Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Watu wengi sana wanauliza kama wewe kwanini Mwanza iliweza kuwa jiji kubwa hivi na ipo mbali na kibuyu cha asali nami nawaambia hata mahali kuliko na buyu la asali kungeweza kuachwa mbali, sema serikali inalibania sana hili jiji la Mwanza.
 
Dodoma unganisha na Arusha.
Nawaambieni nera, kirumba,mwaloni, ghana, kitangiri, bwiru, kabuhoro, kabusungu na pasiansi zishindane na Arusha. Nyakato,buzuruga, mwananchi, Nyasaka, kiloleli, mjimwema na isamilo vs dodoma na wanakaa😀😀😀
 
Narudia tena mshukuruni JPM aliwaonea huruma nyie watani zake maana mlikuwa dhofuri khali kwa kila kitu.Tangu enzi za Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete wote hao walikuwa wanakuja hapo Dodoma kwenye mikutano ya Chama tu.Wakimaliza hawataki hata kuongeza masaa kadhaa wanasepa.

Bila JPM kuwabebeni, mngeendelea kuburuzwa hata na mji wa Kahama
 
Fahari ya jiji la kisasa ni Mvinyo wa kitajiri tokea katika ardhi iliyobarikiwa yenye kustawisha Zabibu adhimu yenye aroma nzuri na ladha murua. Na fahari ya Mwanza ni harufu kali ya vinyesi, dagaa na furu.
Usiniambie Dompo za Kato kwa wanywaji wazuri wa wine hiyo ni sawa na makapi ya wine yapo sawa na kina D'Hof zenye kutengenezwa na mchanganyiko wa makapi ya zabibu au Ambassador's za CETAWICO ndiyo mvinyo wa Kitajiri.Utakuwa unachekesha [emoji3][emoji3]
 
Acha makasiriko leta ushahidi 😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…