Je, ni kweli kuna majini?

Aaah wapi sidhani kama wapo, Maana nishafanya formula zote ila sijawahi kuonana au kuwahisi, Hizi zitakuwa ni hadithi tu za ABUNUWASI.
Isije ikawa na wewe kusema umefanya formula zote ikawa ni hadithi tu.
 
Hii mada ni majini, kwani majini ni mapepo?
Hao wanaotolewa mapepo wanapenda kitimoto, wanaotolewa mapepo ili wakale kitimoto.
Mapepo ndio hao majini, kwahiyo hata watolewa mapepo wanafaa kuulizwa kuhusu uwepo wa majini.
 
Jin au pepo haviwezi kusogelea ile mali(kitimoto)
MBona hao wanakula kitimoto bado tunaona wanaingiwa na mapepo na wanaenda kutolewa kanisani?

Halafu kama jini hawezi kusogelea kitimoto ina maana hata malaika pia hawawezi kusogelea kitimoto? Maana tunaambiwa asili ya majini ni malaika waliyomuasi Mungu.
 
Huenda zile ni story tu za kiarabu.
Nimefanya utafiti wa takribani miaka minne lakini sijawahi kuwahisi wala kuwasikia.
Mbona hauelezie huo utafiti unaishia kudai tu umefanya utafiti, eleza ulifanya vp huo utafiti.
 
Nitafute nikuonyeshe, tena ikiwezekana nikuunganishe na demu Jinsi. Utafurahia sana
 
Jini na malaika sio kitu kimoja,
Majini yapo kuleta madhara tu,ila malaika hawana madhara
Na hao wanaoenda kuombewa hakuna kitu kama hicho,wale wanaandaliwa ili waonekane wamesaidika lakini ukweli ni kwamba hayawezi mwingia mla mdudu
 
Kujua jini zuri na baya unafanyaje, kuna jamaa zangu wawili walikufa kwa sababu ya haya mambo ya ku summon majini
Muhimu kujua njia sahihi na jinsi ya kujikinga kupata madhara unapofanya jambo kama hilo, ni sawa na kulinda mali yako kwenye mkusanyiko wa watu wengi huwezi kujua ni nani mzuri na nani mbaya anaweza kukuibia.
 
Hiyo ni technolojia aliyokuja nayo sultan WA kiarabu alipokuja kutafuta watumwa Africa. Akipandisha majini huitwa ana MALERIA YA KIARABU
 
Huyo mdudu hawezi kufanya hata malaika kuto kukusogelea kweli? maana tunaambiwa majini ni malaika waliyoasi.
 
Nenda kisiwa cha tumbatu
mkwe, bi mkubwa wangu aliwah kunipa story ya hiko kisiwa kua n mwiko kuingia kwamwanamke akiwa kwenye hedhi kipindi hio na kama itatokea kuna sikukuu mmecinja mkusanye mifupa muifukie kua kinahusishwa na majini huko mwanaue kuoa jin kama kufumba machi nikaona b mkubwa ananionaje, kumbe itakua kweli eh?
 
Hakunaga
 
Wewe jini wa nini siushaambiwa kuna majini wazuei na wabaya haya akija mbaya kwako utafanya nini😂
 
Jini na malaika sio kitu kimoja,
Majini yapo kuleta madhara tu,ila malaika hawana madhara
Na hao wanaoenda kuombewa hakuna kitu kama hicho,wale wanaandaliwa ili waonekane wamesaidika lakini ukweli ni kwamba hayawezi mwingia mla mdudu
Sio kitu kimoja kimatendo ila asili yao ni moja wote malaika.

Hawawezi kumuingia mtu anaekula mdudu kwa sababu gani? Maana wengine husema hata ukivuta bangi jini hakufuati.
 
Ilikuwa yapata saa 5 pale Arusha nilisikia marashi ya kuvutia, mbele yangu nikamuona mwanamke mrembo, anaponikaribia anazidi kurefuka, mwisho akaishia angani na kutoweka. Nilitetemeka mpaka meno yakatoa jasho. Nikaamini majini yapo. Yanatumiwa sana katika mambo ya utajiri ila ni kwa siri kubwa. Wanaotatumia mara nyingi ni wacha Mungu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…