Je ni chakula gani cha kustaajabisha umeshawahi kula? Nilikula ugali wa maembe.

ubunifu muhimu kwanini tupambane kula tuu vyakula vilivyo asisiwa na wazee
Kuna jamaa kutoka Ghana amefungua mgahawa Paris anauza mboga za wadudu aina mbalimbali kutoka Ghana
Kwa sasa ana wateja wazungu wengi sana
Food of the future ndio mpango mzima wa kula
Duniani zimefunguliwa nyingi sana kuanzia London, Berlin, NY, na Asia ndio Usiseme maana ndio wanakozaliwa hao wadudu
 

Attachments

  • IMG_3817.jpeg
    43.1 KB · Views: 13
Kuna jamaa nilimuona anakula ugali na nyanya ya kopo miaka ileee
Na dereva mmoja aliangusha container njiani akielekea Zambia
Ilipofika usiku wakasikia njaa na kuanza kufungua makopo
Walikuta nyama ndani wakaanza kula ni utamuu
Asubuhi wanakuja kukuta walikuwa ni vyura
 
Kwa mara ya kwanza nimekula senene simply kwasababu ya kufukuzia nyapu (uhayani kwa nshomile) ,ujana una mambo yake aseee!

Mwaka huu kwa mara ya kwanza nimekula jamii ya nyoka (kamongo) ujitani hukoo wao wanadai ni samaki
 
Loshoro nilikula kwa kujilazimisha kwasababu ilikua ukweni...
 
Mimi nimeshuhudia dogo akila ukali na mafuta ya alizeti, mwingine ,ugali na nyanya mwaka jana tarehe 2 mwezi wa10 na mimi nilienda sehemu kwa mara ya kwanza nakala ugali tena kiporo kwa chai ya rangi
 
Mimi nimeshuhudia dogo akila ukali na mafuta ya alizeti, mwingine ,ugali na nyanya mwaka jana tarehe 2 mwezi wa10 na mimi nilienda sehemu kwa mara ya kwanza nakala ugali tena kiporo kwa chai ya rangi
Hilo la ugali kwa kutoeza mafuta ni jambo la kawaida.

Usukumani ugali unatoezwa samli na mtu anashiba.

Ugali kwa nyanya ni kawaida sehemu zenye uhaba wa mboga.

Halafu ugali na chai ni kawaida.
Mkuu umeshangazwa na vyakula vya kawaida visivyoshangaza ujue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…