Definition ya neno 'ASTRAL' uliotoa hapo haifanani na zile za kwenye kamusi ya Kiingereza. Pili nini maana ya ulimwengu unaoonekana na usio onekana? Ninachojua mimi mpaka sasa kuna ulimwengu ambao ni physical, na ule ambao ni social ambao tume-construct sisi na tunaweza kuutolea scientific empirical evidence.
Halafu kama hakuna tofauti kati ya ulimwengu unaoonekana na ule usio onekana kwa definitions zako ambazo haujatuambia sasa kuna point gani ya kutaka kutofautisha? Scientifically, kwenye physical world kuna vitu hatuvioni au ku-feel kwa kutumia senses zetu ila tunavifahamu kwa kutumia scientific tools kama microscopes, Hubble telescope. Na pia kuna vitu hatuvioni ila tunasikia effects zake mfano upepo na tunatumia instruments kupata uhakika.
Iweje mwili ambao una systems za ku-experience mambo yaliopo kwenye physical na social world baada ya kufa na systems zote kuzimika na biodegradation/ decomposition kukamilika ndani ya karibu mwaka mmoja baada ya kufa zifanye kazi? Au iweje mtu u-experience death wakati ukiwa hai na kinyume chake pia?
Sasa ili tuutafute ukweli unaotuambia hupo tupatie known and agreed scientific methodology and methods ili to replicate unayotuambia otherwise this is a mere hallucination!