Je, ni kweli kuna majini?

Infropreneur eti majini ndo yamegundua technology? 😹
 
Kweli kule unaongea na jini live
 
Sio kitu kimoja kimatendo ila asili yao ni moja wote malaika.

Hawawezi kumuingia mtu anaekula mdudu kwa sababu gani? Maana wengine husema hata ukivuta bangi jini hakufuati.
Hafithi,simulizi na yote yanayosemwa na niliyowahi kuyasikia wanaoingiwa na hao viumbe ni wasiokula mdudu
 
Infropreneur eti majini ndo yamegundua technology? 😹
Wakati kina Albert Einstein, Isaac Newton, Nikola Tesla, Marie Curie, Ernest Rutherford, Michael Faraday, Max Planck, Alessandro Volta, Stephen Hawking, Archimedes, Galileo Galilei, Neil Bohrs wanaumiza vichwa maabara kukuza Teknolojia.

Haya majinga yanayosema majini ndio wamegundua teknolojia, Babu zao ndio kwanza walikuwa enzi za ujima. Wakiwasha moto 🔥 kwa kupekecha ulindi na ulimbombo.

Halafu leo hii hawatambui mchango mkubwa wa wanasayansi hawa, wanasema majini ndio yamegundua teknolojia.

Teknolojia kubwa hasa katika umeme zimeletwa na wanasayansi nguli kama kina "Nikola Tesla" hadi leo hii tajiri mkubwa Elon musk kaita kampuni yake Tesla.

Kwenye mambo ya teknolojia za radiation wanasayansi nguli kama Marie Curie wana mchango mkubwa sana.

Kwenye mambo ya teknolojia za Anga kina Isaac Newton wana mchango mkubwa sana.

Halafu waafrika bado wana amini ni majini!!
 
Hafithi,simulizi na yote yanayosemwa na niliyowahi kuyasikia wanaoingiwa na hao viumbe ni wasiokula mdudu
Tatizo ni maneno tu hakuna huo uhalisia wala maelezo ya kwanini iwe hivyo. Hata hiyo nyama ya ng'ombe au samaki wale wenye kutaka kushughulika na majini kuna wakati hawali hizo nyama ila kuna sababu zake, sasa mtu akisema ukiwa unakula kitimoto unakuwa haupatwi na jini inabidi aeleze kwa nini? Kwamba majini hawapendi harufu tu ya kitimoto au inawadhuru?
 
Wewe jini wa nini siushaambiwa kuna majini wazuei na wabaya haya akija mbaya kwako utafanya nini😂
Tokea nikiwa mdogo naambiwa majini wapo.. Lakini mpaka sasa najitambua sijawahi kuwashuhudia wala kuwahisi😂😂😂.

Kama mishumaa nishawasha sana lakini hola😂😂😂.. Kwa mda nilioufanya uchunguzi, Itoshe kusema MAJINI HAWAPO.
 
Hapana labda ni mawenge yako tu baada ya kuvuta bangi.
 
Hiyo ni technolojia aliyokuja nayo sultan WA kiarabu alipokuja kutafuta watumwa Africa. Akipandisha majini huitwa ana MALERIA YA KIARABU
Ni kweli kuna mambo mengi ya ulimwengu ambayo hatuyafahamu ila hii ya uwepo wa majini kama una ukweli wowote, Maana nishajaribu kila namna nione hao majini lakini cha kushangaza niliambulia patupu.

Ukiachana na story za akina Mshana Jr sidhani kama kuna majini.
 
Isije ikawa na wewe kusema umefanya formula zote ikawa ni hadithi tu.
Sio hadithi Mkuu nimefanya uchunguzi kwa kina lakini hayakuleta matokeo,
Kama unaweza kunipa formula zingine weka hapa. Nipo tayari kuanza upya.
 
Mkuu umetisha.

Nina uhakika hawezi kufanya Wala kujaribu hii.

Humu watoto wengi na immatured fellas.
Hichi kitu unakiona ni kikubwa?
Hii nitaifanya kesho nikiwa na mda.

Japo ku-concentrate kwenye kioo kwa mda wa saa moja kunaweza kuleta hallucination.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…