Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Jiji limepewa hadhi hiyo tokea mwaka 2000 lakini mpaka leo city centre ina mchanganyiko mkubwa wa vibanda na maghorofa dwarfs wakati huo dodoma ya juzi juzi tu hapa 2017 ina-catch up kwa spidi kubwa na siyo CBD tu inaonesha ubabe mpaka katika viunga vya pembezoni mwa jiji maghorofa na mitaa yenye nyumba nzuri iliyopangiliwa kila uchao inazidi inuliwa.

Umeongelea wingi wa daladala katika mji ambao kuanzia saa 2 usiku mpaka ngoma nne pale natta hiace zinakuwa zimekata na barabara zote kuu ni full giza,

Usafiri unaobakia ni bodaboda nazo ni bei sawa na bure kwenda mpaka Igoma unapelekwa hadi kwa buku 5 tena usiku, tax ni za kuhesabu nazo unapanda hata ukiwa na jelo lako mkononi na mko kuanzia mtu bee hii inaashiria kwamba katika eneo hili mzunguko wa pesa ni duni watu wengi ni masikini na hawamudu gharama za usafiri hata huduma za malazi ni hivyo hivyo, endapo unafanya biashara hapa upande wa hospitality ni hasara tupu no wonder utalii kwa Mwanza hauna uwekezaji mkubwa angalia hata Rock city mall huu ni mwaka unaelekea wa 10 haina full occupancy.

Turudi dodoma ulipopadisi katika suala la ROI ambalo uchelewa popote pale katika real estate industry si suala la kuilaumu Dodoma tu hata hizo DSM na Nairobi kuna wakati miradi ina-slow down katika suala la occupancy rate inategemea na factors mbalimbali za kiuchumi na movement ya watu katika nyakati fulani ambacho si kigezo cha moja kwa moja kuwa mji umesimama na hautoendelea kukua.
 
Mara mia choice variable kuliko wewe ,,,,wew ni mjinga nafiki namba Moja ...na wasiwasi na thinking capacity yako Ina ukubwa size ngapi .hope it's 2gb
 
Mara mia choice variable kuliko wewe ,,,,wew ni mjinga nafiki namba Moja ...na wasiwasi na thinking capacity yako Ina ukubwa size ngapi .hope it's 2gb
Hahahaha! Nimetandika kunakouma ahsante kwa povu ukimaliza jibu hoja kwa hoja..nilishawahi kukwambia yaani [emoji24] [emoji24] [emoji24] chenu wanamwanza ndio[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] changu.
 
Eti daladala sa mbili zimeisha ...itakuwa unakaa mwanza ya matakoni .....
daladala mwanza zinaisha saa sita usiku . kuanzia saa 1 zinakuwa full to capacity,,huwezi pata siti kizembe ,,,watu ni wengi kuliko idadi ya daladala,hivyo nyingi hukatisha ruti ili kuwahi watu waliowabakiza town ...ruti ndefu kama kisesa, nyanshishi,nyangulugulu,nyamadoke , buswelu, Usagara,igombe , ilemela ,, hizi ruti huzidiwa sana mida ya jioni Hadi saa 3 usiku ..
Hoja ya rock city mall ni upuuzi tu umeongelea ,,kujaa Kwa shopping mall siku zote kunategema management na sio wateja....kama rock city mall ingekuwa haina wateja,nono supermarket angekuwa keshafunga zamani .
 
Kawaulize trip advisor...by the way kama hujui vigezo vya five star,,usinisumbue[emoji28][emoji28]
Malaika ikijitahidi sana basi ni three star na kama unabisha nitaleta ratings tuone kama kuna hotel hapo Mwanza inanusa 4 star.
 
Kawaulize trip advisor...by the way kama hujui vigezo vya five star,,usinisumbue[emoji28][emoji28]
Kwa taarifa yako 5 star siyo hoteli za mchezo mchezo kwa hapa Tanzania zinaweza zikawa hazivuki hoteli 5 zenye hadhi hiyo natambua Dar zipo mbili na Arusha moja ila zenji sifahamu zipo ngapi, hivyo usiropoke kwenye mambo yanayohitaji utaalamu.
 
Malaika ikijitahidi sana basi ni three star na kama unabisha nitaleta ratings tuone kama kuna hotel hapo Mwanza inanusa 4 star.
Kumbe we ni comedian ,,unadhani mwanza ni ugogoni.hapo,,,,kama malaika ni nyota 3 , mwanza hotel itakuwa nyota ngapi [emoji12][emoji12]...
Kaangalie rating ya hizi hotel uje na majibu
Tilapia hotel
Ryan's bay hotel
Gold crest hotel
Malaika beach resort
The golden pigeon hotel
Mwanza hotel
The kingdom hotel
Eden palace hotel
Midland hotel
Leyshof hotel
Lenana hotels
Antelope hotel...
Katizame Kama hata Moja wapo inashuka nyota 3 .......na left Uzi ,[emoji28]
 
Kwa taarifa yako 5 star siyo hoteli za mchezo mchezo kwa hapa Tanzania zinaweza zikawa hazivuki hoteli 5 zenye hadhi hiyo natambua Dar zipo mbili na Arusha moja ila zenji sifahamu zipo ngapi, hivyo usiropoke kwenye mambo yanayohitaji utaalamu.
Acha uongo wew ,,, endelea kujichimbia huko kisorya mambo ya mjini utayajulia wapi .
Serena hotel
Ramada hotel
Kilimanjaro Hyatt regency
Gran melia
Golden tulip hotel
Sea cliff hotel
Peacock hotel
Kibo palace
Malaika beach resort
And so more hapo dar na Zanzibar
 
Unajua volume sales ya Drostdy Hof dry red kwa Tanzania? Ulizia wanao import hiyo wine peke yake au nenda pale kwa Mohans uone inavyotembea kuanzia retail mpaka kwa wholesalers na ulinganishe na hizo local wines zote kwa pamoja ndiyo utajua SA imelishika vizuri sana soko la wines kwa hapa Tanzania.

Hapo nimekupa tu hiyo moja,bado hatujaja kwenye zile fine wines zinazuzwa kuanzia 25k-35k.Hao kina Fiorenzo wa CETAWICO au Kato wa Alko Vintage wanafanya vizuri sokoni lakini siyo kwa kiwango cha wines zinazotoka SA.
 
Hujajibu kabisa hoja zake,umeishia kuparaza tu ili mradi umejitutumua kujibu.Hebu nenda sambamba na hoja zake,mfano yeye amekupatia mpaka idadi ya routes za daladala kwamba zote zinaishia sehemu moja.

Inawezekana unapata ugumu wa kujibu hoja zake kwakuwa mwenzio kaenda deep na kaichambua Dodoma vizuri sana,ukizidiwa ni vizuri kutundika daruga na ukaachia mwingine ajaribu kupangua hoja za Ngosha.
 
Ngosha wewe ni Mnoma sana, Home Mwanza nimesoma DOM hii DOM 2016 tu nyuma ya Station njia ya UDOM kulikuwa na Tembe, DOM itachukua muda kidogo kuifikia Mwanza ila itafika tu maana uwekezaji wake mkubwa


Hadi sasa DOM kinachoizidi Mwanza ni gari nyingi zenye namba ya STK,STL,STM na SM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…