Kwa wale waliosoma fire and rescue services, moto una tafsiri yake kisayansi. Watu wengi wanaujua moto na infact wanautumia katika maisha ya kila siku lakini ukimuuliza mtu moto ni nini atapata ugumu kujibu.
Ni katika tafsiri ya moto ndipo jibu la swali lako lilipo.
Kisayansi moto ni hali inayotokea vinapokutana vitu vitatu i.e
1. Oxygen(kati ya asilimia 16 na 18)
2. Heat (zaidi ya degree za centigrade 65), na 3. Fuel (chakula cha moto) si kwa maana ya mafuta pekee, inaweza kuwa karatasi, mbao, kitambaa nk nk.
Ikitokea moja kati ya hivyo vitatu hakipo au kikapungua upatikanaji wake, moto hautawaka.
Kwa hiyo dhana ya “zimamoto” huwa ni kudhibiti moja kati ya hivyo vitatu au vyote ili moto usiendelee kuwaka.
Ukitazama hizo components za moto utagundua kuwa maji huwa yanaathiri joto (kulipunguza) hivyo basi, joto likiathiriwa na maji na kuwa kuwa chini ya 65 degrees (C) moto hautakuwa moto tena.
Hiyo ndiyo sababu kuu moto hauwezi kuyaunguza maji, na ndiyo maana maji yanatumika kuzima baadhi ya aina za moto japo si zote.