Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Habari ndugu Wanajamii Forums. Nimeona nije kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalam wa mambo ya usalama barabarani.
Kwa ufupi nilikuwa na safari kutoka Mkoa mmoja kwenda mwingine huku nikitumia usafiri wangu binafsi. Kiukweli njia nzima changamoto zilikuwa ni nyingi kutoka kwa hawa askari wetu wa usalama barabarani. Changamoto mojawapo ilikuwa ni ile ya kuviziana na tochi kwenye yale naeneo ya 50/KPH! Hapa niliwashinda.
Changamoto nyingine ilikuwa ni ile ya kusimamishwa na kuulizwa leseni yako, kukaguliwa bima kupitia mashine, kukaguliwa kama gari inadaiwa, nk. Na hapa pia nilikuwa mshindi.
Jambo lililonifanya kuanzisha huu uzi sasa ni hili suala la askari mmoja wa eneo fulani katika hiyo safari yangu, kunisimamisha na baada ya kukagua gari na kukosa makoda mengine; akanitia hatiani kwa kosa la kutokuwa na sticker ya nenda kwa usalama barabarani. Huyu askari nilibishana naye kwa muda mrefu pasipo na mafanikio! Na mwisho wa siku akalazimisha kuniandikia hiyo faini ya elfu 30.
Kwenye maelezo yake wakati tunabishana, aliniambia eti hizo sticker zinatolewa kituo cha polisi na mtu anayeitwa VECO! Na kwa hiyo kila dereva/mmiliki wa gari anatakiwa kwenda kituo cha polisi na gari lake ili likaguliwe, ndipo apewe hiyo sticker ya nenda kwa usalama!!
Sasa maswali yangu kwenu wanajukwaa ni haya hapa;
1.) Je, huyo VECO ana uwezo wa kukagua magari yote nchini na hivyo kuyapatia hizo sticker za nenda kwa usalama?
2.) Je, ni halali askari wa usalama barabarani kunitoza faini ya elfu 30 kwa kukosa hiyo sticker? Au na hii ni njia mojawapo ya kukusanya mapato ya serikali kupitia mifumo kandamizi na ya hovyo?
3.) Na kama hizo sticker zina ulazima kwa kila gari, ni kwa nini zoezi lisifanyike barabarani ambako magari ndiyo hutembea, badala ya kuwataka madereva/wamiliki wa magari kwenda kwenye vituo vya polisi (tena ni kuanzia vile vya Wilaya) kuwaona hao VECO! (Na mbaya zaidi siyo mara zote utawakuta huko vituoni) Ili tu kununua hizo sticker! Halafu ukimkosa, unaishia kuandikiwa faini? Kwa nini jeshi ka polisi linatengeneza mazingira ya aina hii kwa wamiliki wa magari?
4. Huu mradi wa sticker za nenda kwa usalama ni wa nani? Maana miaka nenda tunalazimishwa tu kuwa na hizo sticker, huku magari yenyewe yakiwa hayakaguliwi! Na badala yake watu wamekuwa wakiuziwa hizo sticker kwa bei ya ulanguzi na hao polisi?
5.) Je, serikali ya CCM hamuwezi kutuondolea huu uonevu tunaofanyiwa wamiliki wa vyombo vya moto, hususani wamiliki wa magari? Maana tumekuwa sasa kama ng'ombe wa maziwa kutoka kwenu na pia kutoka kwa hawa askari wenu wa barabarani!!
Kwa uonevu wa aina hii nikiichukia serikali na pia hawa askari wapenda rushwa, mtanilaumu kweli!!
NB:- kuna kijana wa mwaka 2000 anaweza kuja kuniponda kwa kulalamikia faini ya elfu 30!! Hajui hiyo hela ni bora mara mia ningeenda kunywea pombe, au kwenda kununulia nyama ya swala! Kuliko kuitoa kwa watu wasio na faida.