Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Nimenunua plot Dar miaka 5 iliyopita sijajenga hadi leo nimejaribu kuuza bei iko chini ya nilichonunulia
Nimewaza kujenga naona gharama kubwa sana na hela zangu hazitarudi

Pole chief wengi wako katika dilemma kama yako, wengi sana, tafadhali fata ushauri wa Witmak255
 
Umepata hiyo pesa, yote Ukaizike!? Huo ni wendawazimu wa hali ya kutosha. Kama unawashwa na kujenga, toa hats mil 30 ukajenge nyumba iishe kabisa uhamie hiyo nyingine iweke kwenye mzunguko wa biashara ya kuaminika na uifanye wewe mwenyewe.

Nilishasema sitokaa niyaogope maisha nikimbilie kuizika pesa(kujenga) niache kuiweka kwenye biashara kwa kuogopa kupanga.

Chukulia mfano, umeenda kujenga Mbande au Kisewe huko Mbagala, shughuli zako ziko Tegeta na huko ndiko ulikokuwa umepanga mwanzoni.
 
Jaribu biashara uingizwe mjini upoteze zote ili uanze upya kuliko kupokea 6k monthly
Na hii ndio hofu yetu watanzania wengi.
Huwa hatujiamini kwenye biashara,lakini sababu inatokana na lack of business knowledge.
Ndio maana wote tumekuwa na utamaduni wa kujenga tu au kuziacha hela benki kwenye saving account.
Ila wahindi huwa hawana hobby ya kujenga majumba wapatapo pesa Wana njia zingine za investment Kama kununua bonds/shares au other liquid assets Kama golds na kuzihifadhi ndani.
Siku akifirisika anauza kwa Bei ya juu na kuibuka tena.
 
Kwa hiyo TZS 150,000,000 ukiwekeza kwenye nyumba na ukawa unapata TZS 7,200,000 watoto wako wawili wana uhakika wa kusoma mpaka chuo kikuu bila bugtha ya kukwama ada hata kama Mungu atakuwa amekupenda zaidi
Hutakuwa na stress hata ukiwa kwa grave huko[emoji3]
 
Kuna mmoja yeye ni dereva kwenye ubarozi wa nchi ya kibeberu flani. Amechukua mkopo milio 30,
Akanunua gari Subaru foresta nyingine akaanza kujengea saa hizi hiyo nyumba kaishia kupaua na hela naona imekata.
Hizi ni hesabu kichaa ambazo watumishi wengi huwa wanaangukia pua.
Ananunua Subaru kutia kishoka halafu nyumba ya kulala hana.
 
investment kwenye real estate inalipa,sema inategemea umejenga wapi.kwanza lazima uwe na mtaji wa kutosha,lazima ujue unakwenda kujenga wapi.kuna jamaa amejenga sehemu vijumba vingi sana ni vizuri kweli ila kavipeleka ndani sana,zile nyumba wameishia kupanga watu wa kipato cha chini.usijenge nyumba ya kupangisha sehemu ambako mji ndio kwanza unaanza hiyo itakula kwako.

Boss wangu anafanya real estate investment,yeye ananunua sehemu ambayo ahata akijenga godown ,lazima waje watu wenye pesa kupanga pale kama ni nyumba basi utaskia either ubalozi wamepanga pale
 
Hao ndio utakuta akikamata raia wanawatesa kwa kujificha kwamba raia wamekiuka sheria za jeshi kumbe ni stress.
Hebu mwambie aniuzie hiyo ist yake
Wala usiwaze kuhusu huyo mjeda, anaweza uza hyo Ist akamalizia nyumba nyingine akaingia mtu, mara paaap kapewa jukumu Congo, Darfur anaomba uzima tu akirudi kakupiga gape la hatari
 
Ukitaka kujua km Pesa ni Snitch, pata hizo mil 150 hlf puuzia kujenga nyumba ya kupangisha kwavile utachelewa kupata return yako hahaa uje kushtuka wakati unatafakari biashara ipi nzuri zaidi mwaka umeisha na mil zmebaki 50 [emoji3]
Hapo ndo utajua Pesa thamani yake ni hata kuangalia tu nyumba uliyijenga hata km haiingizi chochote.
PUMBA ya Kufungia Mwaka 2019
 
Nilikua nalipa nyumba laki 6 mwaka 2016 Mikocheni nimehamia Sinza kodi 250,000/= Tshs. Toka nimehama Mikocheni ile nyumba mpaka Leo haijapata mtu. Mwenye nyumba ananipigia simu nirudi atanipunguzia kodi 50% (300,000 Tshs.) Ha ha ha!

Sinza kodi 250,000/=?utakuwa unaishi kwenye nyumba za ajabu ajabu one bedroom jiko nje...
 
Hizi ni hesabu kichaa ambazo watumishi wengi huwa wanaangukia pua.
Ananunua Subaru kutia kishoka halafu nyumba ya kulala hana.
Wala usimcheke na kumbeza ni hatua muhimu kwenye maisha hela isipopotea hutajua thamani yake na ndo shida ya elemu ya mtaaani au maisha kuipata gharama zake ninkubwa sana trust me iko siku utarudi hapa na kutueleza jamaaa wa subara kazishia mafumba ya hatare kbs
 
Real Estate ndio sekta pekee duniani kote inayichangia KWA kiasi kikubwa ili nchi husika ionekane kuwa imeendelea. Unapofika ktk nchi yoyote ile indicator ya kwanza kukujukisha kuwa nchi husika imeendekea ni kuangalia maendeleo yake ktk delta hii ya real estate, e.g, ubora wa majengo, ukubwa wake mpangilio wake ktk ujenzi, n.k.

Tatizo kubwa ktk sekta hii ni kuwa, initial capital/cost for investment ni kubwa sana,hilo tu ndio tatizo lake.
Lakini ukiwekeza ktk sekta hii uhakika wa kupata returns ni mkubwa, tena ni investment ya milele, na risk yake ni ndogo ukilinganisha NA aina nyingine za investments.
 
Na hii ndio hofu yetu watanzania wengi.
Huwa hatujiamini kwenye biashara,lakini sababu inatokana na lack of business knowledge.
Ndio maana wote tumekuwa na utamaduni wa kujenga tu au kuziacha hela benki kwenye saving account.
Ila wahindi huwa hawana hobby ya kujenga majumba wapatapo pesa Wana njia zingine za investment Kama kununua bonds/shares au other liquid assets Kama golds na kuzihifadhi ndani.
Siku akifirisika anauza kwa Bei ya juu na kuibuka tena.
Nimeanzisha biadhara 12 na zote zimebuma na bado nadunda ni,ejifunza mengi sana
 
Back
Top Bottom