Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Contradictions kama hizi ni uthibitisho tosha kwamba Biblia yenu ni HEKAYA.

Ndio maana mnapata mkanganyiko kufahamu nani haswa, Alikuwa Papa wa kwanza.
 
Mleta mada naomba kukufahamisha kuwa Roman Catholic Church na Catholic Church ni makanisa mawili tofauti.
Kwa mtazamo wa kibiblia kanisa la Yesu ni Catholic Church (universal christian church) hili la Roman Catholic ni mchanganyiko wa Ukristo na upagani
 
Ukatholiki haujengwi kwa biblia pekee bali mapokeo ya kihistoria.

Yohana 21:25
Kuna mambo mengine mengi aliyoyatenda Yesu, ambayo kama yangeandikwa moja moja, nadhani hata dunia hii isingeweza kutosha kuviandika vitabu vile.

Sasa jiulize kama Habari ya Yesu full haijaandikwa katika biblia. Hiyo habari nyongine ipo wapi

Kama tu historia ya Bikra Mariamu kuanzia wazazi na uzao wake na kwa jinsi gani aliandaliwa kuwa mama wa Yesu. Haijaandikwa katika Biblia, je ipo sehemu gani

Simaanishi kusema Biblia haijitoshelezi lakini naamini tu kuwa kanisa lolote linaloipinga katholiki kwa kutumia Biblia kama reference pekee.. Naona kama tayari wanajiweka katika nafasi ya kutoelews kina cha ukatholiki.

Kwa hiyo maswali yako ni mazuri na ninatamani kuyajua najiba yake. Ila unahitaji si mtu tu aliyesoma biblia pekee Ila anaijua historia ya kanisa na vyanzo vingine vya taarifa.. Kitu ambacho ni kigumu sana
 
Contradictions kama hizi ni uthibitisho tosha kwamba Biblia yenu ni HEKAYA.

Ndio maana mnapata mkanganyiko kufahamu nani haswa, Alikuwa Papa wa kwanza.
Kuelewa haya mambo huhitaji kusoma Biblia. Soma historia tu inatosha. Mfalme Constantino katajwa kwenye Biblia?
Alexander the Great katajwa kwenye Biblia? Nero katajwa kwenye Biblia?
Majibu ya hii mada yanahitaji uijue Church history.
Kuhusu Biblia hiyo ni shule nyingine
 
Biblia ni hekaya kama hekaya zingine.

Hiyo Church history haiondoi ukweli kwamba Biblia ni hekaya.

Yesu hajawahi kuwepo.

Hao wanaojiita mapapa ni wajanja fulani waliokaa chini kuunda dini ya ukristo kulaghai wajinga.
 
Biblia ni hekaya kama hekaya zingine.

Hiyo Church history haiondoi ukweli kwamba Biblia ni hekaya.

Yesu hajawahi kuwepo.

Hao wanaojiita mapapa ni wajanja fulani waliokaa chini kuunda dini ya ukristo kulaghai wajinga.
Kuhusu uwepo wa Yesu kuna archaeological na historical evidence halafu mtu umeshiba maharage sijui ya wapi unasema Yesu hajawahi kuwepo. Sasa nataka nikeambie wewe ni shetani na sina mda wa kujibizana na shetani, kwenda zako
 
Mkuu yawezakana akawa ndiyo papa wa kwanza. Lakini watakuwa walimfanya au kumhesabu kuwa papa baada ya yeye kufa na sio kwamba yeye mwenyew aliwahi kuhudum kama papa.

Hata mtume paulo huko ugiriki walimwita Mungu baada ya kufanya miujiza kwa bahati nzuri aliwaskia hivyo alipata nafasi ya kuwakemea.

Kwahyo asingeskia kama wamemuita mungu manake huko ugiriki au maeneo mengi dunia kungekuwa na imani ya kumwabudu mtume paulo kama mungu. Na usikute kanisa lingekuwa na utajiri na lenye wasomi wengi tuu wenye kusoma kile kinachoitwa theolojia ya dini yao, kumbe tuu ni vile ambavyo muabudiwa mwenyew hana habari na wanacho kifanya.
 
Ndio...Ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza.
Petro hajawai kuwa papa na hajawai kufika Roma huu ni uongo mkubwa unaoenezwa na wakatoliki kuwahadaa watu waone kanisa lao nila kweli kumbe upagani mtupu huko
 
Petro hajawai kuwa papa na hajawai kufika Roma huu ni uongo mkubwa unaoenezwa na wakatoliki kuwahadaa watu waone kanisa lao nila kweli kumbe upagani mtupu huko
Mkuu...Nipe ushahidi wa hoja Yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…