Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Nondo
 
Hahaha dahh nimecheka sana
 
Asante sana.
Ni matumaini yangu kuwa wote kwa pamoja tutajitahidi kuendeleza elimu hii itakayosaidia watu kuamka na kujitambua
Hiki ulichokiandika kinatoa picha ya mambo makuu matatu.
Kwanza, elimu. Pili, uelewa. Na tatu, utafiti. Una matatizo kwenye hivi vitu vitatu.
Hujui ukweli ni nini? Na hujui nini kilichomo ndani ya mtu? Na hicho kilichomo ndani ya mtu ni mali ya nani?
Bado hujaweza kujua jambo dogo la mwili wako unafanyaje kazi? Lakini pia hujui kama kujitambua ni jambo lililo la kisayansi au lililo nje ya sayansi? Haya machache huyajui, lakini umeandika!
 
Kimsingi unachojaribu kutuambia hapa kwamba unakielewa siyo sahihi.

Wakati wa maisha ni vizuri Kutafakari, kutafuta na kujiuliza mambo mengi.
Hivi: unachokiona, unachokiwaza au unachokihisi ndiyo ukweli?

Je, ni makubaliano, au ni kadiri ilivyo katika jamii ndiyo ukweli?

Umesema Mungu ni nadharia tu. Lakini je, nadharia ni nini?
 
Kuhusu hiki ulichokiandika hapa kutoka kitabu cha Mhubiri, maana yake ni kwamba, Watu hawajui wapi wanaelekea - hawajui nini hufuata baada ya kufa. Huu ndiyo hasa ukweli na maana ya hicho ulichokiandika hapo.
Kwa ujumla kitabu cha Mhubiri kinahusu "Nini thamani ya Maisha?" Kitabu hiki ni mtazamo wa kiulimwengu. Tafiti na fikara za mwandishi wa kitabu cha Mhubiri ni, hasa za ulimwengu.
 
na sisi pia kwa kiasi kikubwa huendeleza maisha yao kuwa kweli kwa kuwekeza nguvu(energy) zetu kwao.
 
The path society ndio wewe, ukiangalia kwa umakini ni sawa tu Christianity.
 
KWELI au NAFSI YA KWELI au TRUESELF.

Nimesoma bandiko lako na michango yako wakati ukijibu kwa wachangiaji wengine humu jamvini. Nashindwa alewa ume maandi yako umeyatoa wapi? Yaani source of backing, where it came from, your intellect or your conciousness? Maelezo yana ukweli lakini it seems huishi katika kweli bali umesimuliwa tuu. Kwa sababu ukweli ni kuwa (it is about to be) na hapo ndio unapata mwanzo na mwisho. In short kuwa kwenye nafsi ya kweli ni kuwa kwenye moment where there is no time or space (to be in moment state). Hapo utakutana na mwanzo wako na mwisho wako na ndio Mungu. Hii ndio kweli aliyoifundusha Issah bin Mariam (Yesu) aliposema wakati umefika Waabudio wa kweli watamwabudu Mungu katika Roho na Kweli kwa sababu Mungu ni Roho.

Yatupasa kuitafuta Kweli na Tukiwa katika hali ya kweli ndio tunamwabudu Mungu, kweli ambayo ipo indani yetu lakini kuipata na kuifikia inahitaji juhudi kubwa, vizuizi vilivyopo kuifikia, ni kifungo tosha ya Nafsi zetu, unless ulichokiandika kimetoka akilini (intellectaul thinking) sio matekeo ya matendo yako, kwani kama matokeo ya matedo ungelitambua kwa nini dunia hii ni kifungo cha nafsi zetu na mungu yupo.

Kila hali tuitambuayo, kwa kuona, kusikia kugusa, kula, kunywa inabadilika. Kweli haibadiliki, ilikuwa kweli kabla hata baadaye, milile na milele daima, lakini tunaona miili yetu haiko kama jana, inachakaa, inazeheka na kuharibika, tunakufa, vitu vinachaakaa, hii inaashiria vyote ni vya uongo, kweli haiko nje yetu bali ndani yetu, ilikuwepo kabla hutujazaliwa na itakuwepo baada kifo cha miili yetu kwani kweli au nasfi ya kweli ndio iliyoumbwa kwa mfano wa Mungu. Hiyo ndio twapasa kuitafuta, kuitafuta ni process, na yatupasa kushindana na majaribu mengi.

Baada ya kuzaliwa tunajenga miili na kukuza akiri na utambuzi wetu unafifia, kupitia akiri tunapata utambuzi wa uwongo uliotafsiriwa katika vigezo vya Muda na Wakati, tunajiona, tunafungwa una vaa ubinafsi, unapata hasira na furaha, Uchoyo na Uroho, Umaskini na Tamaa. Tunakuwa utumwani kutumikia Miili yetu, kuilisha, kuivalisha, kuisafisha, kukidhi tamaa na haja zake, kuilimbikizia mali na kuipatia familia tukizani kuwa sisi mwili na akiri na tuko hai. Tumejikuta tunautumikia ulimwengu wa mawazo (ideas), kumbuka kila ulionalo kuzunguka wewe ukamilishani wazo lililopita akilini kwa mwanadamu. Siku pekee tuna kuwa kwenye nafsi ya kweli ni siku ya kukata roho (KIFO CHA MWILI), tunakumbuka wajibu wetu kuwa na mwili na kuwa hatuja timiza huo wajibu tujajutia but its too late, tunapoteza kumbukumbu, kila tulichozani ndio mafanikio yetu tunachana nacho, mali, familia, elimu, utajiri, tunatafuta mwili mwinine na kuzaliwa tena, tunakuwa watumwa wa mzunguko wa kuzaliwa na kifo. Mpaka utakapo bahatika kupata siri ya kutafua nafsi ya kweli, ukibahatika unaweze pata ukweli in lifetime lakini many lifes.

Dini nyingi au kwa kusudi au bahati mbaya hazitufundishi ipasavyo, mafundisho halisi yamefichwa, lakini kila dini inazungumzia kukutana na Mungu yaani ONENESS. Lakini ukisoma sehemu fulani ya vitabu utagundua kurudi kwa mungu ni kupitia mwili not otherwise . Tafuta Spiritual knowledge achana Imani. Tafuta Kweli ungali hai, usidanganywe na eti kunakufufuliwa. Mwili by nature udongo, ulikuwa udongo, ukapitia kwenye mimea, ukafika mezani kwetu kamachakula, ukaumba miili yetu, siku ya kifu unaanza safari ya kurudi ulikotoka.
 
Kaka kwenye mambo haya huwa nakuelewa sana ngoja nisome tena na tena ili nielewe kama kuna swali nikuulize.
 
In short kuwa kwenye nafsi ya kweli ni kuwa kwenye moment where there is no time or space (to be in moment state).

Nawezaje kuishi bila ya muda au nafasi?
Je mtu anaiyeishi kwakuijua kweli akifa anaenda wapi?
Watu wote wanaozaliwa je washawahi kuishi kabla?
Kama ndio je wote tukifa huku tukiijua kweli hakutazaliwa tena watu wengine?
Ahsante.
 
Nimekuona dumbi niko busy nikipata nafasi nitakujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…