Je, ni kweli RC Paul Makonda alikuwa Dodoma usiku wa kuamkia leo?

Je, ni kweli RC Paul Makonda alikuwa Dodoma usiku wa kuamkia leo?

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
131
Reaction score
379
Heshima kwenu Wanajamvi,

Nmeanzisha thread hii kudadisi au kuconnect Dot kuhusiana na Mambo yanayoendelea Dodoma.

Leo Jumanne 09 Juni 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, aliandaa Mkutano na Madereva Bodaboda. Sijajua alitaka kuongelea nini, lakini ni kwamba aliwakusanya Madereva wote Bodaboda maeneo ya Leaders Club Wilayani Kinondoni mkoani Dar Es Salaam kuanzaia Saa Mbili asubuhi.

Ilipofika Saa Sita na Nusu bado Mkuu wa Mkoa alikuwa hajafika, kitendo kilichofanya Madereva bodaboda kuanza kulalamika kwamba wanachelewa kwenda kufanya kazi. Akatokea mtu mmoja akaropoka kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda hatafika kwani yupo Makao Makuu ya Nchi.

Bodaboda kusikia hivyo walianza kutawanyika na kuelekea kwenye Vituo vyao vya kazi. Pamoja na kwamba MC wa Shughuli aliwasihi kurudi na kusubiri Mkuu wa Mkoa afike kwani huwezi jua kawaandalia nini, Waligoma katakata.

Hata hivyo, baada ya muda, yule Jamaa aliyetangaza kwamba Mkuu wa Mkoa hatafika Leaders Club, akakamatwa na Watu wanaodaiwa ni UVCCM wakamkabidhi kwa Polisi ambao walimkimbiza na kumpakia kwenye gari la Polisi.

Swali langu ni: Je, ni kweli Paul Makonda jana alienda Dodoma? Alienda kufanya nini?

 
Rais wa Nchi yupo Dodoma, Je ni kosa mkuu wa Mkoa kwenda Makao Makuu ya Nchi? Kama rais lazima apate taarifa kila siku za kila mkoa
 
Kuna mambo mengine kutamkwa tamkwa kila tukio baya linapotokea linampa mtu ubabe mkubwa kuliko hata alionao. Bashite ni dhaifu mmoja tu anaetumia madaraka aliyopewa kujinasibu kama vile ni gangwe fulani lakini kiukweli zaidi ya porojo hana hata ujasiri wa kuua mende. Pengine hajatokea makusudi ili kuwapa watu msemo tu.
 
Kwaio makonda mnavyo mwita nanii kila siku kuwa hawez kufanya kitu chochote Ila leo kaweza Kum kanyaga Mbowe?

Imana ametoka dar kwenda kumkanyaga mbowe?
 
kwani alikosekana mwakilishi wa RC kuelezea agenda badala ya kuhairisha kikao
 
Aisee, watu mnajua kuunganisha dots
 
Wamarekani watakuwa wanajua

Ama Pompeo ataongeza vikwazo kwake na huenda mataifa mengine nayo yatatoa ishara za uhusika wake
 
Naona umeamua kushika dodoki
Kuna mambo mengine kutamkwa tamkwa kila tukio baya linapotokea linampa mtu ubabe mkubwa kuliko hata alionao. Bashite ni dhaifu mmoja tu anaetumia madaraka aliyopewa kujinasibu kama vile ni gangwe fulani lakini kiukweli zaidi ya porojo hana hata ujasiri wa kuua mende. Pengine hajatokea makusudi ili kuwapa watu msemo tu.
 
Back
Top Bottom