Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Mkuu ukisema watu wa jamii za siri unamaanisha watu gani?
 
Upendo! sikufikiria kabla lakini kwanini kweli ya ndani ya nafsi ya mtu uje upendo tu? huoni kama nawe umetaka kila anayefikiria ulimwengu aje na majibu yako..hili ndo ulilomaanisha? Jimena.
Bennie 369 yuko saahihi kabisa.... Ukishakuwa na upendo basi kila kitu kitakuwa sawa.
Upendo wa kweli unaotoka ndani yako na sio nje yako
 
Nilimaanisha watu wasitende kinyume na asili yetu
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo maarifa yanavyozidi kukua hapa ulimwenguni, nakupa mfano rahisi tu ili twende sawa, mfano tukiamua kukata miti yote tunajua majanga yatakayotokea.... Sasa basi hiyo ndio nature yetu
Kila kitu kina matokeo yake katika hii dunia... Ni lazima tuipende na kuitunza sayari yetu kama kweli tunapenda tupate matokeo mazuri....
Na maisha yetu sisi binadamu pia yako hivyo hivyo kama huo mfano niliokupa
 
Kwa hiyo nitakuwa nakosea kusema bible ni vile mtu navyoitafsiri yeye au kuielewa yeye binafsi.

Maana nmekuja kuona jinsi mimi nilivyoielewa bible ni tofauti na wewe au yule jinsi watakavyoielewa au kuitafsiri

Ina maana basi hatuweze kuielewa wanadamu wote kwa maana moja
 
Mkuu ukisema watu wa jamii za siri unamaanisha watu gani?

Hard to say cuz the truth will put me in dangerous situations,So just research who are involved in secret societies start with Vrail society in Germany and Hollow earth races by admiral Byrd!!!!Tena hii dunia ni kifungo haswaaaaaaa! hii inahitaji positive thinking ili kutoroka kifungo hiki!!!
 
Jimema
Cheki hapo chini Pasco amesema kitu kizuri,nilikwambia hizi astral projection zenu za elimu ya kianadamu zinaweza kukupeleka kubaya.Hata issue ya kuwa nyoka ulifungua milango inawezekana ukiwa out of body.

Pasco much respect.Jimema life is fully of choices,nakushauri tena Yesu anaokoa,mpokee leo ,dont say I did not warn you.
 
Hakuna uthibitisho wowote ule kwamba kuna mtu aliwahi kufa sababu ya AP hivyo wala hiyo isikupe shida,
Pia sio kwamba mtu akimeditate ndio tayari anakuwa amefanya ap, meditation zipo za nyingi sana mkuu na ni salama sana hivyo acha kukariri
 
Hakuna uthibitisho wowote ule kwamba kuna mtu aliwahi kufa sababu ya AP hivyo wala hiyo isikupe shida,
Pia sio kwamba mtu akimeditate ndio tayari anakuwa amefanya ap, meditation zipo za nyingi sana mkuu na ni salama sana hivyo acha kukariri
Sorry nilimanisha out of body experience ,Jimema kuhusu mtu akifa anafanya out of body experience unataka upewe uthibitisho ili ukimbie.By the way je kama nilikuwa najifanyia mwenyewe room nikapitiliza unatarajia nani athibitishe si itaonekana kama natural death.Hilo shimo/gereza walilokuweka kama hutashituka mapema huwezi kujitoa mwenyewe unahitaji msaada,umetekwa.
Umeniuliza kuhusu elimu mpya,ni ufahamu wa mambo mapya au yale unayoyajua ila kwa matazamo tofauti na uliokuwa nao kwanza.Nikujibu na swali lako lamsingi,ulimwengu siyo kifungo cha nafasi wala huo haukua mpango wa Mungu ila kuna nafsi za watu kweli zimefungwa katika ulimwengu huu ikiwemo yako.Vifungo vya nafsi viko vingi unaweza fungwa usiamini kitu fulani,like your case hauamini kuhusu uwepo wa Mungu.
Mtu anaweza akafungwa katika ukahaba,uongo,ulevi,akatumikishwa huko na yeye akaona ni sehemu ya maisha yake kumbe amefungwa.Kuna mapepo yanahusika na hivi vifungo na yanakulinda kuhakikisha hautoki.
Mtu anaweza akafungwa katika umasikini,unaweza ukawa na nyumba na gari lakini kumbe wewe ulitakiwa kumiliki zaidi ukaona maisha umeyaweza lakini kumbe uko kwenye kifungo.
Kinachofanyika unafanywa uyaone maisha unayoishi kama ni ya kawaida na hata watu wakikwambia mwenzetu vipi mbona hatukuelewi,wewe una waona wao ndiyo wana matatizo na wewe uko ok.Shetani ni master genius,ana akili sana hata elimu mpya zinazokuja nyie manaona mnagundua vitu ambavyo nikinyume na Mungu ni ibilisi yupo ameshaprogram nanyi mnatekeleza matakwa yake pasipo kujijua.
 
Wafia dini mna kazi sana,
FYI ni kwamba hayo maswala ya dini sio elimu mpya kwangu sababu nimekuwa huko toka mtoto,
Swala la kudhani kuwa imani yako tu ndio sahihi nalo ni tatizo linalowasumbua wana dini wengi hivyo jaribu kujirekebisha
Uwe huru na uutafute ukweli... Uamke
Peace and Love
 
Jimema cool down my dear.Nakumbuka nilikwambia inaweza kuwa elimu mpya au unaifahamu ila kwa mtazamo tofauti.Wewe ulishawahi niambia kuhusu kuwa huko tangu utoto,lakini inategemea ulivyokuwa mtoto inawezekana ulikula matango pori,that is why you ended up to be who you are today.I know deep inside you kuna kitu very strong but just give it a second chance now that you are an adult na unajitambua.
Psychologically watoto ni watu wazima wanaokuwa hawana experience.Now you have experince you have to see the big picture.Ulichosema ni sahihi katika imani za dini watu huona zao ni sahihi,tatizo hii ni topic ndevu lakini,mimi siongelei dini naongelea kumjua Mungu aliye hai Mungu wa Israel huyo nataka umfahamu vizuri.
Dini ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu nachojaribu kukueleza ni zaidi ya mipango ya wanadamu kumtafuta Mungu,mimi naongelea mpango wa Mungu kuwatafuta wanadamu waliopotea kupitia mwanaye wa pekee Yesu.
 
Safi kabisa. Muache anitafute mwenyewe,
Sasa mbona wewe ndio unahangaika??? Au yeye kashindwa??
 
Safi kabisa. Muache anitafute mwenyewe,
Sasa mbona wewe ndio unahangaika??? Au yeye kashindwa??
Hajawahi kushindwa,wakati wake ukifika hakuna awezaye kuzuia.Kuna kitu inawezekana anataka ujifunze kwanza au upitie ili ukimjua uwe mtumishi wake mzuri kabisa ukikumbuka ulivyokuwa unamkataa itakuwa inakupa hamasa kumtumikia.
Mimi sihangaiki,natimiza agizo lake la kuwahubiri watu habari njema anasema "tubu na kuiamini injiri kwani ufalme wa Mungu umekaribia".Yeye anatenda kazi na wanadamu,kama ambavyo shetani ana ma agent wake hapa JF na wanatumika vizuri tu kwa kujijua au kutokujijua,nasi tunamtumikia yeye.
 
Sasa Relax acha huo wakati ufike.
 
Sasa Relax acha huo wakati ufike.
Niko relaxed siku zote ila siwezi kukuacha wewe na the likes kama ninayo nafasi ya kuwaambia kitu.Mimi siwezi kukuokoa wewe ,yeye anaweza.Kazi yangu mimi ni kueneza injiri ya amani basi.By the way unaendelaje au umendelea kupuuzia lile jambo?
 
Niko relaxed siku zote ila siwezi kukuacha wewe na the likes kama ninayo nafasi ya kuwaambia kitu.Mimi siwezi kukuokoa wewe ,yeye anaweza.Kazi yangu mimi ni kueneza injiri ya amani basi.By the way unaendelaje au umendelea kupuuzia lile jambo?
Naendelea kulipuuza, kila kitu kiko sawa kabisa and iam happy
 
Upendo! sikufikiria kabla lakini kwanini kweli ya ndani ya nafsi ya mtu uje upendo tu? huoni kama nawe umetaka kila anayefikiria ulimwengu aje na majibu yako..hili ndo ulilomaanisha? Jimena.
ndugu muxar, hii thread kwani wewe umeielewaje?
maana kinachozungumziwa hapa ni mtu kujiunganisha na chanzo chake halisi, ajijue yeye ni nani? katoka wapi? na kwanini yupo hapa duniani?
ila pia kama wewe hupendi kuitambua kweli iliyo ndani yako hakuna wa kukulazimisha na pia hatuwezi kukulaumu, kwa maana umeamua kuikimbia kweli yako na kuamini za wengine kwa kuamini kuwa wanaongozwa na roho mtakatifu, your right!
lakini ningependa kukumbusha kuwa hawa unao waamini na kuwaona wanaweza kwa kufanya ishara na maajabu makuu hata wewe pia unaweza kama ukiamua.
Na hii thread pia haijatoa mwongozo wowote wa kufanyika ili uione kweli yako... labda nikuulize kwa jinsi unavyoelewa wewe kweli ni nini?
 
Bado hajaielewa vizuri
 
Hawa si ndio wale wale wenye elimu ya uongo iitwayo 'kweli huru'
Wenye kufundisha kutoka nje ya mwili na macho matatu.
Ni rahisi sana kwangu mm kuwaelewa watu kama ww..
Haya baadae malizia ulipoishia..ujumbe ufike vzr.

Nb Kweli ni moja tu..
Kumjua aliyekufanya kuwa hivyo ulivyo.
Nje ya hapo ni nyongo..(kweliless)
 
Nikupongeze Jimena kwa uzi mzuri. Ni bahati mbaya sana watu wameacha kufikiri kuhusu mustakabali wao, wamewaachia viongozi wao wa kiroho wafikirie kwa niaba yao. Mambo yanapoenda vile wasivyotarajia hujifariri tu eti "Mungu amependa!" Naamini wenye macho wameona uzi wako, na wenye masikio kadhalika. Hongera ndugu.
 
Asante sana.
Ni matumaini yangu kuwa wote kwa pamoja tutajitahidi kuendeleza elimu hii itakayosaidia watu kuamka na kujitambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…