Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Chuo Cha Mipango IRDP-Dom wanazidi kujiongeza👇👇
 
Wamba naona ni jinsi gani mnavyojitahidi kubishana na huyu mwendawazimu,kiufupi tu hana exposure ndio maana hana aibu kushindanisha Kijiji cha dom ambacho angalau kimepewa favour na serikali ili kio enekane kimekaa ki ustandady wakati ni trashy tupu
Hivi mtu na akili yake anaweza kulinganisha Mwanza (Ilemela na Nyamagana) na Dodoma Jiji???? Yaani Dodoma jiji kuna kitu gani pale cha kulinganisha na Mwanza!!!
 
Hivi mtu na akili yake anaweza kulinganisha Mwanza (Ilemela na Nyamagana) na Dodoma Jiji???? Yaani Dodoma jiji kuna kitu gani pale cha kulinganisha na Mwanza!!!
Hebu tulinganishe hivi vigezo ....kama Mwanza inafika hata nusu ya Dom👇👇
👉Ubora wa miundombinu
👉Mtandao mpana wa barabara za lami
👉Ubora wa mipangomiji
👉Ubora na uwingi wa huduma za kijamii mfano Vyuo Vikuu, Mahospitali n.k
👉Mapato ya halmashauri
👉Mapato TRA
👉Uwingi wa majengo ya ghorofa
👉Uwepo wa taasisi nyingi za Serikali
👉Uwepo wa Ikulu pamoja na mihimili yote ya Serikali...Bunge,Mahakama
👉Makao makuu ya Chama
👉Uwepo wa balozi+mashirika makubwa ya kimataifa
👉Miradi mikubwa ya ujenzi inayojengwa na itakayojengwa mfano Magufuli City,Msalato-uwanja wa ndege,barabara za ring roads n.k
 
Labda mpaka hivyo vyote vikikamilika lakini for the time being bado sana.
 
Labda mpaka hivyo vyote vikikamilika lakini for the time being bado sana.
Rudi shule aisee..eti vikikamilika 😂😂
Kwa kukusaidia tu....👇

👉👉Dodoma ndio Jiji linaloongoza kwa ubora wa mipangomiji Afrika Mashariki na Kati
👉👉Dodoma Jiji inashika nafasi ya pili baada ya Ilala CC kwa mtandao mpana wa barabara za lami
👉Mapato halmashauri ya Jiji Dom wanazidiwa na Dar pekee
👉Mapato TRA Dom wameipita mbali sana Mwanza
👉👉Ujenzi wa miradi ya serikali ...huko ndio usiseme serikali yote almost ipo Dom
👉Vyuo Vikuu....UDOM pekeyake inachukua wanavyuo wote wa vyuo vyote vya kanda ya ziwa na bado nafasi

Kitu pekee ambacho Mwanza mnawazidi Dom ni population ....hilo halina ubishi(Wasukuma hawanaga uzazi wa mpango wanazaliana sana)
 
DODOMA — Serikali ya Uganda imezindua rasmi ujenzi wa Ofisi ya Ubalozi wake katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, ikiwa nchi ya kwanza kuanza ujenzi wa ubalozi wake katika mji huo mkuu wa Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Fred Mwesigye, amesema hatua hiyo ni zaidi ya uwekezaji wa miundombinu, bali ni ishara ya uhusiano wa karibu na wa kihistoria baina ya Uganda na Tanzania. "Hatua hii ni heshima kwa mchango mkubwa wa Tanzania katika historia ya Uganda. Tunafurahi kuwa wa kwanza kuunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuhamia Dodoma," alisema Mwesigye.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Dennis Londo, aliipongeza Uganda kwa kuweka historia hiyo. "Ni kielelezo cha undugu, ujirani mwema na mshikamano wa dhati baina ya mataifa yetu mawili," alisema.

Londo aliwahimiza mabalozi wengine kufuata mfano huo, akisisitiza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi jijini Dodoma. Alitaja miundombinu ya huduma bora kama afya, elimu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kama sehemu ya maandalizi ya kuwakaribisha wanadiplomasia.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, aliahidi kuwa mkoa huo uko tayari kuwahudumia mabalozi wote. "Tunaendelea kuboresha miundombinu yote muhimu kuhakikisha jumuiya ya wanadiplomasia inapata huduma bora na salama," alisema.

Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz

#HabariLEOUPDATES
 

Attachments

  • FB_IMG_1746806753397.jpg
    179.6 KB · Views: 11
  • FB_IMG_1746806746828.jpg
    140.8 KB · Views: 17
  • FB_IMG_1746806738943.jpg
    239.2 KB · Views: 13
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…