Nyerere alitumiwa na Wazungu kumchafua Iddi?
Mengine yote ungeweza kudanganya kwa nia ya kumpamba. Ila hilo la mgongano wake na Mwalimu ungeacha.
Iddi Amini alikuwa na maneno ya hovyo na vitisho. Mwalimu alijitahidi sana kutomzingatia. Mpaka pale Iddi alipojitoa ufahamu kutaka kung'ang'ania eneo la nchi yetu kuwa eneo la Uganda.
Uvumilivu huo usingeuvumilia hata wewe.
Kama ni Wazungu walimtuma Mwalimu kumchafua Iddi, basi hata wakati wa Vita wangempa msaada wa kivita ili kumchakaza Iddi Amini. Badala yake, Iddi Amini ndiyo alipata msaada kutoka nchi wahisani wa Kiislamu (Libya).