Mhhhh... chai hii.. Dar yenyewe haina ukubwa huo wa kutembea km hizo ndani ya mji
Anza Safari Chamazi kuelekea Msongola,,,Nyoosha kwenda Mvuti then Ufike Chanika mwisho...km 15
Chanika mwisho nyoosha mpaka Pugu then ufike Gongo la Mboto...km 15
Gongo Mboto nyoosha mpaka Airport, kunja kushoto uingie barabara ya kwenda Segerea,ukifika Segerea nyoosha kuitafuta kinyerezi ,then nyoosha mpaka Mbezi stendi ....km 25
Uktitoka Mbezi ingia barabara ya kwenda Goba, ukifika Goba nyoosha mpaka Mbezi shule....Kunja kushoto nyoosha mpaka Africana, nyoosha mpaka Mbuyuni kunja kulia...km 20
Utaingia Kunduchi,nyoosha mpaka utakarbia na Mtongani,,,kunja kulia...nyoosha mpaka utafika kota za polisi,endelea na safari mpaka Kilongawima....fuatiza njia mpaka Jangwani Beach ,nyoosha mpaka utafika Kawe Maringo...nyoosha mpaka mpaka Mikocheni Tanesco.....Km 20
Endelea na hiyo njia mpaka Msasani shule,kunja kushoto, endele mpaka Capetown fish market ,fuatisha na kunja kushoto utafika Masaki hostel za Muhimbili, kunja kushoto na Unyooshe mpaka Masaki Mwisho,Yatch Club na Sea cliff ...nyoosha mpaka Coco beach daraja la Tanzanite....nyoosha na ufukwe hadi Ikulu....km 17
Panda pantone, fika feri, then nyoosha hadi kibada, nyoosha utapita kituo cha chuo nyoosha hadi waterpark ya Kigamboni, nyoosha mpaka kufika Tuangoma Masaki,ukitoka nyoosha mpaka pale njia panda ya Kongowe,kunja kulia Itafuta Mbagala, kunja kushoto kuitafuta Chamazi...
Km 28
......hapo zaidi ya km 100,,,na Kuna njia zaidi ya 3 za kupita hizo km.