Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Najua ni mara chache sana watu kuizungumzia Dodoma kwa sababu wanai-underrate nakudhani kuwa Dodoma imelala ukweli mchungu ni kuwa kwa kasi ya ukuaji wa mji huu kuna majiji mengi nchini yajiandae kukabidhi crown very soon akiwemo mbabe Mwanza ambaye so far bado anahold title la jiji kubwa after DSM wakati DOM yeye akishikilia title la jiji la Kisasa zaidi after DSM hayo ndo maoni yangu utaki leta evidence kuwa MWANZA CBD nizaidi ya DODOMA CBD

Hivyo kwa heshima ya Dodoma mpya na ya kisasa ambayo kwa mtizamo wangu binafsi inaichapa Mwanza 3-0 kwenye ukubwa wa City Center (CBD)

Kuanzia majengo mengi ya ghorofa, ukisasa, mpangilio, bustani na round about nzuri, purchasing power (vitu bei ni juu na watu wana-afford) ndiyo maana mabasi makali na ghali mengi uanzia safari zake hapa kuelekea Dar nasiyo vinginevyo.

Kingine Dodoma CBD bado inakuwa kila sekunde mijengo inazidi chepushwa tena project za maana, ila Mwanza CBD haina jipya sana zaidi ya soko linalojengwa pale hamna kingine chakutarajia kwa sasa, kinachoiangusha Dodoma CBD ni ubaya wa soko lake kuu la majengo(ombi langu kwa mamlaka husika walifanyie mpango wa maboresho linafubaza jiji) ila kwingine huko kote ni fire.

CBD ya Dodoma inaichapa mwanza upande wa barabara za lami, private cars na magari ya kifahari,mandhari ya kimjini mjini kama ni mgeni ukiwa mazengo ukajichanganya majengo huko kwa kina vunja bei bila kusahau uhindini n.k wawezadhani uko kariakoo ndogo, Dodoma CBD ina city vibes ukilinganisha na mwanza CBD.

MADHAIFU:
I. Ukarimu na kauli za kibiashara(customer care) ni "F"

II. Usafi ni "F'' mifereji inanuka vinyesi plus taka zinatupwa tu ovyo na hakuna hatua yeyote inachukuliwa mara mia na halmashauri ya manispaa ya Singida.

III. Upande wa Mahoteli na viwanja nawapa "D" demand bado nikubwa kuliko kilichopo, ukiiondoa Morena ambayo nayo ni yakawaida sana bado hakuna hotel za maana.

IV. Hali ya hewa ya vumbi la kuwasha macho, ukame na unusu jangwa, hata kama umetupia nguo mpya na Kali vipi zinaappear zimefubaa nakupaukiana achilia mbali baridi kali usiku. (Tushirikiane wote kuakikisha Sera ya Dodoma ya kijani inatekelezwa kwa vitendo)

V. Shida ya MAJI hapa usishangae chumba kimoja kikilipiwa 15k na kingine kinachofanana nacho kwa kila kigezo kikilipiwa 30k kumbe kigezo ni kimoja kina maji na kingine hakina. Jamani SERIKALI timizeni majukumu yenu mruhusu jiji hili lifunguke zaidi na likuwe maana kikwazo kikuu ni hiki kabla ya vingine.

But all in all ukiondoa mapungufu hayo machache, mwanza CBD inakalishwa benchi kipindi cha kwanza cha mchezo hata kabla ya kipyenga cha mwamuzi kuamuru game lianze.

TAKE HOME
Ninachoipendea Dodoma; UZALENDO kwani karibia asilimia 95 ya majengo yote, mabango na mapambo CBD lazima neno DODOMA litaappear unlike mwanza na sehemu zingine za Tanzania hii.
Mwanza ipi unaizungumzia mangi Mushi ambayo unataka linganisha na manispaa ya Dodoma iliyopewa hadhi ya kuwa Jiji kwa vile ndiyo makao makuu ya nchi?,hebu lala uote tena mangi Mushi
 
Wapi ambako hakuna upepo na Vumbi?

Mbona nyie wa Mwanza mnaishi na harufu za uozo wa madampo,shombo la samaki na slums? Mnaishije Sasa?
Mwanza hamna upepo na vumbi kama Dodoma, Nimewahurumia sana watumishi waliohamishiwa Dodoma itawachukua muda sana kuzoea hiyo hali ya jangwa.

Maji pia ni changamoto sehemu walau zinazopata maji ni Nzuguni na Area C the rest ni mgao huko nkuhugu ndiyo walishasahau hata ratiba ya mgao wa maji ikoje?, halafu maji yenyewe yanachumvi ni hatari.
 
Ebu tutajie barabara za vumbi Dodoma alafu tulinganishe na za Mwanza ...Idadi ya km zote za barabara moja tu ya Dom Ring Road ni sawa na idadi ya km zote za lami kwa Mwanza City Centre 🤣🤣.
Kwa mujibu wa TANROADS Mwanza kwa sasa haifiki hata asilimia 30 ya ubora wa Dom kwenye mtandao mpana wa barabara za lami, ndiomana kilasiku Mwanza wanalalamika upendeleo wa DomDom.
Mzee pambaneni kwanza serikali iwaletee maji kutoka ziwa Victoria, Pili himizeni upandaji wa miti tofauti na hapo hizo ring road hazitakuwa na maana yoyote kwenye hili jangwa lenu.
 
Mwanza hamna upepo na vumbi kama Dodoma, Nimewahurumia sana watumishi waliohamishiwa Dodoma itawachukua muda sana kuzoea hiyo hali ya jangwa.

Maji pia ni changamoto sehemu walau zinazopata maji ni Nzuguni na Area C the rest ni mgao huko nkuhugu ndiyo walishasahau hata ratiba ya mgao wa maji ikoje?, halafu maji yenyewe yanachumvi ni hatari.
Area c mgawo upo kama dawa
 
Mzee pambaneni kwanza serikali iwaletee maji kutoka ziwa Victoria, Pili himizeni upandaji wa miti tofauti na hapo hizo ring road hazitakuwa na maana yoyote kwenye hili jangwa lenu.
Hujajibu swali...peleka facebook hizo porojo zako
 
Mwanza ipi unaizungumzia mangi Mushi ambayo unataka linganisha na manispaa ya Dodoma iliyopewa hadhi ya kuwa Jiji kwa vile ndiyo makao makuu ya nchi?,hebu lala uote tena mangi Mushi
Kwa kukusaidia tu Mwanza ilipewa hadhi ya Jiji tangu mwaka 2000(miaka 25 mpaka sasa) Dodoma yenyewe ilipewa hadhi ya Jiji mwaka 2018(takribani miaka 7)..sasa cha kushangaza Dom wamewazidi Mwanza kilakitu kasoro population tu👇👇
👉Mipangomiji
👉Huduma za Kijamii
👉Huduma za Kiserikali
👉Mtandao mpana wa barabara za lami (za TANROADS+TARURA)
👉Viwanda
👉Vyuo Vikuu
👉Ubora wa miundombinu
👉Mapato ya Halmashauri
👉Mapato TRA
👉Maghorofa
👉Uwepo wa taasisi nyingi za serikali
👉Uwepo wa taasisi nyingi na mashirika ya kimataifa
👉Balozi n.k

Mwanza ikashindane na Mbeya labda kwa sasa ndio level zake
 
Unajitahidi kubadilisha topic kuhamisha magoli...hapa tunaongelea kilimo hatuongelei madini na hata hayo madini kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka GST na Wizara ya Madini mikoa ya Dodoma na Lindi ndio inaongoza Tanzania.
Ngoja nikusaidie tu kukupa maarifa ya bure👇👇

3333333333333333333333333,,,.png
 
Bado hujajibu swali unaleta porojo....huko mwanza kwenye matajiri inakuaje tena wanazidiwa na jiji la Dom karibia marambili kwenye mapato na makusanyo yote ya TRA na Halmashauri😂😂😂👇👇

Masoko yalikuwa yamefungwa, kwa ujenzi.

Yamefunguliwa kwasasa utaanza kuona tofauti..
 
Utagoogle kila aina ya topics....hapa ni facts tupu👇👇

Unashangilia maduhuli wakati wagogo wenzako hawajui hatma ya maisha yao ya kesho, hata mlo mmoja kwao ni kitendawili.
 
Masoko yalikuwa yamefungwa, kwa ujenzi.

Yamefunguliwa kwasasa utaanza kuona tofauti..
Takwimu rasmi tunazoweka humu tangu mwaka 2015 Jiji la Dodoma linashika nafasi ya pili kwa mapato ya ndani likitanguliwa na Dar pekee...Vp huko miji mingine yote ya Tanzania masoko yalikua yamefungwa !!?😂😂
 
Miji mingine ipi,?

Uzi huu unahusu miji yote?
 
Takwimu rasmi tunazoweka humu tangu mwaka 2015 Jiji la Dodoma linashika nafasi ya pili kwa mapato ya ndani likitanguliwa na Dar pekee...Vp huko miji mingine yote ya Tanzania masoko yalikua yamefungwa !!?😂😂
Huna elimu ya uchumi na huna unalolijua kwenye uchumi, kiufupi Dodoma na Simiyu hazina tofauti na rafiki yake singida.
 
Back
Top Bottom