Dah!! Umenikumbusha mbali sana. Mimi nilikatazwa na mama yangu mzazi. Nakumbuka siku hiyo niko na mchumba mwenyewe (nakiri wazi, kati ya wanawake ambao walikufa na kuoza kwangu huyu ni mmoja wapo) nikampigia mama simu na kumpa maelezo kisha wakasalimiana. Mchumba mwenrwe akafurahi sana, aliponirudishia simu mama akaanza kuniambia kwa kilugha jinsi walivyo (sikuwa nalijua hili na nilielezea nikijua ndio kujimwambafy kwa mama kumbe ndio naharibu) aliniambia afadhali uoe hata mwanamke mwenye sura kama wasira, kuliko mrembo wa kinyarwanda (hakujua kabila. Nilimwambia huyu ni mnyarwanda). Sitasahau jinsi mdada wa watu alilia tulipoachana na hata hakujua shida ni nini maana ilibidi nianze vitimbwi mpaka akahama kabisa na hadi leo sijui wapi alipo. Tulikutana mara moja alipokuja kwenye mahafali ya mdogo wake. Tulikutana kwenye gari, alinisema sana, alilaumu hakuna mfano japo tayari ilikuwa imepita miaka mitatu tangia tuachane. Gari nzima walikuwa wakitusikiliza hadi nikaona aibu. Hakuniambia anaishi wapi ila alinionesha picha ya mumewe mtarajiwa😡😡😡