduation yake Rugambwa Girls alirudi nayo pamoja na mizigo iliyotangulia. Bahati mbaya yule dada alifariki kwenye ile ajali,baadae kuangalia kwenye vitu vyake ndo wanakutana na ile diary inaelezea ajali. Kama hapo chanzo cha huyo dada kuota kuhusu ajali ni nini ndo swali gumu.
Sio swali gumu mnalifanya liwe humu wenyewe
 
Wewe umeelewa vizuri
Na mimi nataka kujua hiyo hali ya utambuzi wa mambo yajayo
inatokana na nini

Na unakuta sio kwamba inatokea mara moja moja kuota ndoto halisi ila inakua kama ni maisha yako
 
Akili ya mwanadamu yeyote automatically inajua kwamba kuna kufa.

Na inajua kifo kipo.

Kwa hiyo akili yako, inaweza kuota mtu yeyote amekufa kwa sababu tukio la kifo, Si tukio geni kwenye akili ya mwanadamu.
Mkuu, kwanini aote tu wakati kifo kinatokea na asiote siku nyingine? Kwanini ndoto isitokee wakati mwingine itokee wakati kuna mtu anakufa kweli? Kwanini matukio yafuatane yaani yeye aote na mtu afariki hapohapo? Hiyo coincidence na matukio kufuatana tena si mara moja ndo inazua maswali. Na mtu akiota hivyo moyo unakuwa mzito kabisaa ile hali anaihisi physically.
 
Shukrani so hua hizo ndoto zinatokeaje
Unaweza kitafsiri hizo ambazo hua ni kama ziko hidden
Mambo ya kiroho yanaendana na misingi yake, mfano pendelea kusoma vitabu vitakatifu.

Hivyo ndivyo vitakupa uwezo wa majibu juu ya kile unachokiona kwenye ndoto.

Mfano kwetu wajristu, tunaamini tukishampokea Yesu Kristu akaishi ndani yetu. Basi yeye atatutumia roho wake huyo atakuwa kiongozi wa maisha yetu.
 
Huo ni upande mmoja wa ndoto, na hayo sio maono. Ndoto zenye sura za watu unaowajua, na mambo uliyofanya au kuwaza mchana, sio maono. Hizo ni ndoto za dhamiri na nyingine ndo huitwa nightmare
Na wameshindwa kutofautisha hapa hapa hatuongelei hizo ndoto za stress na kazi za kila siku

Issue nikuota kitu ambacho hakijatokea na mwisho kinatokea vile vile
Tena kitu ambacho ukuwahi kuwaza
wala hukuwahi kukijua
Ndoto za maono, ni ndoto za hatma. Hizi mara nyingi huwa metaphoric, haziji na sura za watu unaofahamu na mara nyingi kama sio mara zote, haziji na tafsiri ya moja kwa moja.
MF kuota dawa fulani hujawahi kuisikia ila ndio mara yako ta kwanza katika ndoto then ukiuliza unaambiwa dawa kama hiyo ipo
 
Mambo ya kiroho yanaendana na misingi yake, mfano pendelea kusoma vitabu vitakatifu.

Hivyo ndivyo vitakupa uwezo wa majibu juu ya kile unachokiona kwenye ndoto.

Mfano kwetu wajristu, tunaamini tukishampokea Yesu Kristu akaishi ndani yetu. Basi yeye atatutumia roho wake huyo atakuwa kiongozi wa maisha yetu.
Asante sana
 
Ooh sawa Asantee

Kwahiyo ndoto ni matokeo au matukio ya kila siku ooh sawa sawa

Vipi kuhusu matukio tunayoota kwanza halafu baadae ndio yanatokea kwa namna ya kufikirisha ?
Sijui hata niseme vp uelewe
Kuna nadharia ya kifalsafa inasema kuwa muda siyo mstari ulionyooka kama tunavyouona, sisi huwa tunaona jana - leo - kesho lakini inawezekana fahamu zetu zina uwezo wa kugusa tukio ambalo lipo mbele kidogo ya huo mstari wa muda, naamanisha mbele kabisa ya kesho au kesho kutwa.

Kwahiyo ndoto zinaweza kuwa ni kuteleza kidogo kwa ubongo wako kuona kitu ambacho kipo kwenye future timeline yako, hapa siyo lazima iwe ni imani ya kidini, inaweza kuwa ni uwezo wa ubongo wako kuona probabilistic outcomes kabla hayajatokea kwenye uhalisia.
 
Back
Top Bottom