Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Inawauma sana wazee wa ziwani mpaka wanalia kimyakimya wakiona Dodoma inavyozidi watimulia vumbi
Wanadodoma pambane kujenga mji wenu,mji haujengwi na serikali wala maneno.Nakupambana na Mwanza hakutawasahidia kitu,Mwanza ina natural growth ilikuja Tanga ikaicha,ikaja Arusha ikapita,inakuja Dodoma kwa kelele za midomo nayo inapita.Ukweli ni kwamba Mwanza ina ecomic diversitifaction kubwa kwahiyo sio shughuli ndogo.Dodoma kwanza tafuteni economic specification ndo mtatoka lasivyo mtaendelea kuwa ombaomba nje ya bunge na majengo ya serikali pia mtaendelea kuzidiwa kiuchumi na vimikoa kama shinyanga,iringa na morogoro.
 
Hayo ni maneno ya kijinga na ya kujifariji.

Hakuna Mji bila intervention za serikali, miundombinu huko kwenu mnajenga wenyewe?

Serikali ndio inawafungulia watu biashara hapo Dodoma? Serikali inagawa pesa? Serikali inajenga watu nyumba?

Ni wajibu wa serikali wa serikali kuweka mazingira rafiki kwa biashara na huduma kama miundombinu ya uchumi na ya kijamii na ndicho serikali inafanya.

Afu watu hata hawaelewi,sensa ya 2012 Dodoma ilikuwa namba 3 kwa wingi wa watu juu ya Mbeya hapo kabla ya kuingiza Mwendazake sasa sijui hapo napo ni serikali ilikuwa inajenga.

Wivu ndio unawasumbua watu wa Mwanza,ni hivi baada ya Dar ni Dodoma hakuna takataka nyingina hapo bado miundombinu haijayengamaa.

Jiji la Dodoma limeshawapita Mwanza na litzidi kuweka gap kwa sabababu kilichofanya.mwanza ikavuma miaka ya JK hapo ni idadinya watu kubwa sasa hivi Dom inakaribiana kwa idadinya watu na Mwanza.Faida ya Dom ni kwamba hao watu waliopngezeka Wana purchasing power kubwa.

Sasa unadhani investors wataenda Mwanza au Dodoma? Saizi Dom inaikimbiza Mwanza bado hata airport ya kimataifa,bado serikali haijahamia mazima ,bado mataasisi mengi.

Mwisho hata hiyo Tanga unayoisemea ni kwamba upanuzi wa bandari ukimalizika na Bomba likianza kufanya Kazi itaizidi Mwanza kama zamani ni swala la muda tuu.

Mwanza kubarini size yenu ni Mbeya,Tanga na Morogoro..Dom na Arusha hamuwawezi.Mwaka ujao Arusha wanaanza kujenga interchange.
 
Hii ndio tofauti ya miji inayojengwa na serikali na miji yenye baraka za kiasili isiyotegemea fadhila za serikali, na daima msema ukweli huwa ni GDP. Waiombe na serikali iwajengee na nyumba bure ili kupunguza umaskini.
 
Punguza mihemko za kijinga, Subiri GDP na census hiyo dodoma size yake ni kigoma
 
Punguza mihemko za kijinga, Subiri GDP na census hiyo dodoma size yake ni kigoma
GDP ya sensa ndio itakuja na jipya gani zaidi ya kinachotolewa na BoT na NBS?

Tofauti itakuwa ni idadi ya watu ambayo itakuwa favourable kwa Dom kuliko Mwanza.
 
Mwanza inazidi kubadilika

Serikali ikiamua kuweka nguvu huu mkoa utakuwa babari nyingine maana ni Hub ya kanda ya ziwa
Aaaahh mumesema serikali haitakiwi kuwekeza kwamba una natural growth,sasa tumieni hiyo hiyo natural Ili iwe habari nyingine.

Tuacheni sisi wa Dar,Dom na Arusha serikali itie mkono.

Na sisi wa Mbeya tunasubiria kwa hamu kubwa ujenzi wa dual carriage ya Igawa Mbeya Tunduma na matawi yake ya Uyole Mbalizi bypass,6 lanes ya Uyole Mbalizi na Iwambi bypass.

Pili tunasubiria kupata chuo Kikuu kikubwa cha tiba tawi la UDSM plus teaching hospital.
 

Dodoma haijawahi kuwa na potential ya kukua naturally ukilinganisha na mikoa kama mwanza inayokua yenyewe.

Uzuri wa Dodoma ni ya middle income class, inapangiliwa vizuri na itaendelea kuwa hivyo, na ninatarajia kama ongezeko la watu litakuwa consistence hasa wafanyakazi bhasi vitu kama malls, Conferences na luxurious stuffs zitamiminika na kuipa ile modern life style.

Kuifikia mwanza inawezekana ila itachukua muda hususani kwa sasa ambapo mwanza inakuwa slowly kulinganisha na mid 2000's. Ila Kama ikitokea serikali ikatia mkono wake mwanza kwa airport, public universities, barabara, maofisi etc HAITOWEZEKANA
 
Aaaaahhh!! NYie mumesema hamuihitaji serikali 🤣🤣🤣 ,universities za nini tena?

Airport tayari mshajengewa kwani mnahitaji airport gani tena?

Kitakachokuja Dom sio hivyo ulivyotaja tuu hata viwanda pia.Hapana kilimo ila kunajengwa kiwanda kikubwa Tzn cha mbolea,hakuna dhababu ila kiwanda cha kusafisha dhahabu kinajengwa and many more 👇





 

Mbona makasiriko mzee kwa comment ya kuisifia mwanza.

Mimi mtanzania kote kwangu na hata Dodoma naijua kiasi toka haina chochote cha maana zaidi ya bunge na vyuo. vikifungwa mji unazima kabsaa, vumbi tupu, maji shida, hali ya hewa nayo sio nzuri, chakula tabu na kila kitu expensive sababu mji umekaa kisiasa.

Leo nikipita Dodoma nasema kweli serikali imefanya kazi maana bila hivyo central corridor ya nchi yetu ingekuwa maskini. Kitu ambacho ni kizuri Tu kubalance maendeleo nchi nzima
 
Tukiweka ushabiki pembeni na ukanda kuna ukweli ni lazima tukubali wote, swali la kujiuliza je ni mji gani unakuwa kwa haraka? jibu ni Dodoma na sababu rahisi tu je Dodoma ya miaka 3 nyuma ndio hii ya leo? jibu hapana. Miji mingine inaweza kuwa iko juu ya Dodoma ila tukisema mji gani unakuwa kwa haraka ziko sababu za kusema Dodoma kwa maana kuna investment kubwa inafanyika kuanzia ring road, new airport viwanda vinajengwa na nasikia TBL pia wanataka kujenga kiwanda mambo mengi ila inaweza kuwa labda Mwanza au Arusha au kwingiene wako juu ila swali mji gani unakuwa kwa haraka hapa halina ubishi ni Dodoma mji unakuwa kwa speed sana sasa hii speed ndio kesho itaifanya kuwa juu ya hao wengine. Nimepita mara nyingi Dodoma na nasema Dodoma ya leo sio ile ya mwaka jana au juzi.
 

Mkuu naona umeingia wrong number. Sipo hapa kwa ajili ya ligi zenu, Hivyo yaani

Nikusaidie Tu Dodoma ukitoa hiyo barabara ya nje ya mji, kuna plan ya kujenga train za katikati ya mji, Msalato international airport, Bandari kavu ambapo itakuwa point ya kuchukulia mizigo pasipo kufika DSM etc.. Kiufupi Dodoma itakuwa ni modern CITY

Hiyo airport ya mwanza hadi Leo haijaisha, plan yake ipo lakini hadi Leo jengo la abiria ni kama halijaisha. Utashangaa iliwezekanaje Songwe ila mwanza ipo ignored.

Pia utakuwa ni mpuuzi kusema kwamba Mwanza ijiendeleze yenyewe wakati ni mji wa pili unaoongoza kwa GDP na hapo bado hujagusa kodi. Kingine Mwanza ipo diversified kiuchumi haitegemei kitu kimoja na bado wingi wa watu na mazingira yake wezeshi kimakazi na kibiashara, yataendelea kuvutia investments miaka na miaka endlessly
 
Dodoma 👇
 

Attachments

  • Mtendaji Mkuu Mahakama Prof. Ole Gabriel aridhishwa na maendeleo ya ujenzi, jengo la Makao Mak...mp4
    15.4 MB
  • Dodoma City 2021 ( 360 X 640 ).mp4
    3 MB
  • UBUNIFU WA MAJENGO YA MJI WA SERIKALI MTUMBA DODOMA ( 360 X 640 ).mp4
    32.6 MB
Huko sahihi ila tukumbuke mkoa hauendelezwi na middle income class au high income class.Siku zote maendeleo yanaletwa na low income class kwa sababu low income class ndo market ya production na ndo labours wa viwanda.Mfano kwanini ucjuilize baada ya Dar inafuatiwa na Mwanza kwa kuwa na viwanda vingi??hii kikwasababu haya maeneo yanamasoko na uhakika wa cheap labour.Na Dodoma wakiendelea na utaratibu huu itaendelea kuwa makao makuu tu ya serikali but no anymore kama pretoria south afrika.
 
Hiyo miradi ya dodoma ukiijumlisha yote je inaweza kuzidi bilioni 700? Unafurahia miradi ya mapambo isiyokuwa na tija kwa wananchi unapost majengo ya serikali ofisi za serikali, majengo hayo yana msaada gani kwa wananchi wa dodoma, Mwanza ina miradi mikubwa ya kimkakati kama madaraja, ujenzi wa meli na meli za mizigo zitakazoinua zaidi uchumi wa Mwanza na kanda ya ziwa kiujumla, mradi kama wa daraja la busisi ni bilion 700, Magufuli alikuwa akiwapa white elephant wakati kanda ya ziwa alikuwa akituletea miradi ya kiuchumi, unapost majengo ya ikulu ya chamwino yana nini kwenye uchumi, yaani makazi ya rais nayo ni yakujisifia ndio maana nasema wewe ndugu yangu hauna akili ata kidogo.
🚮🚮🚮
 
Acha kubwatuka tu, mimi napenda facts kuliko kupiga kelele.Kwanza unatakiwa kuelewa kitu kinachoitwa theory of demand and supply.Mwanza haikuwa jiji kwasababu ni makao makuu ya nchi bali imekuwa jiji kwasababu ili kidhi vigezo tangu mwaka 2000 kipindi cha mzee mkapa na Sio mzee Kikwete,Pili miundombinu ya Mwanza haijengwi kwasababu ya kupendezesha mji au makao makuu ila inajengwa kwasababu inahitajika(demand).Mwanza viwanda havijengwi kwasababu ya kufata bunge ila vinajengwa kwasababu ya productive pulling factors.So kwahiyo usitegemee kwamba makao makuu kuwa Dodoma itakuwa pushing factor kwa maendeleo ya Mwanza hapo umefell.Kwanza nikwambie tu hiyo SGR,Madaraja,Meli kubwa,international airport na Dry port ya fela havijajengwa kwa bahati mbaya.Pia ukiona makampuni makubwa yanawekeza sehemu bila kufosiwa unatakiwa kujiongeze.Mfano,Breweries kama Tbl na serengeti,Coca cola pepsi hawa watu wapo mwanza strategicaly kwaajili ya masoko ya congo mashariki,burundi,uganda na sehemu za rwanda.Kitu kingine Congo na Sudani kusini kuingia EAC inashughulisha sana serikali ndo maana unaona SGR,daraja la kigogonna dry port Fela ili kuweza kuwa karibu na nchi za maziwa makuu.
 
Hao wanazani kuwa jiji kubwa ni kuwa na majengo ya ofisi za serikali kila mtaa,dodoma wanapewa white elephant project wanajiona na wao washaota masharubu.
 
Wewe ni kajinga,je Dodoma ilikuwa Manispaa kwa sababu za serikali? Ukijibu hili swali utajua mengine uliyoandika ni takataka zisizo na maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…