Kwa story za vijiweni.Kuna swali huwa ninalojiuliza sana peke yangu, naomba nishare hapa
Utasikia watu wakisema ulimwengu wa roho, ulimwengu wa siri. Hivi huo ulimwengu huwa ni upi?
Je, mambo ya ulimwengu wa roho au ulimwengu wa siri huwa ni pamoja na ndoto tunazoota usiku au mchana?
Au tuseme ndoto huwa ni dunia au ulimwengu mwingine?
Kwa sababu unapoota ndoto huwa ni kama upo kwenye ulimwengu au dunia nyingine. Maana unakuwa umelala, lakini ni kama bado kuna mambo yanaendelea kwenye akili yako
Wengine husema ndoto huwa ni matokeo ya mawazo, msongo wa mawazo uliozidi, maongezi au vitendo vya muda fulani
Ndiyo huwa ubongo unakuwa kama unarudi kwenye yale mambo
Mimi binafsi nakiri kuna ndoto zingine mtu huota huwa ni matokeo ya mawazo, shughuli za kutwa nzima au kile akili inachowaza au inachokitamani kifanyike
Unajikuta ukiota hivyo, na unapoamka unajua kabisa hizi ni fikra za mchana kutwa na mawazo tu
Au kuota mambo ya zamani, mfano shule, marafiki wa utotoni n.k. Na hii ya shule wengi wanasema wameota, ila mimi sijawahi kuota kabisa ndoto ya shule
Ninakuwa tu na ndoto zangu kivyangu, ambazo sioni hata watu wakizizungumzia
Swali linakuja kwenye ndoto ambazo nitaziita prophetic dreams, kwa sababu ni ndoto unaota kitu kitakachotokea mbele
Nasisitiza, kitu kitakachotokea mbele. Unakuta siku moja kabla au siku mbili kabla
Hii inanifanya nawaza sana, hivi huwa ni kitu gani kinatokea?
Yaani unaota ndoto kuhusu kitu fulani, halafu kikitokea unakuwa shocked 😲
Ukimwambia mtu haamini, anaona ni uongo, kama unapenda kujifanya special
Hivyo unabaki nayo mwenyewe
Pia kuna mtu ana uwezo wa kusoma mtu anachokiwaza
Yaani mfano ukiwa unachat na mtu unaweza ukawa unahisi huyu fulani ana nia fulani, aidha ana chuki fulani dhidi yangu, japo anaweza kuwa anapretend love
Na kweli hatachukua muda mrefu anajifunua rangi zake halisi
Lakini point kubwa hapa ni, inakuaje mtu anaota mambo yajayo? Ni nini huwa kinatokea??
Au huo ndio huitwa ulimwengu wa roho au wa siri?
Nitatoa mfano. Kuna ndoto niliota kuhusu watu fulani
Hao watu sikuwahi kuwajua kabla na hakuna namna ningewajua
Ila ajabu, hiyo ndoto niliyoota na majina yao kwenye ndoto, nilivyokuja kufahamu baadaye ilikuwa the same names
Yaani hata kama ningemwambia mtu asingeelewa, angesema nataka sifa
Niliwahi kuishi na mtu fulani
Huyo nilikuwa namwambia sana, Nimeona hivi katika ndoto kuhusu wewe,na kweli baada ya siku anakutana na situation kama hizo
Akawa ananiuliza, Wewe ni mganga au mchawi?😢😂
Ni mambo mengine mengi, ila hayo machache yanaeleweka
Je, kuna wengine wapo hivi?
Huota mambo halisi kabisa?
Nini sababu?
Faida au hasara?
Welcome Guy's
ShesRise_1 🤚
Kina nani walikudnganya nikinywa sipo sawa?Mambo yako ya kamnyweso 😂
ukiwa sawa karibu bwashee
Wanasayansi majibu yao ni mepesi sanaa tofauti na uhalisiaTatizo ni kwamba hata sayansi yenyewe bado haijatoa jibu la kueleweka kuhusu chanzo cha consciousness, wala haina majibu kuhusu kwa nini baadhi ya watu huwa wanapata experiences za aina hii.
Kasheshe aisee🤔 vicwa vitapasukakwahiyo tukisema tuseme tu kuwa ni suala ubongo tu hapa tutakuwa tunatoa majibu rahisi tukisema pia kuwa ni suala tu la ulimwengu wa roho , hili jibu nalo bado halijakaa vizuri.
Mimi nadhani hua tunakumbuka zile ndoto sensitiveCha kushangaza ni kwamba, huwa tunaota ndoto nyingi sana lakini tunajikuta tuna stuck kwenye ndoto moja tu kati ya nyingi ambazo tumewahi kuziota, na wala hauwezi kuzikumbuka hizo nyingine.
Mambo ni mengii aiseeeTuna
Na kibaya zaidi hatuwezi kutofautisha kati ya kitu kinachotokea kwenye ulimwengu wa roho na kitu kinachotokea kwenye deep subconscious processing ya ubongo wetu.
kifupi, kuna mambo kuhusu akili na consciousness ambayo bado hayajaeleweka kikamilifu.
Ooh sorry karibuKina nani walikudnganya nikinywa sipo sawa?
Nipo liveOoh sorry karibu
Kwa hii comment yako nimekushusha nyota mojaKwa story za vijiweni.
Wanasema mtu anapokuwa amekula sana chakula kingi usiku halafu muda ukiwa tayari unakaribia midnight ndipo anapokuwa kwenye nafasi kubwa ya kuota ndoto za ajabu ajabu kwa kile chakula kingi cha late nite hakina faida yoyote zaidi ya kusababisha imbalance tu
SafiiNipo live
kwenye huu uzi umeelezea vizuri zaidi Thread 'Fahamu zaidi kuhusu ndoto na ufahamu' Fahamu zaidi kuhusu ndoto na ufahamu
Ila nataka ulete challengeSafii
Casto laiti una madini tofauti na wajinga wengine wanaojisifia kulewa muda wote.Deja Vu au Maono ni halisi. Yako na binafsi ninayaamini.
kukubali au kutokubali kuwa mambo kama haya je ni ya kiroho, mawazo au intution ya mtu husika ndio hasa suala la kuhoji.
wanaoamin kuna Mungu watasema ni mambo ya kiroho na maono.
Wasioamini Mungu watasema ni mawazo yako ya mara kwa mara au ni pattern tu na Ubongo umetengeneza hilo tukio baada ya kuwaza sana.
Ila mm niko Upande wa Kiroho zaidi.
Kuna nguvu iko ndan yetu. Na sio Ubongo pekee.
Na ndio Maana kuna mambo ukiwaza sana huwa yanatokea.
Means you attract that energy. Iwe positive au negative into Life reality.
Ipi hiyo bwasheeIla nataka ulete challenge
Mkuu kwanini huo ujumbe uje ukiwa umefichwa?Ndoto za mambo yajayo ni matokeo ya ulimwengu wa roho. Hizi kwa jina lingine huitwa maono. Humtokea mtu akiwa hajawaza jambo lolote kuhusiana na ndoto husika, zenyewe huja kama ishara ya kukuonesha nini kinachoweza kukutokea, au kitakutokea siku za mbele.
Baada ya kuota hizo ndoto, linafuata jambo lingine muhimu, ambalo ni uwezo wa kuzitafsiri ujue maana yake, kwani sio zote huja na maana ya moja kwa moja, nyingine huja kwa namna ya kujificha hivyo lazima muotaji aweze kuwa na uwezo wa kuijua maana, au aulize kwa wengine ili aambiwe maana.
Naweza kuongezea kidogo...Kaka umeeleza vizuri mnoo utafiti zaidi unaitajika
shukrani mnoo
Kama kuna vingine vya kuongeza ongeza namatani kujua zaidi
Mkuu ndoto zinahitaji tafsiri kwa uzoefu wako kivipi huwa unaweza kutofautisha kati ya tafsiri sahihi ya kiroho na tafsiri inayochochewa na hofu au matamanio yako binafsi?Wanasayansi majibu yao ni mepesi sanaa tofauti na uhalisia
Kasheshe aisee🤔 vicwa vitapasuka
Mimi nadhani hua tunakumbuka zile ndoto sensitive
Mambo ni mengii aiseee
Extra sens inachota taarifa zake kutoka wapi?Katika mwili wa binadamu Kuna vitu vingi bado havijagunduliwa jinsi vinavyofanya kazi...
Mfano Ubongo wa binadamu ni very complex kiasi kwamba..ugunduzi wa mambo mbalimbali bado unaendelea kuvumbuliwa..
Ndio maana ndoto binadamu anazoota Kuna vitu vinafanyiwa research...
Kuna watu wakiota ndugu yake labda anaumwa... Kesho yake wakipiga simu wanaambiwa alikuwa hoi kapata nafuu
Au hata sio ndoto tuu.. Kuna watu Ubongo unampa hisia tuu..ondoka hapa.. baadae mnasikia sehemu imevamiwa au Kuna shida imetokea eneo Hilo
Ila sio Kila mtu Ubongo wake unaweza haya mambo.. na ndio maana Kuna tafiti zinafanyika ili kujaribu kuangalia Ubongo wa binadamu na mazingira yake
Wataalamu wa tafiti wanasema Kuna extra sense..(mlango wa ziada wa fahamu) hasa ndoto au hisia ya kitu ambacho ukioni lakini Ubongo unakupa taarifa hasa katika hali ya utulivu sana
Nani anawajibika kwa yale mabaya yanayowapata watu wasio na hatia?Means you attract that energy. Iwe positive au negative into Life reality.
Hapo kwenye hisia ya kupata tatizo.. ujue Hilo tatizo lipo...Extra sens inachota taarifa zake kutoka wapi?
Unawezaje kutofautisha kati ya extra sense na anxiety?
Kwasababu mara nyingi watu huwa wanapata hisia kwamba labda kuna tatizo lakini hilo tatizo likaacha kabisa kutokea.