Je, ni kwanini Ugonjwa wa Kansa, Figo, Ini unaonekana kuwa ni tatizo Tanzania ?

Inawezekana ikawa kweli kuhusu hizo Pombe za bei rahisi lkn wagonjwa wa figo asilimia kubwa ni watu wakipato cha kati na visungura ni kilevi cha watu wa kipato cha chini.
Utafiti huu umeutoa wapi?

Wanywaji visungura kwa kujitetea hamjambo 🤣
 
barikiwa sana ndugu, pia kuna mchangiaji amesema katika moja ya comment kuwa ulaji wa unga mweupe [sembe] na carbonated drinks ni miongoni mwa sababu ya chanzo cha magonjwa hayo yaliyotajwa kwenye hii mada. Vp unaweza ukatupa elimu ili tuweze kujiepusha tafadhali.
 
Sembe inaweza kusababisha matatizo ya Figo kama ukiila kupita kiasi kwakuwa ukiila kupita kiasi sukari itazidi mwilini hivyo kusababisha Figo kufeli. Wanga huzalisha glucose mwilini ambayo ni sukari hivyo hata dona au wali ukiitumia kupita kiasi kuna chances za kupata kisukari.

Kwaupande wa ini sembe inaweza kuleta madhara kama ilihifadhiwa vibaya au ilisindikwa pamoja na kemikali zilizotumika kwenye kilimo kama vile dawa za kuulia wadudu. Uhifadhi vibaya wa sembe huzalisha sumu iitwayo aflatoxin ambayo inaweza kusababisha saratani ya ini.

Kwaupande wa carbonated drinks zina uwezo wa kuharibu ini na Figo kama utazitumia bila mpangilio mzuri kwakuwa zinakemikali na sukari inayoweza kusababisha magonjwa ya ini na Figo.
 
Asante kwa muda wako, nadhani nimtafute mtu wa kunifundisha namna ya kupunguza sumu mwilini kisayansi ili kuwa salama.
 
Suala hili ni serious Sana kuhusiana na maisha ya Sasa. Vyakula vingi Sana tunavyokula ni artificial and processed foods. Huku mamlaka za udhibiti ubora na viwango zikiwa ziko hoi bin taabani.

Jaribu kufikiria tukio baya Kama hili kwenye hii video hapa chini, it's terrible!
 

Attachments

  • 5929966-5358adcd11ca564ef6ab279deb233ae9.mp4
    14 MB
Population control ni Siri ya viwandani!!hata america ni
hivyo!!
Green tea without sugar is the best!!
 
Mtu analima shamba kubwa la hekari 1-2 ale kipande cha mhogo hapo ni kama mzaha
 
Asante kwa muda wako, nadhani nimtafute mtu wa kunifundisha namna ya kupunguza sumu mwilini kisayansi ili kuwa salama.
Sawa.
Ila moja ya njia ya kupunguza sumu mwilini yaani detoxification ni kutumia ndimu au limao aidha kwa kuweka kwenye chai au kunywa kama juice. Pia usisahau mazoezi.
 
Si wanauza za kisuna ili waongeze nguvu za kuwakomoa wanne,, haya unafikiri figo inaspea?

Si viwanda vya energy vinazidi kupngezeka na vijana wanabugia wakidhani ni juice? Chigende go
 
Upo sahihi kabisa.
Dr. Janabi naye ni miongoni mwa tatizo, yafaa tumuunganishe na TBS pamoja na TMDA.

Hivi kweli mtu ushindie kipande cha muhogo ama maji si utajikuta trip 2 barabarani trip 2 hospital.

Utapiamlo.
 
Kati ya dona na Sembe Basi Dona ndo mbaya ... Ndo maana mikoa inayoongoza kwa Kansa ni Mikoa kanda ya ziwa
Mkuu dona ni bora kuliko sembe kwakuwa inanyuzi nyuzi na madini ya kutosha kuliko sembe.
 
Sahihi, Regulatory ndio mpango mzima

REFORMS NI LAZIMA
MKuu shukurani na bandiko lako.

Kwa Batanzania wenzangu

mtumie rafiki wako kwenye grupu lako iwe ni feisbook ,enstagraam,whatsup, x, JF. Ujumbe huu mzito.

Vilevile umpigie simu Mbunge wako umwambie asipo weka hili suala kwenye vipaumbeke vyake vya bunge lijalo, kura hapati. Simple as that.

Hatuezi endelea na vifo visivyo vya lazima. We can't be complacent.

kwa wenzangu wa CHADEMA, haya ndio masuala tunapaswa kuwaambia Wananchi. Tuchukue wasaa na ramli hii kama sehemu ya sera zetu.


Reform ni Lazima

Hakikisha unaweka na link hii ya huu Uzi huko

Jamani hatuwezi kukaa kimya na hili.

#REFORMNILAZIMA
 
Wazeee wetu wameishi kwenye mchele ngano na dona plus mbege miaka yao tisini. Zote hizo ni carbohydrates leading to glucose.

With all that ,,Hawajui sukari, presha wala figo, wengi wqmekufa just for old age

Iweje nyie vijana wa 30 na 40 to 50 , ulaji wa ngano sembe na dona na mchele iwaletee figo na sukari

Unaweza kutoa Data to support your claim , mind that everything in excess is harmful including water
 
Wazeee wetu wameishi kwenye mchele ngano na dona plus mbege miaka yao tisini. Zote hizo ni carbohydrates leading to glucose.

With all that ,,Hawajui sukari, presha wala figo, wengi wqmekufa just for old age

Iweje nyie vijana wa 30 na 40 to 50 , ulaji wa ngano sembe na dona na mchele iwaletee figo na sukari

Unaweza kutoa Data to support your claim , mind that everything in excess is harmful including water
 
Mnaishi kama machokoraa au mbwa waliokosa mfugaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…