Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Najua ni mara chache sana watu kuizungumzia Dodoma kwa sababu wanai-underrate nakudhani kuwa Dodoma imelala ukweli mchungu ni kuwa kwa kasi ya ukuaji wa mji huu kuna majiji mengi nchini yajiandae kukabidhi crown very soon akiwemo mbabe Mwanza ambaye so far bado anahold title la jiji kubwa after DSM wakati DOM yeye akishikilia title la jiji la Kisasa zaidi after DSM hayo ndo maoni yangu utaki leta evidence kuwa MWANZA CBD nizaidi ya DODOMA CBD

Hivyo kwa heshima ya Dodoma mpya na ya kisasa ambayo kwa mtizamo wangu binafsi inaichapa Mwanza 3-0 kwenye ukubwa wa City Center (CBD)

Kuanzia majengo mengi ya ghorofa, ukisasa, mpangilio, bustani na round about nzuri, purchasing power (vitu bei ni juu na watu wana-afford) ndiyo maana mabasi makali na ghali mengi uanzia safari zake hapa kuelekea Dar nasiyo vinginevyo.

Kingine Dodoma CBD bado inakuwa kila sekunde mijengo inazidi chepushwa tena project za maana, ila Mwanza CBD haina jipya sana zaidi ya soko linalojengwa pale hamna kingine chakutarajia kwa sasa, kinachoiangusha Dodoma CBD ni ubaya wa soko lake kuu la majengo(ombi langu kwa mamlaka husika walifanyie mpango wa maboresho linafubaza jiji) ila kwingine huko kote ni fire.

CBD ya Dodoma inaichapa mwanza upande wa barabara za lami, private cars na magari ya kifahari,mandhari ya kimjini mjini kama ni mgeni ukiwa mazengo ukajichanganya majengo huko kwa kina vunja bei bila kusahau uhindini n.k wawezadhani uko kariakoo ndogo, Dodoma CBD ina city vibes ukilinganisha na mwanza CBD.

MADHAIFU:
I. Ukarimu na kauli za kibiashara(customer care) ni "F"

II. Usafi ni "F'' mifereji inanuka vinyesi plus taka zinatupwa tu ovyo na hakuna hatua yeyote inachukuliwa mara mia na halmashauri ya manispaa ya Singida.

III. Upande wa Mahoteli na viwanja nawapa "D" demand bado nikubwa kuliko kilichopo, ukiiondoa Morena ambayo nayo ni yakawaida sana bado hakuna hotel za maana.

IV. Hali ya hewa ya vumbi la kuwasha macho, ukame na unusu jangwa, hata kama umetupia nguo mpya na Kali vipi zinaappear zimefubaa nakupaukiana achilia mbali baridi kali usiku. (Tushirikiane wote kuakikisha Sera ya Dodoma ya kijani inatekelezwa kwa vitendo)

V. Shida ya MAJI hapa usishangae chumba kimoja kikilipiwa 15k na kingine kinachofanana nacho kwa kila kigezo kikilipiwa 30k kumbe kigezo ni kimoja kina maji na kingine hakina. Jamani SERIKALI timizeni majukumu yenu mruhusu jiji hili lifunguke zaidi na likuwe maana kikwazo kikuu ni hiki kabla ya vingine.

But all in all ukiondoa mapungufu hayo machache, mwanza CBD inakalishwa benchi kipindi cha kwanza cha mchezo hata kabla ya kipyenga cha mwamuzi kuamuru game lianze.

TAKE HOME
Ninachoipendea Dodoma; UZALENDO kwani karibia asilimia 95 ya majengo yote, mabango na mapambo CBD lazima neno DODOMA litaappear unlike mwanza na sehemu zingine za Tanzania hii.
Mji wa Mwanza ulianza kujengwa na Wajerumani mwaka 1892 wakati Dodoma ilianza kujengwa kidogo kuanzia miaka ya 1916 wakati Wajerumani wanasimamia ujenzi wa reli ya kati.

Dodoma imepangwa vizuri na ujenzi wake unafuata taratibu kwa kiasi fulani kasoro maji ya kuogelea hamna kwa wale waliozoea hivyo

Mwanza majengo yake mengi ni ya kijerumani na mengine ramani zake zimepitwa na wakati labda jengo la NSSF Capri Point ijapokuwa na lenyewe mahali lilipo na nafasi haisadifu manjonjo ya ubunifu wake.

Mlima Bugando nkali nyumba zote za wananchi wa kawaida zilitakiwa zifidiwe na serikali kisha eneo hilo lipimwe na miundo mbinu ya barabara iwekwe sawa kisha ujenzi uruhusiwe pangependeza zaidi na ingekuwa ni mojawapo ya eneo la kufanya utalii baada ya kisiwa cha saa nane ijapokuwa na chenyewe ladha yake imeisha kutokana na ukiritimba wa malipo ya kutembelea huko.

Mwanza wakifaulu kuweka fyl over bridge kati ya Bugando na Mabatini basi watalifikia jiji la Wuzberg la Ujerumani
 
Mwanza ni Jiji la hovyo na limejaa slums na umaskini
 
Jangwani city
Dom🔥🔥
983434501.jpg
1334007306.jpg
 
Yamekua haya leo? 😅😅
Dodoma imeikalisha Mwanza kwenye Private investments Kwa mara nyingine mwezi August 😂😂😂😂

Zaidi ya Bilioni 100 zinaenda kumwagwa na pia nawakumbusha kwamba hakuna mwezi umepita kuanzia January Hadi August bila commitment ya private investments
20230913_143601.jpg
 
Back
Top Bottom