Je, ni kweli kuwa Wayahudi walikuwa weusi?

Je, ni kweli kuwa Wayahudi walikuwa weusi?

Hapa kwenye Judah unanichanganya kidogo. Unaposema Judah una maanisha mji au kijiji au ?

Hapa naomba ufafanuzi kidogo.
Hahahah mkuu huwa uko deep sana naamini hii story unaijua ila sijafahamu kuna mtego gani umeniandalia....

Anyway Judah ilikuwa ni kabila waisrael ambalo lilitokana na mtoto mmoja wa Yakobo alieitwa Judah ambao ukapewa jina la mji walioishi watoto wake however baada ya Israel kugawanyika mmoja ya makabila mawili yaliyobaki Israel ya kusini ilikuwepo majority ni kabila la Judah hivyo ufalme wao ukaitwa JUDAH na hivyo judah ukatoka kuwa mji hadi kuwa nchi kamili yenye utawala wa mfalme wa kwanza aliyeitwa Rehoboam.

And the rest is history.....
 
Naomba nirejee maelezo yako hapa ambayo ndio msingi wa swali - Ni kweli Gamal Abder Nasser alipoulizwa kipindi cha vita kati ya Misri na Israel kuhusu Amani mashariki ya kati hasa Wayahudi kuishi kwa Amani katika nchi ya Israel - Jamaa alijibu hivi "The Jews will never be able to live here in peace ,because they left here black but come back white"

Hapo hapo tuulize swali moja Je? Wayahudi kwa asili yao(race) - Wanahistoria wanakubaliana Wayahudi ni Semitic; Na neno hili linapotumika halijumuishi rangi ya ngozi isipokuwa linajumuisha Lugha zenye asili ya Kiafrika na asia.

Tukirejea mateso ya Wayahudi kipindi cha Utawala wa Manazi wakiongozwa na Hitler waliwasaka wayahudi kila kona ya Ulaya na Waliwajua kwa Nywele zao na pua,vernier caliper zilitumika kupima ukubwa wa pua ili kujua iwapo mtu huyo ni Mjerumani(Aryan) au Myahudi.Hii ikaja kujulikana kama Antisemitism.

Hivyo kwa asili ya neno semitic hatupati rangi ya Myahudi kwa asili bali tunapata phenotype yao ya Nywele na maumbile mengine ya nje pamoja na mfanano wa lugha yake ambayo inafanana sana na kiarabu na lugha baadhi za kiafrika kama vile maeneo ya ethiopia na misri.

Bruce Britten mmissionari swaziland anadai kuwa Myahudi original(Kutokana na utafiti wake) sio mweusi wala sio Mweupe! Yaani wale wayahudi waliobaki palestina baada ya 70 AD! Ni Dark Brown- Weupe na Waeusi wa wayahudi tunaowaona leo ni wale waliokwenda kaskazini wa dunia wakawa weupe na wale waliokwenda kusini wakawa weusi.

Katika Historia ya biblia Sijui kwanini Mjadala huu haupo! hakuna mkazo wa dhati juu ya rangi ya mtu isipokuwa mkazo ulikuwa juu ya Makabila na Mataifa yaliyowazunguka wayahudi( Myebusi,Mhivi,Mhiti,mfilisti na nk).

Katika Biblia kuna maeneo machache sana yanayoongelea rangi ya ngozi ya mtu.Hii inawezekana kabisa walibagua makabila sio rangi kwa sababu kama wangelibagua rangi walikuwa wanashabihiana sana na ingekuwa vigumu kudumisha huo ubaguzi! Mfano; Mzaramo na Mhehe! wote wanafanana sana kwa rangi na ngozi lakini wao wanajuana kuwa yule mhehe na yule ni mzaramo.

Wimbo ulio bora 1:5 - 6
Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.

Lakini pia tunaona ulikuwepo Ubaguzi wa waziwazi iwapo myahudi alichangamana na watu wasio wa taifa lake,kwa kuoa au kukubali kuishi nao ilileta shida sana.

Hesabu 12:1
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

Hivyo basi Myahudi kwa asili yake kabla ya Kuchangamana hasa kwenda Ulaya na Asia
1. Alifanana sana na waarabu kwa rangi na maumbile ya mwili
2.Myahudi hawezi kuwa mweupe kama Trump kulingana na sababu za kijiografia.

Myahudi wa Asilia,Sio Mweusi wala Mweupe! Jiografia inakataa Myahudi kuwa Mweupe! Na jiografia ni sayansi.

Wayahudi yaani kizazi cha Ancient Levant walikuwa na ngozi ngumu yenye Melanin yakutosha kuwasaidia kuhumili Jua kali la Maeneo hayo ya israel ya Leo.
Asante.
View attachment 953906

View attachment 953906
Courtesy :https://www.quora.com/Were-the-original-Jews-black
Mkuu nakupa kongole kubwa mno, umetisha sanaaa.
 
Naona umechomoka kaka mkubwa.

Nakuja....
 
Hapa natilia mkazo hata ukija kusoma kitabu kiitwacho "Definition of Arab" utayaona haya,kwamba uarabu unaangaliwa kwa sampuli mbili ya kilugha na kinasaba.

Yeyote ambaye lugha mama yake ni kiarabu basi na yeye ni muarabu yaani huitwa muarabu.

Ndio maana kuna watu au wasomi waliotoka afrika nchi kama Habashi ya kale,Mali,Bukinafaso na kwingine wote maadamu walihamia huko na wakazaliwa huko kwa maana ya wazazi wao kuwepo huko nchi zinazo ongea lugha ya kiarabu na wao huitwa waarabu kilugha.

Hili swali au maelezo kama haya nilitaka kumuuliza mtoa mada nikaghafilika.
 
Mkuu malcom achana naye huyo anachuki binafsi kuna post moja nilikuacknowledge akanishambulia sana.... You're way ahead of our league to argue with such an empty piece of sh**t na hawa ndio wanashusha hadhi ya JF intelligence yaani watu wanakuja na mada za kufikirisha badala wajibu kwa hoja wanakuja na matusi na kejeli.

Mpotezee tu

[emoji481][emoji482] kunywa hiyo kwa kulijua hilo la kunipotezea

Ila kesho usirudie kuniita mimi piece of nini.....!? Utanioga[emoji939]
 
Mkuu nakupa kongole kubwa mno, umetisha sanaaa.
Kiongozi wewe ndio Unatisha! haya Maswali sijui huwa mna yatoa wapi wewe na Athenian Zitto jr.? Yanafikirisha sana! Yanawazisha na kuleta maana ya kuu ya Maisha na tofauti zetu! Thanks Malcom Lumumba keep posting sir.
 
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
wale waisrael waliotoka Misri walikua colored.......

hata wakat wa kuzaliwa kwa Yesu pia, bado wazazi wake walikua colored.........

hata wamisri nao walikua colored na sio waarabu tunaowaona leo!............

sishangai kwann leo wamisri ni wekundu, kama ambavyo sishangai kwann libya, algeria, tunisia, palestina, israel na morocco ni wekundu............

ukitaka kuanza kufumbua fumbo la kwanm waisrael wa leo wako tofauti na wale wa kale, kwanza anza kufumbua fumbo kwann kaskazini mwa afrika kuna watu wasio colored kama walivyokua watu wa miaka 2000 iliyopita!!!

afrocentric views VS eurocentric views........
 
Kwa Kutumia Bibilia. Sipingi kuwepo kwa Wayahudi Weusi ila sioni kama wote walikuwa weusi.

Ile nchi hakuahidiwa kila mtu bali Watoto wa Ibrahimu Uzao wa Isaka, Aliyemzaa Yakobo. Ibra na Sara wote walitokea huko Ur hivyo ni kabila Moja. Isaka alipotaka Kuoa alirudishwa kwa Ndugu zake, Yakobo Pia. Hivyo michanganyiko ilianza hapo Baada ya watoto wq Yakobo.
Kama Ibrahimu alitokea Huko karibu na Iran na Iraq. Atakuwa alikuwa kama mwarabu flani au muajemi.
Kama Mke wa Ketura alikuwa Mmisri alikuwa ni Mweusi na Ibrahimu alizaa watoto weusi.
Musa Alimuoa Sipora ambaye Bibilia inasema alikuwa Mweusi, Hivyo Watoto wa Israel baadhi lazima wawe weusi.
Suleiman alioa wake 1000, miongoni mwao kwa mujibu wa masimulizi aliozwa watoto wa malkia wa Sheba, Hivyo lazima mbegu nyeusi iwepo.
Kwa Sababu Pia walienda utumwani Misri, Yusufu akapewa mke wa kimisri kuna uwezekano wa watu weusi kuzaliwa.

Kuna uwezekano kukawa na waisrael wa karibu race zote maana wamejichanganya tangu miaka ya zamani.
Mfano, Boazi alioa Ruth Mmoabu. watoto lazima wawe chotara.
Irani waliishi utumwani wayahudi.
Ulaya walisambaa kila kona enzi za uvamizi wa 70AD.
India Pia walifika.
Ethiopia Pia.
Kingine Pale ilipokuwa ni Highway ya Dunia. Carravan za watu wa kila taifa zilipita. Hivyo intermarriage waliokatwazwa nyingi zilifanyika.
Sishangai hata akitokea mchina akasema asili yake ni Uyahudi.

maoni
huko kwa nebukadreza hakukuwa na watu wekundu (mnawaita weupe japo sio weupe).....

watu wa kule walikua colored....... nenda india vijijin utaona wenyeji wengi ni colered!.....

ngozi hii colored kuna watu may b (wana/wali)taka kuipoteza!...... hizo juhudi mpk leo zipo!
 
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?

Kila mwafrika anajitahidi kua jew!

Unasikia sijui Tutsi wanajiita jews,sijui Chagga wanajiita jews,sijui Kikuyu wanajiita jews,etc

We are Africans,niggaz stop this madness!

Hata kama whatever the case,zamani ulikua Jew,who cares?You are now Africans!

Be proud of Africa,stop kissing jews asses!

They dont like us anyway,f.uck em!
 
nadhan tatzo ni kwamba hii race yetu imeshushwa chini kiasi kwamba tunaona hatuna thamani mbele za Mungu!!!!

hata upande wa wenzetu waislamu nao, kuna tatzo la kuona mwarabu ndio mwenye dini, kwaio wao inabidi waishi kama mwarabu, waongee kama mwarabu, wavae kama mwarabu!!........ bila kujua kwamba mwarabu anavaa vile kwa sababu ya joto huko kwao!

Mungu atupe neema weusi tujitambue, hakika hatutakua watumwa wa hawa ngozi nyeupe kiasi cha fikra zetu kuathiriwa na wao!
 
nadhan tatzo ni kwamba hii race yetu imeshushwa chini kiasi kwamba tunaona hatuna thamani mbele za Mungu!!!!

Tuko deprived mpaka aina ya deity..wametupa deity wao ambae ni white na sisi tukakubali..We accepted and worship our oppressors God..

Tuachane na ujinga wa dini and god altogether...infact there is none to begin with....Delete everything!

Mungu atupe neema weusi tujitambue, hakika hatutakua watumwa wa hawa ngozi nyeupe kiasi cha fikra zetu kuathiriwa na wao!

Mungu yupi mzee baba?A white caucasian God representing a face of our own oppressor?

There is no God whatsoever!

No one has ever prove its existence ,and we can dismiss it with no evidence too!
 
Unaielewa vipi hii kauli "Kila yahudi ni ukoo wa Israeli,lakini si aliye katika ukoo wa Israeli ni yahudi"
Israeli Kama ufalme kabla haujagawanyika ulikua umejumuisha makabila 12 likiwemo kabila la Yuda kwaio ni sawa Kila myahudi ni mwisraeli.....ukisoma baadae huu utawala uligawanyika katika falme mbili moja ukaitwa ufalme wa Yuda ukiwa una beba makabila mawili Benjamin na Yuda na mwingine ukabaki kuitwa ufalme wa Israeli ukiwa na makabila 10 yaliyobaki,baadae huu ufalme wa Israeli ulisambaratika na hayo makabila Mengine 10 Kama hayapo hivi Sasa, Bali ufalme wa Yuda uliendelea kuwepo na baadhi ni Hawa tunaowaona wamechanganyika Sasa na kuunda ilo taifa lao Tena.
 
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
Mada nzuri sana hii mkuu,hili swali nimekuwa najiuliza siku nyingi sana.Kama mama yake Ishmail(Babab wa Palestina) alikuwa Mwafrka wa Misri,ni kwa nini leo Wapalestina wote ni weupe hakuna hata chotara wa kiafrika?.Na kwa nini tuseme tu wayahudi ndio walistahili kuwa weusi na siyo wapalestina.
 
Nitumie bible. Kuna mstari kwenye biblia unasema "Je mkush/muethiopia anaweza kubadili rangi yake". Hii inatuonyesha kuwa waliokuwa wanaambiwa haya maneno walikiwa na rangi tofauti na wakush/waethiopia.
 
Yeremia 13:23 Mungu anawauliza Waisraeli baada ya kumuasi kuwa:
Je Mkushi(mtu mweusi) aweza kuibadili rangi yake??

Maana yake mpaka enzi za Yeremia Mtu mweusi ambaye alikuwa akitoka Ethiopia alijulikana kwa weusi wangozi yake na alikuwa tofauti na race ya Kiisraeli mpaka kuweza kumfanyia reference.

Lakini pia Biblia inamtaja mfalme Daudi kama mtu mwekundu wa ngozi, maana na alikuwa tofauti na wengine.
Maana yake Waisraeli pia hawakuwa wekundu kama wazungu.

Kwa hiyo basi huenda Muisrael ngozi yake ilikuwa chotara au ilikuwa ya njano(mtu wa mashariki ya kati).
 
1. Ham ni baba wa weusi lakini sio baba wa negroes au wabantu ambao wameshathibitika kisayansi kuwa ndio Waisrael halisi hasa wa kabila la Lawi (Walawi).
2. Wimbo Ulio Bora 1:5-6, Mfalme Sulemani anajitanabaisha kuwa mweusi. Kumbuka huyu ni Muisrael
3. Waarabu wa asili ni weusi...
4. Uyahudi ni kabila pia dini. Wa uzao wa Yuda. Waisrael ama Wayahudi wengi wa leo walianza kama dini lkn baadae wakasema wao ni wa damu; Ashkenazi Jews...Ukiiangalia Mwanzo 10:1-3 utagundua Ashkenazi ni kizazi cha Yafethi, mtoto wa mwisho wa Nuhu. Israel hatokani na Yafethi bali Shem. Lakini leo hao Wayafethi wa Ashkenazi ndio Waisrael kwa asilimia kubwa!
5. Yesu alikuwa mweusi na atarudi mweusi. Ukiusoma Ufunuo 1:14-15 unamtaja Yesu katika ujio wa pili; sifa ainishwa hapo ni sifa za mtu mweusi
6. Tukumbuke Yesu mweupe na Wayahudi weupe wameanza kuwa mashuhuri mwishoni mwa karne ya 16. Hapo nyuma masanamu yote ya kanisa yalikuwa ya watu weusi: kuanzia Yesu, Yosefu, Maria, Mitume wote n.k
7. Wajuvi watajazia
 
Neno Jews (wayahudi) si jamii Bali hii ni dini iliyoanzishwa na wana ukoo wa yuda kwa lengo la kumuabudu Mungu.
Baada ya wana wa Israeli kutawanyika kila pande za dunia, hiyo dini ikabaki haina mwenyewe, jamii mbali mbali zikaiga desturi zake nayo ikatawanyika huko ulaya, uturuki, marekani, urusi, ethiopia na irani ikapata wafuasi wapya.

Mtu yeyote toka pande zozote za dunia awe, mchina, mwarabu,mwafrika au mzungu akiwa mfuasi wa dini ya wayahudi ataitwa myahudi, haijalishi yeye ni muisraeli(damu ya yakobo) au laa.

Wale wayahudi wanaoitwa walowezi huko palestina ni wazungu toka ulaya na niwahumini wa dini ya wayahudi.
Hata Mimi Leo hii nikiwa muumini wa dini ya kiyahudi nitaitwa myahudi. pia naweza nikajiita muislamu,mkiristo au mpagani kama nikipenda.

Kwa hiyo mtu kuitwa myahudi haina mahusiano yoyote na damu ya yuda au wana wote wa yakobo.

Hata biblia inatambua hilo;

Ufunuo wa yohana 2:9

najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la shetani.

Akaendelea kusisitiza tena

ufunuo wa yohana 3:9

Tazama nakupa walio sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo.

Tusomeni maandiko.

"" watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa""
 
Back
Top Bottom