Je ni kweli mwanaume anaejielewa lazima awe bahili? Toa maoni yako

Kwahiyo wewe uliingia kwenye mgahawa na hao akina Musk ukaona hajagawa tip inayozidi 50$?

Nje ya hao hakuna matajiri wengine ambao huenda wanatumia hela zao bila kuzifanya?

Halafu aliyekuambia kuwa ubahili ni kutokugawa pesa kwa watu bure ni nani?

Bilgate amekuja Tanzania mara kadhaa na matajiri wengi tu wanakuja kila mara
ILA wakija mapumziko hawaingii kwenye media kwa kuwa hawataki watangazwe kwa sababu za kiusalama.

Nakumbuka siku moja Bilgate aliulizwa, kwa nini unatoa tip ya dola $50 wakati mtoto wako ametoa dola $500; akasema huyo ni mtoto wa Bilionea ILA mimi ni mtoto wa seremala niliyepata hela kwa kufanya kazi
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hakika

Mzungu anafundisha mtoto wake ku-save pesa then invest

Mwafrika anafundisha mtoto kuwa bahili, then tena ndio asevu, sasa tutafika lini😁😁
Wanafundishwa kufanikiwa binafsi. Mtu hata ndugu yake afe njaa hajali
 
Kama huamini na Huna aibu basi tafuta watu unaoona ni matajiri kama kumi hivi jaribu kuwaomba kiasi Fulani cha pesa ambacho Kipo ndani ya uwezo wao halafu utaona jinsi watakavyo kukaushia mikausho mikali ndio Utajua maana ya ubahili ni neno Tu watu wanalichukulia sivyo but watu wanaenda na bajeti zao hata kama wanazo...Dunia haina huruma, hata matajiri wakubwa duniani Wana ndugu zao wengi Tu Wana maisha ya kawaida Tu ya kupata pesa za Kula Tu basi.
 
Ubahili ni roho mbaya tu hamna kingine! Mtu unamnyima 20k mama ako/mke/mpenzi/dada/kaka tuseme akafanyiwe matibabu wakati huo huo unapata changamoto isio na tija inakumalizia 50000
Kama katumia elfu 50 pasipo na tija, maana yake wewe kwa wakati huo sio kipaumbele na anayo mahitaji ya msingi na sio kwamba huyo mtu ni habili.

Ubahili wa mtu unapimwa nyanja zote na sio kwa mpenzi, ndugu au rafiki. Wewe unaweza ukamwita bahili sababu akupi pesa, ila yeye akawa anajifanyia mambo makubwa kwa pesa zake hizo hizo
 
Ubahili ni nini ?
Ni ile hali ya kuelekeza pesa kwenye mambo ya msingi na yenye ulazima.
Binafsi marakadhaa wadada wananiita bahiri lkn sioni ubahili wangu uko wapi maan nikweli nafahamika lkn je napaswa kumnunulia kila anae niomba yani ukitamani soda wewe nighalamie mm ukiishiwa vocha wewe nighalamie mm?
 
Bilgate amekuja Tanzania mara kadhaa na matajiri wengi tu wanakuja kila mara
ILA wakija mapumziko hawaingii kwenye media kwa kuwa hawataki watangazwe kwa sababu za kiusalama.

Nakumbuka siku moja Bilgate aliulizwa, kwa nini unatoa tip ya dola $50 wakati mtoto wako ametoa dola $500; akasema huyo ni mtoto wa Bilionea ILA mimi ni mtoto wa seremala niliyepata hela kwa kufanya kazi

Lakini, Baba yake Bill Gates hakuwa sersmala.

"Bill Gates' father, William H. Gates Sr., was a prominent Seattle attorney and co-founder of the law firm Preston Gates & Ellis. His mother, Mary Maxwell Gates, was a schoolteacher who later served on the boards of directors for First Interstate Bank, the United Way, and as a regent for the University of Washington."
 
in fact Yes,
Ukifika hatua fulani ya mafanikio lazima uwe bahili kiasi kwamba inafika mahali ndugu, jamaa na marafiki zako wanakuchukia, but kwa kua wew uko kwenye mission ya kutimiza malengo yako mahususi, kunakuaga na hali ya kua huzingatii tena lawama zao kuhusu ubahili wako wenye malengo 🐒
 
Ubahili ni nini ?
Ni ile hali ya kuelekeza pesa kwenye mambo ya msingi na yenye ulazima.
Binafsi marakadhaa wadada wananiita bahiri lkn sioni ubahili wangu uko wapi maan nikweli nafahamika lkn je napaswa kumnunulia kila anae niomba yani ukitamani soda wewe nighalamie mm ukiishiwa vocha wewe nighalamie mm?
👊
 
Juz nipo gheto akapita zuhura sijui mnamuita zu nini sijui akaniambia we mkaka huna buku tano hapo ukanilee hapo mfukon niko na milion isio na kaz sikutoa
 
Vijana wengi wa Kitanzania wana roho mbaya na ubinafsi.. wanajifichia kwenye ubahili wakidhani ni sifa na wanajisifu...

Ubahili ni roho, ile roho ngumu ya kutoa kitu.. aisee watu wa hivi siwapendi..

Kitakachofanya mtu afanikiwe si ubahili bali nidhamu ya pesa, kujali muda, kuishi chini ya uwezo...

Kwanini nasema ubahili ni upuuzi, mtu bahili hafahamu tofauti ya thamani ya kitu na bei ya kitu...
Umekuta spare ya gari inauzwa moja imara bei ghali na nyingine sio imara bei chini, bahili atanunua ya bei chini, lakini ukija kwa mtu anayejielewa anayefahamu umuhimu wa thamani dhidi ya bei, atachukua spare ghali..

Matajiri wakubwa si bahili, Bill Gate, Warren n.k wanatoa mabilioni kusaidia watu kujenga shule, kuanzisha prigrams mbalimbali , kujenga mahospitali n.k ila bahili hawezi, anaona fedha yake inapotea.. bahili hata awe na milioni kutoa alfu kumi ni vuta nikuvute...

Bahili hata biashara zao kukua huwa ni ngumu, maana ili upate pesa lazima utoe pesa..

Ubahili ni ujinga na upumbavu, kama unategemea ubahili utakufanya uwe tajiri basi endelea kuota...
 
Kimsingi kila mtu ana haki ya kupangia matunizi pesa zake.

Na hutakiwi kufikiria mambo mengi kwa pesa za mtu. Kufanya hivyo unakiwa kama mtu ambaye kashindwa kutengeneza oesa zake, anatamani kutumia za wenzake anavyotaka yeye.

Kama hupendi ubahili, tafuta pesa zako uzigawe tuone unakataa ubahili.

Bila kuwasema vibaya wanaotaka ubahili.

Kwa sababu hata wakifanyia ubahili, hizo ni pesa zao sio zako. Wana haki ya kufanyia ibahiki pesa zao. Tatizo liko wapi?

Sasa pesa za mtu unampangiaje jinsi ya kuzitumia?
 
Hii ndio maana sanifu ya neno "bahili" kutoka kwenye kamusi ya TUKI;
Screenshot_20260708_184416.jpg

Kubania/kuwa mchoyo na pesa yako sio vibaya, sababu ya kufanya hivyo ndo inaweza kuwa nzuri au mbaya.

Maneno "mchoyo" na "bahili" yamefanywa kuwa mabaya kwasababu ya ujamaa, ambapo ni lazima wote tuwe sawa.
 
Kimsingi kila mtu ana haki ya kupangia matunizi pesa zake.

Na hutakiwi kufikiria mambo mengi kwa pesa za mtu. Kufanya hivyo unakiwa kama mtu ambaye kashindwa kutengeneza oesa zake, anatamani kutumia za wenzake anavyotaka yeye.

Kama hupendi ubahili, tafuta pesa zako uzigawe tuone unakataa ubahili.

Bila kuwasema vibaya wanaotaka ubahili.

Kwa sababu hata wakifanyia ubahili, hizo ni pesa zao sio zako. Wana haki ya kufanyia ibahiki pesa zao. Tatizo liko wapi?

Sasa pesa za mtu unampangiaje jinsi ya kuzitumia?
Lengo hapa ni kupeana elimu..

Labda nikuambie tu hao bahili sisi ndio tunaongoza kuwalipia bill kwenye mgahawa, bar n.k.. kama mpo marafiki..

Kibaya zaidi inakuwa tabia inayijirudia kwamba wewe tu ndiye utoe, kwenye msosi na vinywaji wanafurahi kweli kweli bill ikija unashangaa mtu yupo busy na simu.. au anaongea na simu ya maana sana...

Yaani hawana shukurani, pesa anayo ila kuitoa sasa.. anaona kama anakata roho..

Na hii tabia inaua hata mahusiano, unakuwa kwenye dharula ya kifedha lakini rafiki bahili hawezi kukusaidia, sasa urafiki gani huo?

Mtu hata kuchangia shughuli za familia anakuwa mzito..

Bahili yupo radhi hata wazazi wake waishi maisha duni, watoto wasome shule duni.. kisa anaogopa kulipa ada kubwa..

Na jamii ikashafahamu hizo tabia ulizonazo, siku ukipata shida kubwa hakuna mtu atakayejitokeza kukusaidia.

Ubahili ni ujinga...
 
Ushawahi kufikiri kuwa wewe unayemlipia mtu bahili bill kwenye bar, mgahawa etc ndiye unahitaji elimu?

Wewe ndiye unahitaji elimu ya financial literacy. Usiwalipie watu wengine bila sababu.

Hutakiwi kuwalaumu wao, unatakiwa kujilaumu wewe kwa kulipia watu ovyo ovyo. Wao wanakutumia wewe tu kama fursa.

Ushawahi kufikiria hili?
 
Hata Kama Hujielewi Ubahili Ni Sunnah Kwa Mwanaume.....​
 
Back
Top Bottom