Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Hapa sasa unakosa elimu ndogo ya Biblia kwamba kila verse inakua na ujumbe wake maalum (conceptual meaning) ambao unatokana na lengo maalum la kitabu ama sura hiyo. Lakini maana hizi hazipingani kwenye dhumuni kuu la Mungu kutuumba ili tumtumikie, kutukomboa kutoka utumwa wa dhambi na kutuahidi kuwa siku moja tutarejea katika makao yake ya milele na kufurahi pamoja na watakatifu wake.

Ukiongelea kitu kimoja kutajwa kwa maana tofauti katika Biblia unaweza kuelezeaje hivi vifungu?
1. Uumbaji kufanyika kwa njia mbili tofauti (Mwanzo 1:1 na kuendelea na ule wa Mwanzo 2:4-25.
2. Mungu kuumba mwanamke na mwanaume kwa pamoja na baadae tena Mungu kumuumba mwanamke mwishoni kutoka katika ubavu wa Adam (Mwa 1:27 na Mwa 2:21)
3. Baba mzazi wa Yusufu aliekua mume wa Mama yake Yesu, je ni Yakobo (Mat 1:16) ama Eli (Luk 3:23)
4. Yohana Mbatizaji ndie alikua Elia ambae waisrael waliamini atarudi? Yesu alimtambulisha hivyo alipokua anawafundisha makutano (Mat 11:14) lakini Yohana mwenyewe alikana hilo alipoulizwa na makuhani na walawi (Yn 1:21)
5. Yesu kumpa sifa kedekede Simoni Petro katika vipindi tofauti, lakini pia kumwita shetani baada ya Petro kutaka kuonesha imani yake kubwa kwa Yesu kwamba hawezi kupatwa na mambo mabaya (Mat 16:23). Kwahiyo hapo napo utatuuliza kuwa Je Petro ndie aliekabidhiwa kuchunga kondoo kweli kwenye injili ya Yohana baada ya Yesu kufufuka na kuwatokea mitume kule pwani ya Thiberia (Yn 21:15-17) ama ni shetani?

Biblia sio kitabu cha Chinua Achebe ambacho unaweza kukisoma na kukifanyia nukuu kadri unavyojiskia.
 
HAKUNA UPAPA ALIOUACHA MTUME YEYOTE!

PAPA NI KIONGOZI WA KUZIMU ANAEWAKILISHA HUKU DUNIANI KWA KUWEKA TAWALA ZOTE ZILIZOPO BILA MAPATANO NAE HUWEZI TAWALA!!!

SASA JE PETRO ALIKUA NA MAPATANO GANI NA SERIKALI YA KIRUMI!!?
Uliulozwa wewe? Mbona unajibu swali ambalo halikuelekezwa kwako?
 
Ndugu yangu mpendwa, hebu tafakari tena kidogo: Kama Papa ni mwamba, na Kanisa limejengwa juu ya Papa, anapofariki, Kanisa nalo linabomoka? Maana msingi wa nyumba ukiharibika, na jengo lote lazima lianguke. Kama Kanisa limejengwa juu ya Papa, wakati huu ambapo Papa mpya hajapatikana, Kanisa linasimama juu ya nani?

Petro hakuwa mwamba. Na Papa hawezi kuwa mwamba. Sifa kuu ya mwamba ni hii: mwamba unadumu milele. Yesu baada ya kufufuka yuko hai milele. Ndio sababu katika lile Andiko, anatajwa kuwa ni mwamba wa milele.
 
Umetoka kwenye ushahidi ulioleta wa vifungu vilivyotaja Mungu ama Yesu Kristo kuwa mwamba badala ya Petro.

Hoja yetu ilikua ni kwamba, kila neno lililotamkwa ama kuandikwa katika Biblia lilikua na sababu ama kusudio lake, na pia lilikua na kundi lengwa. Kwahiyo Yesu kumtambulisha Petro kama mwamba hapingani na wengine waliomtambulisha yeye Kristo ama Baba yake kuwa mwamba wa milele.

Kuhusu kanisa kujengwa juu ya Petro, haimaanishi kwamba yeye ndie atalisimamia kanisa kwa kipindi chote, bali imani aliyonayo juu ya Kristo ndiyo itakayokua chanzo cha imani ya kanisa atakaloliacha Yesu Kristo ambalo msingi wake ni Kifo na ufufuko wake.

Kuhusu muendelezo wa kanisa baada ya kifo cha Papa, hapa unataka nikueleza kwa misingi ya Kanisa katoliki na makanisa washirika yanayoheshimu mamlaka ya Papa, maelezo haya yanaweza yasikubalike na makanisa mengine yasiyoamini katika mamlaka ya Papa (kwahiyo hayawezi kuwa sehemu ya majibu ya hoja yetu ya msingi).
 
Ni mamlaka gani kikanisa (kanisa lolote) ni ya kiMungu?

Yesu aliacha kanisa? Na kama hilo kanisa lipo lenyewe limetoa wapi hayo??

Huu mtililiko wa mapapa toka huyo Petro, wakatoliki walianza kuutumia lini na muasisi wake ndie huyo papa Gregory??
 
Piga spana mkuu, kwanini mijadala ya namna hii huwa unakimbia mapema??
Na itakua vizuri zaidi sometimes ukiwa unaambatanisha walau na vitabu ulivyotumia.
 
Hoja zako hazijanishawishi. Unasema tusome historia ila wewe unaweka historia jumuishi, weka mahali, majina na miaka, sio story tu mkuu.
Unaposema Petro alifia Vatican, mwaka gani, kiongozi alikua nani, alikufaje, kwanini, alienda huko Vatican, sio kusema tu alifia hapo, hiyo haitoshi.
Ina maana alipokufa ndio akaacha ukatoliki? Alikufa akiitwa papa? Kwanini anaitwa papa ilhali alikufa akijua yeye sio papa??

Jiweke huru, usilipiganie kanisa, pigania imani yako kwa Kristo. Kristo yu ndani yako, humpati kwa ekaristi Usifungwe na kanisa mkuu,
Kuna raha ya kujifunza mengi ukiwa huru.

Ila kama ndiko imani yako ilikolalia ni sawa.
 
Umetoka kwenye ushahidi ulioleta wa vifungu vilivyotaja Mungu ama Yesu Kristo kuwa mwamba badala ya Petro.
Rafiki yangu Munamuge
Sijatoka kwenye ushahidi nilioleta wa vifungu; nilitaka tu na wewe upige bongo kidogo, usikumbatie tu mapokeo.

Sasa ngoja nirudie kukufafanulia vizuri Maandiko niliyokupa, inaonekana hujayaelewa.

Kwa Kiyunani(lugha ya mwanzo ya Agano Jipya), mwamba ni Petra, sio Petros. Yesu aliposema “juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu,” hakumzungumzia Petro (Petros). Alikuwa anajitaja Yeye mwenyewe - Mwamba, Yesu Kristo(Petra).

Angalia vizuri tofauti ya lugha – Petros na Petra
Katika Mathayo 16:18:
“Wewe ndiwe Petro (Petros), na juu ya mwamba huu (Petra) nitalijenga Kanisa langu...”

Petros = ni jiwe dogo, jina la Simoni.
Petra = mwamba mkubwa, thabiti, usioweza kuhamishwa – ni Kristo!

Yesu hakusema kwamba atajenga Kanisa juu ya Petros, bali juu ya Petra – Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai (Mathayo 16:16).

Maandiko niliyokupa ya Agano la Kale yanayomtaja Mungu kuwa ni mwamba hayana kusudi jingine kama ulivyosema.

Hebu tuchunguze tena muktadha wa Kiebrania(lugha ya mwanzo iliyotumika kuandika Agano la Kale), katika andiko jingine la Agano la Kale linalosema Mungu ni Mwamba.
Kwa Kiebrania, mwamba ni Tzur, na maana yake ni mwamba mkuu, usioweza kutikisika. Maana hiyo haitofautiani na ile ya Petra(mwamba mkubwa, thabiti).

Angalia Kumbukumbu la Torati 32:4
“Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu; maana njia zake zote ni haki.”
(Kiebrania: הַצּוּר – HaTzur)

Agano Jipya linathibitisha kwamba Mwamba(Petra) ni Kristo
1 Wakorintho 10:4
“...na mwamba huo ulikuwa ni Kristo.”
(Kigiriki: hē petra dē ēn ho Christos)

Andiko hilo linaunganisha vizuri kabisa Agano la Kale na Jipya.

Halafu, hata Petro mwenyewe hakudai kuwa yeye ni Mwamba
Petro anaandika hivi:
1 Petro 2:6-7
“Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima; na kila amwaminiye hatatahayarika. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni..”

Hapo Petro anamtaja Yesu Kristo kuwa ndiye Jiwe Kuu la Pembeni. Jiwe Kuu haliwezi kuwa sawa na jiwe dogo(Petros).

Angalia Mtume Paulo naye anavyounga mkono:
Waefeso 2:20 SRUV
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

Jiwe Kuu la Pembeni ndilo Jiwe muhimu linalofanya jengo(Kanisa)liwe imara. Hivyo Kanisa limejengwa juu ya mwamba/Jiwe kuu la Pembeni(Yesu) na sio Petro.

Daudi anasema katika
Zaburi 18:2
"BWANA ni... Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu."

Ukiwa na Mwamba Yesu, milango ya kuzimu haiwezi kukushinda. Lakini ukimkimbilia binadamu mwenzako ambaye hawezi kuzuia mauti, huwezi kupata msaada.

Ndio sababu mapepo yanakimbia tunapoyakemea kwa Jina la mwamba Yesu. Jaribu ukemee mapepo kwa Jina la Petro au Papa uone kama yatatoka!

Mpaka hapo naamini umeelewa kuwa Petro hastahili kuwa Jiwe Kuu wala Mwamba.
MWAMBA NI YESU TU
 
Na kepha ?
 
Asante kwa ufafanuzi wako, nadhani nilielezea kuhusu tofauti ya Petra na Petros huko nyuma, nikagusia pia kwanini Simoni aliitwa Petros na si Petra. Hata kwa majina ya kiingereza, kireno, kiitaliano na kiarabu tunayoyatumia sasa yana hizo tofauti, Emmanueli na Emmanuela wote asili yao ni Noeli lakini moja linatumika kwa jinsi KE na jingine kwa jinsi ME, Paskali na Paskalina vivyo hivyo.

Kwahiyo hatuwezi kumlazimisha Yesu amuite Simoni kuwa Petra ambayo kwa kiebrania inatumika jinsia KE.

Nilielezea pia utofauti wa maana kati ya mwamba ambapo kanisa litajengwa (ardhi ngumu) na msingi ambao ni Kristo, kwa maana hiyo hiyo naongezea tofauti ya mwamba na jiwe kuu la pembeni. Ukiachana na tofauti ya muktadha katika maneno hayo kutumika ambayo kristo anapotambulishwa kama jiwe kuu la pembeni lililokataliwa na waashi ni kama kuwapa ujumbe wana wa Israel kwamba pamoja na kumkataa kwao na kumuua, lakini yeye ndie atakuja kuwa chanzo cha wokovu wao. Haiongelei habari ya nani atasimamia kanisa.

Ukisoma kwa kutulia huo waraka wa Mtume Paulo kwa waefeso Efe 2:20, utaona Paulo anawaambia wamejengwa JUU YA MSINGI WA MITUME NA MANABII, hiyo nayo inaweza kukueleza kuwa pamoja na Kristo kuwa ndie corner stone, kanisa lake limejengeka katika misingi ya mitume na manabii ambao ndio watu waliozibeba habari hizo, kuzishuhudia kwa watu na kuzitangaza kwa mataifa yote.
 
Kitakachokupa wakati mgumu ni kwamba hao wakatoliki ndio wamiliki wa ukristo, maandiko na historia. So huna budi kuwasaport
 
Ndio sababu mapepo yanakimbia tunapoyakemea kwa Jina la mwamba Yesu. Jaribu ukemee mapepo kwa Jina la Petro au Papa uone kama yatatoka!
Nadhani kuna dhana isiyo sahihi uliyonayo juu ya kanisa Katoliki kuongozwa na Papa, na pia kuamini kwamba Mtume Petro ndie aliekabidhiwa funguo na kundi la kondoo kuwachunga.

Hakuna mahali popote katika mafundisho ya kanisa ambapo Mtume Petro, ama watakatifu wengine wowote wanapotajwa kama chanzo cha wokovu ama kuelezwa waabudiwe. Ni Mungu pekee anaeabudiwa na kutukuzwa katika nafsi zake tatu (Kwa njia yake, pamoja nae na ndani yake, Mungu Baba katika ushirika wa roho Mtakatifu anapata heshima na utukufu wote milele na milele).

Kwahiyo unaposema nijaribu kukemea mapepo kwa jina la Petro ama Papa yeyote nakua sikuelewi. Maana Petro mwenyewe alimponya Kiwete aliewekwa kati lango liitwalo Mzuri kwa jina la Yesu Mdo 3:6.
 
sawa
 
Nadhani kuna dhana isiyo sahihi uliyonayo
Dhana gani tena nyingine ndugu yangu Munamuge
Si umesona hoja zangu zote? Endelea kutafakari kwa kina. Hata mimi mwanzoni, nilikuwa sielewi kwamba Petro ni Petros na mwamba ni Petra.

Petro alijifahamu kwamba yeye ni jiwe dogo, hana uwezo alio nao mwamba Yesu. Ndio sababu hata yeye(Petro) aliponya wagonjwa kwa Jina la Yesu.

Angalia hapa jinsi Paulo anavyoendelea kukazia kuwa mwamba ni Yesu.
Warumi 9:33
Kama ilivyoandikwa: “Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu na mwamba (petra) wa kuwaangusha. Yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe."

Jiulize sasa: Anayetajwa hapo kwamba Yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe ni Petro au ni Yesu?
NI YESU
 
Hicho cheo cha Papa hakipo kwenye Biblia. Mbaya zaidi tafsiri ya kiswahili ni Baba Mtakatifu. Hilo jina tu linapingana na Biblia. Yesu Kristo alionya wanafunzi wake wasiitwe Baba.
Jambo lingine ni kwamba Petro alikuwa kiongozi wa wale mitume 12 ambao wote walikuwa Wayahudi. Hivyo, baada ya Wayahudi kukataa kuamini Yesu Kristo alimteua Mtume Paulo na kumpa wajibu wa kupeleka Injili kwa watu wa mataifa. Hivyo, wakati wa Kanisa la Kwanza kulikuwa na makanisa mawili. Kanisa la Wayahudi makao makuu Yerusalemu na kanisa la Wamataifa ambalo makao makuu yake yalikuwa Antiokia. Hapo Antiokia ndipo wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo. Kabla ya hapo waliitwa Wanazarayo. Sasa kanisa la mataifa liliendelea kuongezeka hadi Roma na Ulaya. Wakristo waliteswa sana na utawala wa Rumi hadi pale kiongozi mmojawapo wa Utawala huo alipopewa maono na Mungu akaamua kuwa Mkristo. Yeye ndiye aliamuru ukristo uwe dini rasmi. Na urasmi huo ndio ulioanzisha cheo cha Askofu Mkuu wa Rona ambaye anaangalia makanisa yote. Huyo Askofu ndiye huitwa Papa. Na kama wanataka kuonesha structure hadi mwanzoni basi Mtume Paulo nduye angekuwa mfano mzuri kwa kuwa yeye ndiye Mtume wa kwanza kuanzisha makanisa ya watu wa mataifa. Isitoshe Paulo hakuoa. Lakini Petro alioa na aliongoza kanisa la Wayahudi ambalo lilisambaratika baada ya wayahudi kupigwa na kufukuzwa kutoka nchi yao mwaka 70 AD.
Kikubwa ni kwamba Yesu Kristo ndiye mwanzilushi wa kanisa na tangu mwanzo ameendelea kuteua viongozi ambao ni Mitume, Manabii, Waalimu, Wainjilisti na Wachungaji. Uaskofu ni cheo cha kidini sio huduma anayotoa Yesu.
 
mimi naona mmeshabadili point mnayojadili

iwe Petro ni Mwamba au sio mwamba vyovyote vile ila point ni kua aliachiwa mamlaka ya kuongoza kanisa
 
mimi naona mmeshabadili point mnayojadili

iwe Petro ni Mwamba au sio mwamba vyovyote vile ila point ni kua aliachiwa mamlaka ya kuongoza kanisa
Aliachiwa mamlaka kwa Andiko lipi, mkuu. Tafadhali weka vifungu vya Biblia hapa
 
Ni mamlaka gani kikanisa (kanisa lolote) ni ya kiMungu?

Yesu aliacha kanisa? Na kama hilo kanisa lipo lenyewe limetoa wapi hayo??

Huu mtililiko wa mapapa toka huyo Petro, wakatoliki walianza kuutumia lini na muasisi wake ndie huyo papa Gregory??
Swali la Kwanza ni kama Sijalielewa Hivi Unazungumzia mamlaka Ipi ya Kimungu ambayo unahisi Kanisa lolote linayo yaani mamlaka ya Kiungozi au kikuhani?

Swali la Pili:
Yesu hakuacha Kanisa ,Aliacha Mitume wake! Na Mitume wake hawakuacha Kanisa pia!

Swali la tatu!

Wazo la Petro kuwa papa wa kwanza ni msimamo wa baadaye wa Kanisa Katoliki nadhani ni kwenye Kaerne ya Pili mapaka ya Tatu hivi na si mafundisho ya mitume wenyewe. Hakuna mahali Petro alijitambulisha kama kiongozi wa ulimwengu wa Kikristo...
Na hata Paulo ameenda Rumi mara Nyingi ameenda Antiokia Mara Nyingi hakuwahi kumtambulisha Petrk kama kiongozi wa Kanisa..

Kuhsu Mtiririko wa mapapa ulianza kufuatiliwa rasmi katika karne ya 3–4, lakini ulirasimishwa kisiasa na kiteolojia wakati wa Papa Gregory I (590–604 BK). Yeye si muasisi wa Kipapa, maana Mapapa walikuwa wengi Dunia Nzima kila Nchinna Kila Ukanda ila lakini yeye ndiye aliyepatia Upapa sura Mpya ya ya kisasa na Kisiasa (papa kama kiongozi mkuu wa ulimwengu wa Kikristo) ambayo hapo Kabla haikuwepo na Rasmi papa wa Roma Akawa Ni papa wa Dunia Nzima..
 
Piga spana mkuu, kwanini mijadala ya namna hii huwa unakimbia mapema??
Sababu Huwa Naogopa Sana Kutengeneza Maumivu upande wa Watu maana Maumivu hugeuka na Kuwa Hasira na Chuki..
Unajua Sometime Ukweli Huwa unakuja na Maumivu makali sana na Mara nyingi Ukweli Unauma Kuliko hata Matusi..

sasa Huwa sipendi Kuusema Ukweli Direct kwa sababu ninaogopa Kuumiza Nafsi za Watu na Kwa bahati mbaya Ukishaumiza nafsi ya Mtu kwa Kumwambia Ukwli Huwa Halifutiki Moyoni atakuchukia hata kama Ukiomba Msamaha...

mwanzoni Kipindi ninaanza Kusema Hivi Vitu nilikuwa Sina Breki wengi waliumizwa Na hivj vitu na Nilijifunza Na Nilionywa Kwenye Ulimwengu wa Roho so naenda Kwa steps sana
Na itakua vizuri zaidi sometimes ukiwa unaambatanisha walau na vitabu ulivyotumia.
Vitabu kwa Maana Ya Biblia Nitafanya Hivyo..
Ila Kuna elimu nyingine Ni ngumu Kuielezea maana inatokana na Maarifa ya Elimu ya Theology niliyosoma, Experiences usomaji wa Vitabu vingi , Kuwepo Kwenye Dini zaidi Ya nne ..

Ila nitajitahidi Kadri ya Uwezo wangu kufanya Hivyo..

Nimepokea Ushauri Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…