Je, ni kwanini wachezaji washiriki wa CAF Champions Ligue hawachezi EPL (England Primier Ligue?)

Wewe unaichukulia ahly poa kumbe kwa taarifa tu hiyo club inafikaga hadi nusu fainali kombe la vilabu la dunia.
 
Ligi za kati kama Uturuki Sweden Norway Poland etc Mayele, Feisal, Baka, Mudathiri wanacheza vizuri tu..
Tena hawahitaji Majaribio.

Kuna mambo mawili hapo;
Kuwa na uwezo wa kucheza ni jambo moja, Kuweza Kuaminiwa na kocha ni jambo jingine nalo ndio gumu zaidi (refer history ya okocha)

Enock Inonga ndiye mchezaji pekee kutoka ligi za Afrika aliyefanikiwa kuaminiwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya DRC...akiwaweka benchi mabeki wenye profile ya juu wenzie kutoka ulaya.

Ukiwatoa kolo Toure na Amri Zaki Sina kumbukumbu kama kuna mchezaji mwingine aliyewahi kutoka CAF CL kwenda EPL moja kwa moja na kupata namba.
Toure alitoka Asec akasajiriwa Arsenal moja kwa moja na kupata namba.

Amri Zaki yeye alisajiriwa Wigan kutoka Zamaleki na kuaminiwa kuanza kwny first 11.

Ni nadra sana kuondoka Afrika ukiwa na over 23...na ukawa star ulaya..

Andre Onana kaondoka Cameron akiwa na 16...Victor osimhem, Drogba na Etoo wametoka kwny nchi zao wakiwa watoto sana.
 
Mpira wa ulaya unahitaji mambo mengi Sana. Wenzetu wanaamini kwenye umri, saikolojia ya mchezaji, historia ya mchezaji/taiga, malengo ya mchezaji nk.

Leo hii Samata anaonekana mwamba Tz, kwa kuifunga Liverpool na Man city. Yeye mwenyewe anaweza akawa anataja kama moja ya mafanikio yake. Wazungu wanahitaji watu wanaowaza vikombe vikubwa kwaajil ya timu. (Sio mchezaji na taifa lake)
 
Ila sii uliona jinsi game lilivyobadilika second half sevilla wakafanya yao.
Wee bwana levels tofauti hizo wale na huwezi kupima nguvu na timu kwenye friendly wachezaji wanajua jinsi ya kujipace kwenye mechi za kirafiki
 
Noted,. Nimepata cha kwenda kupigia kelele kijiweni leo
 
Dakika 90 za mechi ya EPL ni sawa na dakika 270 za CAFCL huyo kibabage sijui Aziz K akicheza EPL ile GPS itamcount kama mzururaji tu uwanjani
Samatra kuna siku alitapika maji kabisamaana kilometer alizokimbia mle ywanjani ni sawa na ktoka ubungo mpaka chalinze kwenda na kurudi.
Breakfast mtihaniwa kwanza ni kumaliza mkatemmoja na kuku mzima unashushia ndizi saba na maji ya kunywa lita tatu,nani anaweza
 
Huku wachezaji wanadanganya sana umri, wachezaji wengi mpaka wanaonekana wanakuwa washamaliza 75% ya maisha yao ya soka hakuna jipya wanaloweza kufanya kwenye ligi ngumu kama ile.

Kingine wenzetu wanaamini katika profile ya mchezaji na takwimu zake, huku mchezaji alikuwa bodaboda kaingia kwenye professional soccer hana hata misimu mitatu, kwao hii ni big no ndio maana timu nyingi zinachukua wachezaji wanaotokea kwenye academy.

Mchezaji akishavuka miaka 25 na hajapata nafasi ya kutwaliwa na vilabu kutoka Ligi hiyo ndio asahau labda iwe ngekewa.
 
Kuna jamaa anachezea E.tunis anaweza kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…