Je ni kweli mwanaume anaejielewa lazima awe bahili? Toa maoni yako

Je ni kweli mwanaume anaejielewa lazima awe bahili? Toa maoni yako

Hata Kama Hujielewi Ubahili Ni Sunnah Kwa Mwanaume.....​
 
Umasikini umewafanya kudhani ubahili ndio njia ya mtu mwerevu au mafanikio.

Njia ya mwerevu na mwenye mafanikio ni fikra imara na mtaji.

Unaweza kuwa bahili na usiwe na knowledge ya kumanage ulichokitunza.
Hapa umetetea nn mkuu?
 
Mwanaume anaejielewa hawezi kuwa bahili , ninazo sababu.

1. Mwanaume anaejielewa huipa afya kipaumbele .

Afya na pesa vinahusianaje ?
Usipomuhudumia mpenzi wako nirahisi kushindwa kujimudu kiusafi ,nirahisi kurubuniwa na wengine kwasababu ya changamoto zakiuchumi,nirahisi kupoteza hamu ya tendo la ndoa kwasababu ya msingi wa changamoto zakimaisha .

Sababu hizo zinaweza aidha kumsababishia magonjwa moja kwa moja mwanaume husika kupitia hiyo mwanamke au akayapata baada ya kushindwa kuvumilia changamoto za ndani .

Mwanaume asiyehonga ni nadra sana kufanikiwa kimaisha ,Fanya utafiti utakubaliana na hoja yangu

Mwanaume anaeyakimbia majukumu huwa na changamoto sana kwenye ufanikishaji hata tu wa mipango yake kiuchumi na wengi wao huwa ni watu wa nyeto.

Mwanaume rijali utaachaje kuhonga aisee .

Mnatuhaibisha guys .
 
Lengo hapa ni kupeana elimu..

Labda nikuambie tu hao bahili sisi ndio tunaongoza kuwalipia bill kwenye mgahawa, bar n.k.. kama mpo marafiki..

Kibaya zaidi inakuwa tabia inayijirudia kwamba wewe tu ndiye utoe, kwenye msosi na vinywaji wanafurahi kweli kweli bill ikija unashangaa mtu yupo busy na simu.. au anaongea na simu ya maana sana...

Yaani hawana shukurani, pesa anayo ila kuitoa sasa.. anaona kama anakata roho..

Na hii tabia inaua hata mahusiano, unakuwa kwenye dharula ya kifedha lakini rafiki bahili hawezi kukusaidia, sasa urafiki gani huo?

Mtu hata kuchangia shughuli za familia anakuwa mzito..

Bahili yupo radhi hata wazazi wake waishi maisha duni, watoto wasome shule duni.. kisa anaogopa kulipa ada kubwa..

Na jamii ikashafahamu hizo tabia ulizonazo, siku ukipata shida kubwa hakuna mtu atakayejitokeza kukusaidia.

Ubahili ni ujinga...
Huyo wa kuwategea wenzake sio bahili, ni kupe.
Screenshot_20260708_190223.jpg

Huyo wa kuwasahau watu wa karibu amekosa "life skills" ni wa kuelimishwa kidogo.
 
Hata Kama Hujielewi Ubahili Ni Sunnah Kwa Mwanaume.....​
 
Ushawahi kufikiri kuwa wewe unayemlipia mtu bahili bill kwenye bar, mgahawa etc ndiye unahitaji elimu?

Wewe ndiye unahitaji elimu ya financial literacy. Usiwalipie watu wengine bila sababu.

Hutakiwi kuwalaumu wao, unatakiwa kujilaumu wewe kwa kulipia watu ovyo ovyo. Wao wanakutumia wewe tu kama fursa.

Ushawahi kufikiria hili?
Wewe umejuaje mimi nalipia watu hovyo hovyo?

Lengo hapa ni wao wapate kufahamu wanachofanya ni ujinga..

Mimi napenda kutoa lakini si fala wa bwege hata siku moja.. na mtu hawezi kunitumia nina boundaries..

Ikishatokea mara moja, mbili tatu.. basi naweka boundaries..
 
Ukimlipia mtu bahili, unamlilia mtu ovyo tu. Huna financial discipline.

Wao hawafanyi ujinga, wanatumia fursa ku exploit wajinga, mjinga ni wewe hapo.

Huelewi wapi?
 
Kuna ubahili wa aina nyingi mzee upo ubahili wa faida na upo ubahili wa hasara kuna mtu ili ashibe inabidi ale chakula cha 5000 ila anaamua ale chakula cha 2000 ili 3000 akaweke kwenye kibubu
 
Vijana wengi wa Kitanzania wana roho mbaya na ubinafsi.. wanajifichia kwenye ubahili wakidhani ni sifa na wanajisifu...

Ubahili ni roho, ile roho ngumu ya kutoa kitu.. aisee watu wa hivi siwapendi..

Kitakachofanya mtu afanikiwe si ubahili bali nidhamu ya pesa, kujali muda, kuishi chini ya uwezo...

Kwanini nasema ubahili ni upuuzi, mtu bahili hafahamu tofauti ya thamani ya kitu na bei ya kitu...
Umekuta spare ya gari inauzwa moja imara bei ghali na nyingine sio imara bei chini, bahili atanunua ya bei chini, lakini ukija kwa mtu anayejielewa anayefahamu umuhimu wa thamani dhidi ya bei, atachukua spare ghali..

Matajiri wakubwa si bahili, Bill Gate, Warren n.k wanatoa mabilioni kusaidia watu kujenga shule, kuanzisha prigrams mbalimbali , kujenga mahospitali n.k ila bahili hawezi, anaona fedha yake inapotea.. bahili hata awe na milioni kutoa alfu kumi ni vuta nikuvute...

Bahili hata biashara zao kukua huwa ni ngumu, maana ili upate pesa lazima utoe pesa..

Ubahili ni ujinga na upumbavu, kama unategemea ubahili utakufanya uwe tajiri basi endelea kuota...
Mbona kama anataka watu waishi unavyotaka wewe? Mtu akiwa bahili wewe unapungukiwa nini? Pesa ni yake, acha aende nayo vile anavyotaka yeye maadam kaitafuta mwenyewe..

Yaani huwapendi wakati pesa wametafuta wenyewe..
 
Ukimlipia mtu bahili, unamlilia mtu ovyo tu. Huna financial discipline.

Wao hawafanyi ujinga, wanatumia fursa ku exploit wajinga, mjinga ni wewe hapo.

Huelewi wapi?
Wewe naye utakuwa ni bahili..

Naona hata hunielewi..

Mimi silalamiki hapa, nimeshakuambia tunapeana elimu, tunapeana facts.. nani analalama?

Kulinda heshima na mahusiano sio ujinga, ni uwekezaji.

Matajiri wakubwa wenye akili wanajua thamani ya mtandao wa watu , social capital.
Ukimfanyia mtu ubahili na tabia za kikupe kwa kigezo cha kutumia fursa, unajijengea sifa ya uaminifu mdogo , low integrity...

Hakuna tajiri duniani aliyepata utajiri kwa kukwepa bili za mlo au vinywaji...
 
Whether mimi ni bahili au si bahili si issue.

Issue ni kwamba wabongo wengi kama wewe mnalialia sana kwa mambo ambayo yapo katika maamuzi yenu.

Mtu pesa zako, una maamuzi yote kulipia mtu au kutolipia.

Unalipia halafu unalialia watu mabahili sana, unawalipia.

Hujioni kuwa wewe mwenyewe ndiye mjinga hapo?
 
Kiukweli utamaduni wa kijamaa na kijima umefanya mambo mengi ya basic financial literacy kuonekana kuwa ni ubahili.

Kwa mfano, mtu akijiwekea bajeti, akakataa kuivunja, Waswahili wengi mtamuita mbahili.

Mtu akijiwekea malengo ya ku invest kwa maisha yake ya baadaye, akakataa kutumia pesa kijinga, mtamuita mbahili.

Mtu akikataa kuishi kama Kimwaga anayehongahonga wanawake ovyo, mtamuita mbahili.

Mtu akikataa maisha ya kufanywa ATM na ukoo mzima, mtamuita bahili.

Tatizo ni la jamii, si la huyu mtu anayejipangia matumizi mazuri ya pesa zake.

Kama hupendi mtu kutumia pesa zake kwa hicho unachoita ubahili, tafuta zako uzitumie unavyotaka bila ubahili.
Mkuu huu ndio ukweli kabisa.
 
Whether mimi ni bahili au si bahili si issue.

Issue ni kwamba wabongo wengi kama wewe mnalialia sana kwa mambo ambayo yapo katika maamuzi yenu.

Mtu pesa zako, una maamuzi yote kulipia mtu au kutolipia.

Unalipia halafu unalialia watu mabahili sana, unawalipia.

Hujioni kuwa wewe mwenyewe ndiye mjinga hapo?
Nani analia lia? Mimi nipo hapa kutoa elimu.. kwa mafanikio yao wenyewe..

Siwezi kuwa bahili , hio roho sina.. na haitotokea.. na sijapungukiwa chochote..

Usinifundishe roho mbaya.. sikuzaliwa hivyo..
 
Back
Top Bottom