Je, ni kweli kuna majini?

Je, ni kweli kuna majini?

Tafuta kioo chakujiangalia weka mbele yako, hakikisha chumba chambo hakina mwanga, kisha chukua mishumaa miwili. Mmoja weka kushoto na mwingine weka kulia kwako na kioo kikae kakikati ya hiyo mishumaa miwili. Washa mishumaa yako na uwanze kuangalia kioo chako bila kufumba macho mara kwa mara, au ku blink kwamaana nyingine.

Jitahidi usiwe una blink blink mara kwa mara na uweke uzingatiwe kwenye kujiangalia au kuangalia kioo chako kisha tamka maneno haya kwenye mabano kwakuyarudia rudia “Renich Tasa Uberaca Biasa Icar Lucifer My God”

NB: Jitahidi kuwa katika hali ya utulivu na usipungue chini ya lisaa 1 ukiwa unaangalia kioo na kurudia rudia hayo maneno kwenye mabano.

Marejesho uje nayo sio wasema story zakiaarabu halafu wasoma tuu uzi na practical hufanyi. JF ingetaka kupata experience yako kwenye hili
Mkuu umetisha.

Nina uhakika hawezi kufanya Wala kujaribu hii.

Humu watoto wengi na immatured fellas.
 
Kwani kwenye Suratul Jinn original, Majini yaliongea lugha gani ?
waliosoma ilm ya majini wanazijua lugha za majini na ziko nyingi tu,sasa kama hawa waliosoma hii ilm al ghayb wanauwezo wa kuzijua inawezekana wakawasiliana na hao majini kwa lugha za majini Qu'ran haituambii yale majini yaliyoisikia Qu'ran na kuiamini walizungumza Lugha al arabiyya au lughatul jinniya pengine moja kati ya hizi lugha zilitumika nina imani Muhammad alikuwa na ilm kuhusu hivi viumbe pengine hata lugha yao inawezekana alikuwa anaijua
 
M

Mwamba uko vizuri.
Unaonekana umesilimua.
 
Habari zenu WanaJamiiForums?

Swali langu linauliza je, ni kweli majini wapo? Katika utafiti wangu kuhusu majini sijawahi kukumbana nao. Na nimefanya utafiti wa kina mpaka majaribio lakini mpaka sasa sijawahi kuwa-expirience.

Au hii pia tuweke kwenye story za ABUNUWASI? Kama kuna anayeweza kuweka muongozo wa namna ya kuwaita aje,. Nahitaji kumaliza huu utafiti.

Asanteni.
Unafanya utafiti ila hauna nyenzo za hypothesis.
 
Eeeh jini la kiume ukawe mlinzi kwenye Mali zangu zote, nilindie asiwepo wa kuzichukua, Linda Mali zangu

Jini la kike kalete muonekano, kavutie wateja, waipende biashara yangu, wakiitizama hakuna kujiuliza, ewe jini ke lete muonekano wako!

Haya rusha sadaka hizi kwenye lango la bahari! MARUFUKU kugeuka nyuma
 
Tupe kisa kilivyokuwa kisha tukupe ilm
Ni kwamba walikua watatu walihitaji ku summon majini kwaajili ya kusimamia mali zao, walienda chumbe huko zenji majini wabaya walikuja wakawadhuru wawili kasoro jamaa mmoja tu sijaelewaga mpaka leo
 
Hakuna kitu kama hicho. Ni dhana ya kiarabu ya kuwatisha watu au kutumika kupigia fedha za mazwazwa wanaoamini ujinga huu. Majini, pepo, na roho mtakatifu ni dhana mfu na za kufikirika zisizoingia akilini kwa watu wenye vichwa vinavyochemka. Ukitaka kujua kuwa hivi vitu ni feki, vya kubuni, na havipo, waambie wanaodai vipo wavilete lau kimoja tuvione au kuvihisi.​

Sasa wazungu wana hadi dhana ya kuwasiliana na watu waliyokufa kitu ambacho hata hao waarabu hawana, google kuhusu Mediumship uone jinsi wazungu wanavyozungumzia kuwasiliana na majini na watu waliyokufa.
 
Nishaskia watu kadhaa wakihojiwa na efm kwa visa vya kuiutana na majini,mmoja alikua akihojiwa na mkoi ghafla vifaa vikaungua vyote mpaka simu kwa kujaribu tu kueleza yaliyomkuta kwa huyo jini,
Ila kama wewe unakula mdudu kama mimi ni ngumu sana kukusogelea,
Nenda magomeni pale ulizia kuna nyumba moja ukikaa siku mbili utafiti unakamilika
 
Habari zenu WanaJamiiForums?

Swali langu linauliza je, ni kweli majini wapo? Katika utafiti wangu kuhusu majini sijawahi kukumbana nao. Na nimefanya utafiti wa kina mpaka majaribio lakini mpaka sasa sijawahi kuwa-expirience.

Au hii pia tuweke kwenye story za ABUNUWASI? Kama kuna anayeweza kuweka muongozo wa namna ya kuwaita aje,. Nahitaji kumaliza huu utafiti.

Asanteni.
Wewe sema huamini dini pamoja na Allah, hawa viumbe hapo na wameumbwa kumwabudu Allah, pamoja na binadamu.
 
Unataka kusema wale tunaoona wanaotolewa mapepo huwa hawapendi kitimoto?
Hii mada ni majini, kwani majini ni mapepo?
Hao wanaotolewa mapepo wanapenda kitimoto, wanaotolewa mapepo ili wakale kitimoto.
 
Back
Top Bottom