Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Biblia imeandikwa na watu tofauti kwa vipindi tofauti

Kanisa katoliki limechukua baadhi ya maandiko ya namna hiyo na kuyaweka pamoja hiyo ndo ikaitwa Biblia
Padre Jerome alitafsiri kutoka lugha mama.
Kwa maana hiyo wayahudi ndio waliachiwa kanisa la kwanza sio waroma.
 
Biblia imeandikwa na watu tofauti kwa vipindi tofauti

Kanisa katoliki limechukua baadhi ya maandiko ya namna hiyo na kuyaweka pamoja hiyo ndo ikaitwa Biblia
kanisa katoliki lilikuwa ni dola katili la rumi ya kale iliyokuwa inawapinga na kuwauwa wakristo na biblia ilikuwepo kabla ya dola hilo kuwa kanisa kwasababu ukristo ulikuwepo kabla ya dola hilo ushawai kusikia hii historia ?
 
sasa kwan
kwani nimesemaje labda ?

Katoliki ndo iliyoamua kitabu gani kikae kwenye biblia na kipinkisikae
Sawa, uko sahihi.
Ila sio wao waliachiwa kanisa la kwanza. Na wao walichukua hivyo vitabu toka kwa kanisa la kwanza ambao walikuwa wayahudi.
 
Sawa, uko sahihi.
Ila sio wao waliachiwa kanisa la kwanza. Na wao walichukua hivyo vitabu toka kwa kanisa la kwanza ambao walikuwa wayahudi.
unaposema kanisa la kwanza unamaanisha ni kanisa gani hilo litaje ?
 
Padre Jerome alitafsiri kutoka lugha mama.
Kwa maana hiyo wayahudi ndio waliachiwa kanisa la kwanza sio waroma.
ni sawa tu na ni kweli, na makao makuu yalikua Jerusalem mtume petro aliuwawa roma kwaajili ya kusambaza ukristo,

Roma ilikua na nguvu ya kisiasa dunia nzima ilisaidia kulikuza na makao makuu yaliwekwa Roma kwa heshima ya Petro ata ile Basilica ( kanisa kuu ) imepewa jila la Mtume Petro

sasa hata kama wameachiwa wayahudi au waroma haibadilishi kitu kanisa Katoliki linabaki lilelile
 
safi unajua mtume petro aliishi katika kipindi cha ufalme wa dola hilo kubwa lenye nguvu la roma ambalo sasa ni kanisa katoliki ? sasa inakuwaje kuwaje petro awe mwanzilishi wa dola hilo ambalo hivi sasa ni kanisa katoliki ?
 
kanisa iatoliki lilikusanya kama nani ?
Kwa sababu Roman empire ilikuwa inatawala dunia.
Walichukua nyaraka nyingi kutoka sehemu mbali mbali za dunia, ambazo zilikuwa zinztumiwa na makanisa ya kale.
Wakaamua kuchagua baadhi ya vitabu na kuacha vingine.

Wakati maandiko ya Agano Jipya yalikuwa yakiandikwa (karne ya 1 BK), makanisa mbalimbali yalikuwa tayari yanayasoma, kuyaiga, na kuyahifadhi. Lakini kulikuwa pia na maandiko mengi ya uongo (pseudo-gospels), hivyo ilibidi kanisa lichunguze ni yapi ya kweli.

Miongozo ya Kuchagua Vitabu ilikuwa

-Katika kuamua vitabu vya Biblia, viongozi wa Kanisa walitumia vigezo kama:

-Vilitungwa na mtume au mtu wa karibu na mitume?

-Vilitumika sana katika ibada na makanisa mbalimbali?

-Vilikuwa vinakubaliana na mafundisho ya Kikristo yaliyoenea?

-Viliongozwa na Roho Mtakatifu (kulingana na imani yao)?
 
hebu nenda kasome kitabu cha ezra au nehemia chote kisha utaona walikuwa na vitabu vya torati vya musa wakiwafundisha watu inamaana biblia ilikusanywa na waisrael wenyewe na ilifundishwa kabla ya dola la roma. najua hata kisa cha ezra na nehemia hukijui
 
nenda kasome kitabu kizima cha ezra na nehemia katika agano la kale kisha uje uniambie kuwa kanisa katoliki ndio limekusanya vitabu vya biblia ni kweli limekusanya lakini biblia ilishakuwepo ikiwa imekusanywa kabla yake.

mfano mimi naweza kukusanya vitabu vya biblia pia hivi leo haimaanishi mimi ndio nimekusanya biblia hapo awali pekee
 
ndio sasa wewe unajua historia sio kufata ushabiki

sasa kuna walokole wanatumia biblia lakini hawajui hata ilipatikanaje
 
unaposema kanisa la kwanza unamaanisha ni kanisa gani hilo litaje ?
Biblia yako imeliita hivyo hivyo haijalitaja kwa jina.

Hili ni kanisa la mitume, ambalo lilianza huko Yerusalemu siku ya Pentekoste, wakati Roho Mtakatifu alishuka juu ya wanafunzi (Matendo ya Mitume 2).

-Sifa za kanisa la kwanza katika Biblia:
-Lilijengwa juu ya mafundisho ya mitume (Matendo 2:42).


Halikuwa na jina maalum kama madhehebu ya leo (k.m. Katoliki, Pentekoste, n.k.). Lilijulikana tu kama "kanisa" 1 Wakorintho 1:2, Warumi 16:16. Hili linaonyesha kuwa lilikuwa na umoja na halikugawanyika kwa majina kama ilivyo sasa.
 
Sawa, uko sahihi.
Ila sio wao waliachiwa kanisa la kwanza. Na wao walichukua hivyo vitabu toka kwa kanisa la kwanza ambao walikuwa wayahudi.
hakukua na mfumo huu rasmi wa vitabu vyote kupangwa kama sasa

ila vilikwepo vilivyokua vinatumika na wayahudi ambavyo vikawekwa kama agano la kale
 
ndio sasa wewe unajua historia sio kufata ushabiki

sasa kuna walokole wanatumia biblia lakini hawajui hata ilipatikanaje
leo nimepata wasaha wa kujadiliana na wewe hebu nikuulize hivi unajua kuna maneni kwenye biblia yaliandikwa na mungu mwenyewe kwa mkono
 
Tazama hapa👇

View: https://www.scribd.com/document/408400532/list-of-Popes-pdf
 
kila kitu kina gawanyika kutokea sehemu fulani,

Je katoliki imegawanyika kutokea wapi ?

Je katoliki ina jina ? Catholic maana yake ni kitu kilichoenea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…