Je, ni halali kwa askari wa usalama barabarani kuwatoza wananchi faini ya 30,000/= kwa kutokuwa na sticker za nenda kwa usalama?

Muwe mna wagonga wakifa faini ni 50k tu road accident haina kifungo jela... Hakuna faini ya 30k ukiwa huna sticker
 
😁 Kuna gari za kukagua hiyo Sticker... nasubiri siku traffic police aniulize swali la kijinga kama hilo.

Labda nikiwa naendesha Mkweche... kweli kweli.

The fact ni kwamba unaweza kuwa na Sticker lakini gari ilipatq changamoto baada ya ukaguzi. Sticker ni valid ila chombo kina dosari.

Vitu ambavyo sina ujanja na sina ktk gari kwa sasa ni Fire extinguisher, Reflector ile ya pembe 3 hapo wakinidaka wakauliza hivyo vitu sina.. nitatafuta.
 
Tumewalea hawa wadudu kwa ujinga wetu.
Tunajifanya kuokoa muda siku moja ili tuteseke sisi na vizazi vyetu.

Huwezi amini kwangu mimi hasa maeneo ninayopita kila mara asilimia 70 wamenielewa msimamo wangu na hawanisimamishi hovyo...akinidimamisha sio kudumbua labda atsomba ndg...leo niko vibaya nisaidie ya chai.
Sio kwamba najitutumua hapa ...hapana niko very serious na hili...niko tayari tusumbuane saa 1 leo kwa ukombozi wa siku zijazo.

Ni wajinga wachache ambao bado hawajanielewa katika barabara yangu ya kila siku.

Wananiita mtata..na nitakuwa mtata wa wajinga siku zote.
 
Tumewalea hawa wadudu kwa ujinga wetu.
Tunajifanya kuokoa muda siku moja ili tuteseke sisi na vizazi vyetu.
Wapo kisheria boss. Kama ni lawama ziende bungeni na serikalini.
Siwapendi Trafiki sababu wapo wengi mno barabarani na hatuna utaratibu maalum wa ukaguzi, hii inasababisha kukaguliwa hapa na kusimamishwa tena pale kwa ukaguzi siku hiyo hiyo ila tatizo halipo kwao lipo kwenye mfumo wetu unaowaruhusu wao kuwepo barabarani kwa huo mtindo.

Hakuna ukombozi wowote utakaouleta mkuu kwa kugombana na Trafiki lisaa lizima. Ukombozi unapatikana kwenye sheria zetu. Sasa yeye akienda kwenye sheria anakulima faini ukapambane nayo baada ya kugombana naye lisaa lizima.
Ni wajinga wachache ambao bado hawajanielewa katika barabara yangu ya kila siku.
Mkuu, Trafiki huwa wanabadilishwa maeneo baada ya kipindi halafu pia huwezi endesha gari mitaa ya kwenu tu lazima tu utatoka maeneo mengine ya wilaya au mkoa.
Wananiita mtata..na nitakuwa mtata wa wajinga siku zote.
 
Najua nisemalo mkuu.
Mfano mzuri barabara yangu ya kila siku nimezoeleka hivyo karibu mwaka mzima huwa sikaguliwi hovyo.
Pili...ni kweli lazima nisafiri, hata hivyo mimi ni mtu wa kusafiri sana kutokana na nature ya kazi yangu.

Huko huwa nina silaha nyingi za kupambana kama hivi:
1. Upole hii silaha ya kwanza.
Namsikiliza anachotaka, nami nachagua neno la kiungwana la kumjibu.
2. Kutumia sheria za barabarani.
Kwa mfano nimesahau leseni analazimisha anipige faini..hapa natumia sheria isemayo...nina haki ya kuleta leseni ndani ya saa 72.

3. Nikikutana na mbabe asiyesikilizs hapa nina silaha zangu....( hii huwa haishindwi....nikilazimika huwa nampandia juu, yaani kwa wakubwa zake ambapo kamwe hawezi kujinasua hasa ikiwa hayuko sahihi)

Mwisho...nikiwa na kosa huwa ninakubali kuwajibika lakini sio kuonewa
 
Najua nisemalo mkuu.
Mfano mzuri barabara yangu ya kila siku nimezoeleka hivyo karibu mwaka mzima huwa sikaguliwi hovyo.
Pili...ni kweli lazima nisafiri, hata hivyo mimi ni mtu wa kusafiri sana kutokana na nature ya kazi yangu.
Umeona mkuu, kama unasafiri hawakwepeki.
Upo sawa.
 
Mkuu uko kama Mimi,ni mwendo wa Tano elfu tu,trafiki anakagua Hela siyo gari,km uliweza kununua gari, wape trafiki elfu Tano acha ubahili
 
Da nchi yangu na watu wake. Hivi hakuna tiba ya kumaliza huu ugonjwa badala yake unaelekeza atumie vidonge vya kuendeleza siku za kuishi ukikamuliwa kipato.
Tukajiandikishe kupiga kura wajamen
 
Dah! Pole sana. Mimi natakiwa kulipa elfu 30 ya faini, na bado natakiwa tena kwenda kituo cha polisi kumlamba miguu VECO ili aniuzie hiyo sticker!!

Hii nchi inahitaji mabadiliko aisee.
 
Sawa wanakosea lakini mbona wakati wa mwanzo wa wiki ya nenda kwa usalama zilikua nyingi tu na zinapatikana kwa urahisi.
Kwa hiyo Comrade ingewezekana kweli wa wananchi wote wa nchi hii kuhudhuria hiyo wiki ya nenda kwa usalama, ili kupata hizo sticker? Nchi kubwa sana hii!

Sisi wengine tunaishi vijijini na tuna majukumu mengi. Hivyo siyo rahisi kusafiri kwenda mjini kuhudhuria hiyo wiki. Mimi nashauri askari waendelee kuwa nazo barabarani. Na kama nitasafiri na gari langu, alikague! Akiona lina sifa anipe hiyo sticker! Na siyo kuviziana na kupigana faini za kipuuzi.
 
Ona sasa! Mambo gani haya!! Polisi wa nchi hii ni viumbe wenye roho mbaya sana. Halafu siyo waelewa hata kwenye mambo ya kawaida kabisa.
 
Faini za makosa barabarani kwa gari linaanza Tsh 30,000.
Na hata mimi pia nimepigwa faini hiyo hiyo kwa kukosa hiyo sticker! Je, kuna ulazima wa wamiliki wa magari kulazimishwa kuwa na hizo sticker na wakati ukija kwenye uhalisia hakuna ukaguzi wowote ule unaofanywa kwenye magari yetu? Huu si wizi wa mchana kabisa!
 
Ni kweli ila kwa Nchi mfano Tanzania kila kitu ni fursa hapo washaifanya kua ni fursa kwao.
 
Shida iliyopo, mimi nipo kijijini Comrade. Sasa nilipata safari ya kwenda Mkoa mwingine. Nikajiandaa kwa kila kitu. Kuanzia Bima, nk. Hayo mambo ya sticker ni mpaka uende kwa VECO ngazi ya kuanzia Wilaya huko! Jambo ambalo linatuwia vigumu kwa sisi watu wa pembezoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…