Vipindi vya swala
Quran 73:20,11:114,20:130,17:78-79,30:17-18,24:58
Udhu
2:222,5:6,4:43
Kuelekea kibla 2:144
Ndoa
2:221,4:22-32
Mahari 4:24
Talaka
65:1-6,12
2:231,2:226-237
Kijana ujue unajadili na mwanazuoni mbobevu, mwanatheolojia wa degree ya Engineering na theolojia ,mwanahistoria
Kwahiyo usijibu kihuni, ndio maana umebandika tu hizo Aya ,UKIJUA unajadili na mtu wa kawaida tu ,
Tuanze na swali la kwanza nilikuomba idadi ya Swala Tano na Namna ya Kuzitekeleza, Aya za
Qur'an ulizoleta zinataja nyakati za swala kwa ujumla, lakini haibainishi kuwa ni tano wala kueleza jinsi ya kuziswali. Aya kama 11:114, 17:78-79, 20:130, na 30:17-18 zinataja nyakati za swala, lakini hazisemi wazi kuwa swala ni tano wala kueleza rakaa zake.
Kama Qur'an pekee inatosha, basi wapi kuna maelezo ya rakaa za kila swala, sifa za swala kama Takbira, Rukuu, na Sujudi?
Swali la 2 nilikuomba Sheria za Zaka,Aya za ,Qur'an ulizoleta zinataja umuhimu wa kutoa zaka (2:267, 9:60), lakini hazisemi kiwango maalum cha makato (asilimia 2.5% ya mali, n.k.).
Ikiwa Hadith si muhimu, je, unaweza kuonyesha wapi Qur'an inasema kiwango cha makato ya zaka kwa pesa, biashara, mifugo, au mavuno?
Swali la 3 nilikuomba Maelezo ya Kina Kuhusu Hija, Aya za Qur'an ulizoleta zinataja Hija na Umra (2:196, 3:97), lakini hazijaeleza hatua kwa hatua jinsi ya kuitekeleza, kama vile:
Idadi ya tawafu
Umuhimu wa Sa'i kati ya Safa na Marwa
Kuanza na Ihram
Kusema "Labbayk Allahumma Labbayk"
Kupiga mawe Jamarat
Bila Hadith, je, unaweza kueleza wapi Qur'an inaeleza hatua zote za Hija?
Swala la 4 nimekuomba Adhabu za Vilevi na Makosa Mengine ya Jinai
Aya ULIYOILETA Qur'an inakataza ulevi (5:90-91), lakini haisemi wazi adhabu yake ni ipi.
Kwa uzinzi, Qur'an inataja kupigwa viboko (24:2), lakini haijaeleza adhabu kwa waliokwisha oa (rejea Hadith kuhusu rajm kupigwa mawe hadi kufa).
Kwa wizi, Qur'an inasema mkono ukatwe (5:38), lakini haielezi mipaka kama thamani ya kitu kilichoibwa au mazingira maalum.
Swali la mwisho niliomba Maelezo ya Mahitaji ya Ndoa na Talaka,katika Aya ulizoleta Qur'an inataja ndoa na talaka (2:221, 4:22-32, 4:24, 2:226-237, 65:1-6), lakini haielezi:
Jinsi ndoa inavyofungwa
Mashahidi wa ndoa ni wangapi?
Mimba inapoingilia talaka
Utaratibu wa iddah kwa talaka tofauti
NJOO UJIBU MASWALI KWA UFASAHA
NATAKA HADI UIKANE QURAN KAMA ULIVYOZIKANA HADITHI