Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Hii inawezekana ikawa kweli kwa sababu inasadikika Hii tuiitayo earth's surface siyo sahihi Bali tupo ndani ya dunia.Vitabu na baadhi ya watu waliofanikiwa kwenda Nje ya Dunia kupitia North pole wanadai huku ni ndani ya dunia(Hollow earth) .Ambapo jamii za siri zinajaribu kuficha hii kitu kwa kuuaminisha umma kuwa dunia hakuna kitu ka hicho .Admiral Bryd naye akaja na explorations zake kuwa Dunia ni physical multiple world yaani Ndani na nje kote watu wanaishi .I mean katikati ya dunia kuna space na watu of more advanced technology wanaishi huko.Siri hii ilizimwa na watu wa jamii za siri .
Mkuu ukisema watu wa jamii za siri unamaanisha watu gani?
 
Upendo! sikufikiria kabla lakini kwanini kweli ya ndani ya nafsi ya mtu uje upendo tu? huoni kama nawe umetaka kila anayefikiria ulimwengu aje na majibu yako..hili ndo ulilomaanisha? Jimena.
Bennie 369 yuko saahihi kabisa.... Ukishakuwa na upendo basi kila kitu kitakuwa sawa.
Upendo wa kweli unaotoka ndani yako na sio nje yako
 
Ulimwengu hauna mwisho! labda uko sahihi kwa unachoamini.Naomba nieleweshe kitu unaposema "Against of nature" ni nani anaamua kwamba "do this,or don't do that because it is against of nature? au chochote anachofanya binadamu ni sawa asili yake inamruhusu?
Nilimaanisha watu wasitende kinyume na asili yetu
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo maarifa yanavyozidi kukua hapa ulimwenguni, nakupa mfano rahisi tu ili twende sawa, mfano tukiamua kukata miti yote tunajua majanga yatakayotokea.... Sasa basi hiyo ndio nature yetu
Kila kitu kina matokeo yake katika hii dunia... Ni lazima tuipende na kuitunza sayari yetu kama kweli tunapenda tupate matokeo mazuri....
Na maisha yetu sisi binadamu pia yako hivyo hivyo kama huo mfano niliokupa
 
Mkuu kuna mtun nimemjibu,lakini nilitaka nikuambie kitu si kwamba unapokuwa unasoma akili yako haihusiki,issue ya kuambiwa kuomba roho mtakatifu akuongoze katika kusoma kwako ni ili usije ukaelewa ndivy sivyo.
Kwa mfano agano la kale liliongelea habari za watu kutahiliwa na ilikuwa mwanamume ambaye hajatahiliwa alionekana hajakamilika,lakini ndani ya biblia kuna andiko linasema "mioyo yetu itahiliwe" sasa unaweza wewe ukatahili moyo wako?
Kwa hiyo nitakuwa nakosea kusema bible ni vile mtu navyoitafsiri yeye au kuielewa yeye binafsi.

Maana nmekuja kuona jinsi mimi nilivyoielewa bible ni tofauti na wewe au yule jinsi watakavyoielewa au kuitafsiri

Ina maana basi hatuweze kuielewa wanadamu wote kwa maana moja
 
Mkuu ukisema watu wa jamii za siri unamaanisha watu gani?

Hard to say cuz the truth will put me in dangerous situations,So just research who are involved in secret societies start with Vrail society in Germany and Hollow earth races by admiral Byrd!!!!Tena hii dunia ni kifungo haswaaaaaaa! hii inahitaji positive thinking ili kutoroka kifungo hiki!!!
 
Hofu ni hofu tu mkuu hebu acha kujustify basi
Hofu ya kutenda dhambi
Hofu ya moto
Hofu ya Mungu
Na hofu ya kudanganywa na shetani
Hizo zote ni hofu.

Sasa matokeo yake mnakuwa na nidhamu ya uoga.
Badala ya kuacha kufanya kitu kwasababu si kizuri mtu ataacha kukifanya kitu hicho kwasababu anaogopa na hiyo ndo hupelekea watu wengi kuishi maisha ya kinafiki.
Naomba kujua elimu mpya ni ipi??
Jimema
Cheki hapo chini Pasco amesema kitu kizuri,nilikwambia hizi astral projection zenu za elimu ya kianadamu zinaweza kukupeleka kubaya.Hata issue ya kuwa nyoka ulifungua milango inawezekana ukiwa out of body.

Mkuu Rakims na MziziMkavu, naombeni sana wakati mnatoa hili somo, pia muwape angalizo hao wanafunzi wenzi, kuwa mchezo huu pia ni sawa na kuijaribu sumu kwa kuilamba!. Wapeni kabisa masharti ya kuzingatia, wakikosea ndio safari jumla!, asubuhi unakutwa ulitangulia ukiwa usingizini!.

Masharti ni haya.

  1. Fanya hivyo ukiwa umelala peke yako chumbani, na kabla hujaanza ujinga huo, hakikisha umefunga mlango kwa fungua, kwa sababu akitokea mtu akakuamsha tuu na kuchange position hata ya milimita moja, ile cord ni kama utando wa buibui, inakatika, wewe unakuwa ndio basi tena!.
  2. Unaweza kukutana na "the under world" ukaona maisha hayo ndio bora zaidi, hivyo cord ikakatika, huku unakutwa ndio basi tena!, safari jumla!.
  3. Hizi ni highest stages za maditation ambazo haziruhusiwa kufanywa na beginners, na hazifanywi un supervised vinginevyo ni safari!.
  4. Yote utakayoyashuhudia kwenye astra body, unaweza kuyafanya by simply opening the "third eye!"
  5. Hizi ndizo the first stages za wachawi!.

Wito wangu mimi, kama hujui unataka nini, utoke out of body ili kuachieve nini, please don't do!. Mtu asikudanganye its is not fun!. Too much knowledge is harmful please don't try!.

Pasco
Pasco much respect.Jimema life is fully of choices,nakushauri tena Yesu anaokoa,mpokee leo ,dont say I did not warn you.
 
Jimema
Cheki hapo chini Pasco amesema kitu kizuri,nilikwambia hizi meditation zenu za elimu ya kianadamu zinaweza kukupeleka kubaya.Hata issue ya kuwa nyoka ulifungua milango inawezekana ukiwa out of body.

Pasco much respect.Jimema life is fully of choices,nakushauri tena Yesu anaokoa,mpokee leo ,dont say I did not warn you.
Hakuna uthibitisho wowote ule kwamba kuna mtu aliwahi kufa sababu ya AP hivyo wala hiyo isikupe shida,
Pia sio kwamba mtu akimeditate ndio tayari anakuwa amefanya ap, meditation zipo za nyingi sana mkuu na ni salama sana hivyo acha kukariri
 
Sorry nilimanisha out of body experience ,Jimema kuhusu mtu akifa anafanya out of body experience unataka upewe uthibitisho ili ukimbie.By the way je kama nilikuwa najifanyia mwenyewe room nikapitiliza unatarajia nani athibitishe si itaonekana kama natural death.Hilo shimo/gereza walilokuweka kama hutashituka mapema huwezi kujitoa mwenyewe unahitaji msaada,umetekwa.
Umeniuliza kuhusu elimu mpya,ni ufahamu wa mambo mapya au yale unayoyajua ila kwa matazamo tofauti na uliokuwa nao kwanza.Nikujibu na swali lako lamsingi,ulimwengu siyo kifungo cha nafasi wala huo haukua mpango wa Mungu ila kuna nafsi za watu kweli zimefungwa katika ulimwengu huu ikiwemo yako.Vifungo vya nafsi viko vingi unaweza fungwa usiamini kitu fulani,like your case hauamini kuhusu uwepo wa Mungu.
Mtu anaweza akafungwa katika ukahaba,uongo,ulevi,akatumikishwa huko na yeye akaona ni sehemu ya maisha yake kumbe amefungwa.Kuna mapepo yanahusika na hivi vifungo na yanakulinda kuhakikisha hautoki.
Mtu anaweza akafungwa katika umasikini,unaweza ukawa na nyumba na gari lakini kumbe wewe ulitakiwa kumiliki zaidi ukaona maisha umeyaweza lakini kumbe uko kwenye kifungo.
Kinachofanyika unafanywa uyaone maisha unayoishi kama ni ya kawaida na hata watu wakikwambia mwenzetu vipi mbona hatukuelewi,wewe una waona wao ndiyo wana matatizo na wewe uko ok.Shetani ni master genius,ana akili sana hata elimu mpya zinazokuja nyie manaona mnagundua vitu ambavyo nikinyume na Mungu ni ibilisi yupo ameshaprogram nanyi mnatekeleza matakwa yake pasipo kujijua.
 
Wafia dini mna kazi sana,
FYI ni kwamba hayo maswala ya dini sio elimu mpya kwangu sababu nimekuwa huko toka mtoto,
Swala la kudhani kuwa imani yako tu ndio sahihi nalo ni tatizo linalowasumbua wana dini wengi hivyo jaribu kujirekebisha
Uwe huru na uutafute ukweli... Uamke
Peace and Love
 
Jimema cool down my dear.Nakumbuka nilikwambia inaweza kuwa elimu mpya au unaifahamu ila kwa mtazamo tofauti.Wewe ulishawahi niambia kuhusu kuwa huko tangu utoto,lakini inategemea ulivyokuwa mtoto inawezekana ulikula matango pori,that is why you ended up to be who you are today.I know deep inside you kuna kitu very strong but just give it a second chance now that you are an adult na unajitambua.
Psychologically watoto ni watu wazima wanaokuwa hawana experience.Now you have experince you have to see the big picture.Ulichosema ni sahihi katika imani za dini watu huona zao ni sahihi,tatizo hii ni topic ndevu lakini,mimi siongelei dini naongelea kumjua Mungu aliye hai Mungu wa Israel huyo nataka umfahamu vizuri.
Dini ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu nachojaribu kukueleza ni zaidi ya mipango ya wanadamu kumtafuta Mungu,mimi naongelea mpango wa Mungu kuwatafuta wanadamu waliopotea kupitia mwanaye wa pekee Yesu.
 
Safi kabisa. Muache anitafute mwenyewe,
Sasa mbona wewe ndio unahangaika??? Au yeye kashindwa??
 
Safi kabisa. Muache anitafute mwenyewe,
Sasa mbona wewe ndio unahangaika??? Au yeye kashindwa??
Hajawahi kushindwa,wakati wake ukifika hakuna awezaye kuzuia.Kuna kitu inawezekana anataka ujifunze kwanza au upitie ili ukimjua uwe mtumishi wake mzuri kabisa ukikumbuka ulivyokuwa unamkataa itakuwa inakupa hamasa kumtumikia.
Mimi sihangaiki,natimiza agizo lake la kuwahubiri watu habari njema anasema "tubu na kuiamini injiri kwani ufalme wa Mungu umekaribia".Yeye anatenda kazi na wanadamu,kama ambavyo shetani ana ma agent wake hapa JF na wanatumika vizuri tu kwa kujijua au kutokujijua,nasi tunamtumikia yeye.
 
Sasa Relax acha huo wakati ufike.
 
Sasa Relax acha huo wakati ufike.
Niko relaxed siku zote ila siwezi kukuacha wewe na the likes kama ninayo nafasi ya kuwaambia kitu.Mimi siwezi kukuokoa wewe ,yeye anaweza.Kazi yangu mimi ni kueneza injiri ya amani basi.By the way unaendelaje au umendelea kupuuzia lile jambo?
 
Naendelea kulipuuza, kila kitu kiko sawa kabisa and iam happy
 
Upendo! sikufikiria kabla lakini kwanini kweli ya ndani ya nafsi ya mtu uje upendo tu? huoni kama nawe umetaka kila anayefikiria ulimwengu aje na majibu yako..hili ndo ulilomaanisha? Jimena.
ndugu muxar, hii thread kwani wewe umeielewaje?
maana kinachozungumziwa hapa ni mtu kujiunganisha na chanzo chake halisi, ajijue yeye ni nani? katoka wapi? na kwanini yupo hapa duniani?
ila pia kama wewe hupendi kuitambua kweli iliyo ndani yako hakuna wa kukulazimisha na pia hatuwezi kukulaumu, kwa maana umeamua kuikimbia kweli yako na kuamini za wengine kwa kuamini kuwa wanaongozwa na roho mtakatifu, your right!
lakini ningependa kukumbusha kuwa hawa unao waamini na kuwaona wanaweza kwa kufanya ishara na maajabu makuu hata wewe pia unaweza kama ukiamua.
Na hii thread pia haijatoa mwongozo wowote wa kufanyika ili uione kweli yako... labda nikuulize kwa jinsi unavyoelewa wewe kweli ni nini?
 
Bado hajaielewa vizuri
 
Hawa si ndio wale wale wenye elimu ya uongo iitwayo 'kweli huru'
Wenye kufundisha kutoka nje ya mwili na macho matatu.
Ni rahisi sana kwangu mm kuwaelewa watu kama ww..
Haya baadae malizia ulipoishia..ujumbe ufike vzr.

Nb Kweli ni moja tu..
Kumjua aliyekufanya kuwa hivyo ulivyo.
Nje ya hapo ni nyongo..(kweliless)
 
Kwa kipindi kirefu sasa nimesikia mafundisho ya kwamba dunia hii ni kifungo cha nafsi na roho za watu... na pia wapo watu mahsusi kwa kazi ya kufungua hizi nafsi na roho zilizofungwa.

Kwanza kabisa ningependa ndugu zangu tutambue ya kwamba sisi binadamu tupo katika ASTRAL, inamaana kwamba hakuna tofauti yeyote ile katika ulimwengu unaoonekana na usiooneka, Vitu ambavyo unaweza kuvijua au kuexperience wakati umekufa pia unauwezo wa kuvitambua sasa, hivyo basi jukumu ni lako kama utataka kuvijua sasa au hadi pale utakapoonja mauti,

Katika hii dunia tunayoishi kila kitu kipo katika kanuni au sheria ambazo zinawezesha huu ulimwengu kufanya kazi zake sawia, hivyo kwa kila jambo ambalo linapata kutokea hapa duniani lina sababu zake, na sababu ndio huleta matukio... sasa ningependa mtambue hapa duniani hakuna aina yeyote ile ya miujiza, kwa sababu miujiza ni kitu ambacho hutenda kazi kinyume cha sheria za ulimwengu huu, hivyo basi ili miujiza ili iweze kutenda kazi ni lazima ifuate kanuni na sheria...

Je, tutaendelea kuita ni miujiza? Kuibuka kwa neno muujiza ni kukosa kwetu maarifa ya kutambua kanuni na sheria za ulimwengu huu.

Hii dunia au ulimwengu sio jela wala kifungo cha nafsi wala roho za watu na wala haitakuja kuwa hivyo.

Kama utakuwa unajua chochote kuhusu LAW OF ATTRACTION utaweza kutambua ya kwamba kitu chochote unachokielekezea nguvu(energy) ndivyo kitu hicho kitazidi kukua au kuongezeka, ina maana kwamba kama watu watazidi kuelekeza nguvu zao katika mambo wasiyoyataka au mabaya ndivyo watakavyozidi kuzalisha na kuyakaribisha wasiyoyataka na mabaya zaidi ya hapo mwanzo, au utashangaa kitu gani kuona mpingaji au mkemeaji wa vitu asivyovitaka akivifanya hivyohivyo anavyopinga?

Jaribu kuchunguza maeneo ambayo kuna mafundisho mengi ya kukemea vitu vibaya au vile wasivyovitaka hali ikoje? Ndugu zangu ningependa mtambue ya kwamba vitu vibaya au vile tusivyovitaka kamwe haviwezi kuondolewa kwa kuvifikiria vitu hivyo au kuviwekea nguvu... labda kama tutakuwa na uhitaji wa makubwa yake.

Ni watu pekee ambao huleta matatizo na kukimbia matokeo ya kile walicho kileta ndio hukimbilia kusema uwepo wa kufungwa kwa nafsi na roho zao katika huu ulimwengu, na ndio aina ya watu hawahawa hubaki kunyosha vidole vyao katika mambo mabaya tu, huona mabaya yanayofanya na papa au vatican, huona mabaya ya Rothischilds family, huona mabaya ya malkia wa uingereza, huona mabaya ya U.S.A n.k bila ya kujua watu hawa huelekeza nguvu(energy) zao katika maisha na mambo yao wenyewe kuwa kweli, na sisi pia kwa kiasi kikubwa huendeleza maisha yao kuwa kweli kwa kuwekeza nguvu(energy) zetu kwao.

Ndugu zangu hapa duniani hakuna nafsi wala roho ya mtu yeyote iliyo kifungoni... ila matatizo yote haya yameanzia pale tulipo ukimbia mwanga,mwanga wa kweli hivo tukaanza uoga na kuamini tusivyovijua, na kwa uoga huohuo hatuwezi kuhoji juu ya kile tunachoamini, imefika hatua kwamba watu wanatamani kufa na kwenda kuishi mbinguni, lakini swali la kujiuliza ni kwamba kama maisha ya duniani umeyashindwa je una uhakika upi kama ya mbinguni utayaweza? Maana mbinguni ni kama duniani(As above as below).

Ndugu zangu baada ya kupita na kukua kimwili huu ni wakati muafaka wa kukua kimaarifa, tuache kuwa kama watoto wadogo wanaolalamika bila ya kuchukua hatua zozote zile, huu ni wakati wa kushika majukumu yako na kuacha kunyosha vidole na kuhukumu wengine, maana pale unavyomhukumu mtu pia ujue hata wewe pia unajihukumu, ila mbaya zaidi hutaishi.....

Watu ambao huwataki ndivyo wao wenyewe walivyoamua kuwa hivyo, je ni vipi kwa wale ambao hawakutaki pia? Je si kwa jinsi wewe ulivyoamua kuwa hivyo?... Ni vigumu sana ndugu zangu kuibadilisha dunia ila dunia ni rahisi sana kukubadilisha wewe, lakini jambo la kufurahi ni kwamba dunia haiwezi kukubadilisha bila mwenyewe kukubali, hivyo lengo la mhimu ni kubadilika mwenyewe, Vatcan sio wamiliki wa hii dunia, Alpha draconis hawatatengeneza maisha yako, Reptlians hawana mamlaka yeyote juu yako, Freemasons, Illuminat Rosscrucian, Skull & bones je hawa wote wana nini na wewe? Kwanini unapoteza nguvu zako kwao?

Wana jamvi mimi nimeona wakati unakuja, na saa imeshafika na ndio tunayo sasa ya kila mmoja wetu kuitambua kweli, kweli ambayo itakuweka huru, na hii kweli ndio itakuwa mwanga wako, nawe utakuwa nuru hapa ulimwenguni, na jambo la kuzingatia ni kuwa hii kweli haiuzwi wala haitolewi bure.

Huu si wakati tena wakushika vitu usivyovijua wala kuwa na uhakika nao, ila kweli ya kweli ipo ndani yako mwenyewe... je hamkusikia ya kwamba unabii hutoka ndani ya mtu mwenyewe? Maana humo ndimo kuliko na kweli yake. Huu ndio wakati wa kila mtu kujiunganisha na chanzo halisi kutoka ndani yako mwenyewe bali si kutoka nje...

Hapo ndipo utagundua uwezo na nguvu ulizonazo, hapo ndipo utagundua wewe ni nani na umetoka wapi na kwanini upo hapa duniani.

Najua itakuwa ni vigumu kueleweka maana lengo la mtumwa ni kuwa huru ila sio habari za kufikiri kuurithi ufalme. Na hapa duniani hakuna mtu yeyote aliyemfungwa, na kama ingekuwa hivyo basi watu wote tungekuwa wafungwa wenye hali sawa, je hizi tofauti zilizipo zinatokea wapi? Je nitakuwa nimekosea kusema hawa wanaotutoa kifungoni ndio waliotuweka? Je wanashindwa nini kumkamata na kumfunga yule anayetufunga? Na je kama ni kweli wanatoa watu vifungoni inakuwaje tena ufalme wao unazidi kuimalika siku hadi siku? (Hamtachelewa kusema nakufuru)

Ndugu zangu sisi tu huru, na hakuna mtu yeyote awezaye kutufunga zaidi ya sisi wenyewe, hakuna kiongozi yoyote wa dini wala mganga yeyote mwenye mamlaka juu yako isipokuwa wewe mwenyewe... na hakuna mtu yeyote awezaye kuifungua kweli iliyo ndani yako zaidi yako mwenyewe, ni wewe tu uliye na hizo funguo, je mpaka sasa hujatambua wale wa kutoka nje wanaosema kukufungua ndivyo huzidi kukufunga zaidi kwa kukuamrisha kipi ufanye na kipi usifanye, na hata wao ndio huamua ni jinsi gani wewe uishi?

Hii ndiyo kweli ambayo leo kwa ujasiri nimepata kuja kuishuhuduia mbele yenu, kwa sababu sasa umefika wakati wa kuamka... AMKA...AMKA...AMKA. sitaweza kukwambia hiyo kweli ni nini, na inatafutwaje maana ipo ndani yako wewe na wala sio kwangu... sitataka kuendeleza kukupa mafunzo ya uongo ili uipate hiyo kweli yako... ila cha kukusaidia ni wewe kufungua macho na ubongo wako na sasa jaribu kuangalia dunia yako katika kona tofauti...

Ni kwa njinsi hii tuliupenda ulimwengu... hivyo tupo hapa kwa dhamira zetu wenyewe... na hakuna yeyote anayepaswa kulaumiwa kwa chochote kile.

Msisahau ya kuwa hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, kila unachokifanya kina matokeo yake yawe ni mabaya au mazuri.

TUENDELEE KUISHI KWA AMANI NA UPENDO!!
Nikupongeze Jimena kwa uzi mzuri. Ni bahati mbaya sana watu wameacha kufikiri kuhusu mustakabali wao, wamewaachia viongozi wao wa kiroho wafikirie kwa niaba yao. Mambo yanapoenda vile wasivyotarajia hujifariri tu eti "Mungu amependa!" Naamini wenye macho wameona uzi wako, na wenye masikio kadhalika. Hongera ndugu.
 
Asante sana.
Ni matumaini yangu kuwa wote kwa pamoja tutajitahidi kuendeleza elimu hii itakayosaidia watu kuamka na kujitambua
 
Back
Top Bottom