Je, ni kwanini viongozi wengi na Taasisi nyingi hasa za Serikali hawapendelei sana kufanyia kazi Tafiti zinazofanyika hasahasa vyuo vikuu?

Je, ni kwanini viongozi wengi na Taasisi nyingi hasa za Serikali hawapendelei sana kufanyia kazi Tafiti zinazofanyika hasahasa vyuo vikuu?

Heaven Seeker

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2017
Posts
479
Reaction score
1,071
Kwa taarifa tu ni kwamba, Wakufunzi ( Wahadhiri) wa Vyuo mbalimbali hasahasa vyuo vikuu, mojawapo ya majukumu yao ya msingi ni kufanya Tafiti mbalimbali. Ukiangalia kwenye google scholar kisha ukaanza kutafuta research zilizofanyika hapa nchini na wahadhiri wetu, utakutana na utitiri wa tafiti nyingi sana kwenye journals mbalimbali. Hata tu ukitembelea kwenye websites zao za vyuo wanavyofundisha utakutana na tafiti nyingi sana ambazo zimefanyika.

Kikubwa zaidi, ukisoma hizo tafiti utakuta zimetoa recommendations mbalimbali kutokana na tafiti husika kuwa ni kipi kifanyike.

Hakika kama kweli sisi kama nchi, tungeamua kufanya mambo yetu kwa kuzingatia tafiti zilizofanyika, tungekuwa mbali sana, maana mambo mengi yangefanyika kitaalamu na tungekuwa tumepiga hatua kubwa.

Chakushangaza, ni nadra sana kumsikia kiongozi wa Serikali, awe wa kisiasa au wa Taasisi flani akitoa maelezo au amelekezo kwa kuanzia na maneno kama ''kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka flani kuhusu kitu flani, ilibainika kuwa changamoto kubwa ya jambo flani ni kutokana na sababu kadha wa kadha na hivyo tumeamua kuanza utekelezaji wa mapendekezo kulingana na utafiti huo kwa kufanya jambo moja mbili tatu''. Yaani unakuta kiongozi anaongea mambo muhimu sana kuhusu sera au utekelezaji wa mambo muhimu yanayowagusa wananchi kwa maoni yake binafsi tu.

Hata watunga sheria huko Bungeni ni nadra sana kuwasikia wakizungumza kuhusiana na utafiti wowote uliofanyika. Hii kwa maoni yangu ni kuamua kufanya mambo kienyeji sana. Huenda Serikali ikawa inatekeleza baadhi ya mapendekezo ya Tafiti hizi, ila nina mashaka makubwa kama huwa wanafanya hivyo kwa kiwango kikubwa.

Nchi za wenzetu, unakuta wana Taasisi maalumu ya kufanya analysis ya research zinazofanyika, na baadhi ya lecturers wanafanya kazi Vyuoni na pia kwenye Taasisi nyingine za Serikali za kuchakata sera za nchi kulingana na Tafiti zinazofanyika, kisha wanaishauri Serikali nini kifanyike.

Sisi tunafeli wapi? Shida haswa ni nini kwani? Kwanini tusitekeleze mipango yetu kwa kuzingatia tafiti za wasomi wetu zinazofanyika kwa gharama kubwa hapa nchini? Nini umuhimu wa hizo tafiti kuendelea kufanyika?

karibuni kwa mjadala.
 
sana sana pale chadema inapoishauri ccm .
 
Tz siasa ndio kila kitu. Mwanasiasa, licha ya ukweli na uhalisia kuwa ni mtupu kichwani, atakachosema huwa. Bahati mbaya, wao ndio wanaongoza kila idara.
 
Tz siasa ndio kila kitu. Mwanasiasa, licha ya ukweli na uhalisia kuwa ni mtupu kichwani, atakachosema huwa. Bahati mbaya, wao ndio wanaongoza kila idara.
Mkuu vipi kuhusu wawakilishi wa wananchi (Wabunge)? wanapokuwa bungeni kupitisha maazimio mbalimbali ni nadra sana kusikia wakisema wanatoa maelezo yao kulingana na tafiti za kitaalamu zilizofanyika huko nyuma.
 
Kwa taarifa tu ni kwamba, Wakufunzi ( Wahadhiri) wa Vyuo mbalimbali hasahasa vyuo vikuu, mojawapo ya majukumu yao ya msingi ni kufanya Tafiti mbalimbali. Ukiangalia kwenye google scholar kisha ukaanza kutafuta research zilizofanyika hapa nchini na wahadhiri wetu, utakutana na utitiri wa tafiti nyingi sana kwenye journals mbalimbali. Hata tu ukitembelea kwenye websites zao za vyuo wanavyofundisha utakutana na tafiti nyingi sana ambazo zimefanyika.
Umegusia jambo muhimu sana sana.
 
Karibu mkuu. Utupatie pia maoni yako kuhusiana na jambo hili. Tunakwma wapi?
Nachelea kusema chochote kuhofia nitaharibu andiko hili zuri.

Ila niseme tu kuwa tatizo kubwa mpaka hawa viongozi hawafuati mapendekezo ya kisayansi ya wasomi wetu ni kuwa hakuna mwenye uchungu na Tanzania 🇹🇿 yetu, ukimwona mtu anadai kuwa na uchungu jua kuwa maslahi yake ya kiuchumi yanakwenda sambamba na ‘status quo’

Hawa watu wangelikuwa na uchungu, na ile hali kuumia kwa hali tuliyonayo hakika wangefanya makubwa sana, ila hakuna. Hakuna mtu anayeona yeye ni Tanzania 🇹🇿, kila mtu anaona Tanzania 🇹🇿 ni ya mwingine hivyo anaweza fanya anachotaka kwakuwa si mali yake.

Ndiyo maana hawajali hili wala lile, wanachoangalia ni kuendelea kukaa kwa muda mrefu zaidi kadri inavyowezekana.
 
Wivu, ujinga na umaskini vinatufanya tudharauliane sembuse kugusia mambo nyeti kama hayo wanaona kana kwamba ni kumpa credit mtafiti.
 
Back
Top Bottom