Je ni kweli vinyama vina ladha tofauti au sababu ya wanaume kuendelea kuchepuka ni ipi?

Je ni kweli vinyama vina ladha tofauti au sababu ya wanaume kuendelea kuchepuka ni ipi?

Wanaume ambao mko kwenye mahusiano nawaombeni hapa.
Jana kuna binti amekuja kwenye kikundi analia, mume wake amezalisha mtoto wa pili nje ya ndoa.

Hivi, mkichepuka au mkabadilisha hiyo michepuko kuwa nyumba ndogo za kudumu, huwa mnatafuta nini hasa kati ya hivi?
  1. Ladha tofauti za kipochi manyoya (zinazochochewa na tamaa na mihemuko ya hovyo)

  2. Utulivu halafu mnanogewa

  3. Utundu na ufundi wetu mishangazi au vibinti vya alfu mbili

  4. Faraja na amani mnayoikosa nyumba kuu

  5. Au ni tabia mbovu tu za kihuni

Elezea jibu lako kwa undani na ruksa kuchagua jibu zaidi ya moja.
Vyote hivyo ni kweli,Ila kila mtu anajua cha kwake
 
Gharama zipo ila ni stahimilivu otherwise hiyo nyumba ndogo iwe maeneo ya kishua sana na nyumba yenyewe iwe ya viwango vya juu sana. Lakini nyumba nyingi ndogo huku kwetu hazina mambo mengi ni chumba kimoja, sebule, jiko na CHOO KIZURI kitu ambacho ni maradufu kama ukiamua kuwa na jumba kubwa
Haya buana, mimi ni nani nikubishie :peepoPantsWalk:
 
Enyi wanawake mkishapata watoto na waume zenu msijisahau kuwa waume zenu ndio watoto wenu wa kwanza. Maana wao ndio wakwanza kuwanyonyesha kipindi mnapata watoto
Na tunavyopenda kuwanyonyesha, tatizo mnatuachia mizigo ya malezi peke yetu, tunachoka sana mpaka tunashindwa kujigawa.
 
Huwezi kula nyama kila siku na muda wote,,kuna siku utamisi mlenda dagaa au samaki.
Sawa, mkeo pia mfikirie kwa hilo, uwe unamuachia achia anajaribu karoti, matango, au bamia na siyo kila siku biringanya lako tu.
 
Na tunavyopenda kuwanyonyesha, tatizo mnatuachia mizigo ya malezi peke yetu, tunachoka sana mpaka tunashindwa kujigawa.
Mimi na mama watoto wangu tulikua tunapeana zamu ya kubembeleza mtoto usiku ,akimaliza kunyonyesha mimi namcheulisha mpaka alale.
Afu kesho naenda job,ili badae nipate chuluruu.
 
Siku mkijua binadamu nayeye ni mnyama mtaacha kuuliza haya maswali!, binadamu kinachomchanganya na kumzuzua ni anapambana na asili mbili yani kuna muda anafuata tamaa za mwili na kuna muda anafuata utashi wa akili!.

Akili mambo yake ni kufuata sheria na tamaa hufuata hisia!, kinachoshinda ndio huwa kinachukua nafasi kwa muda huo. na ndio maana baadhi ya matendo mtu huyafanya halafu baadae akija kuulizwa hana majibu maana unauliza kitu kilichotumia tamaa kujibu jibu la mantiki!.

So yote kwa yote mi nionavyo kuna vitu hatujavifahamu bado na ndio maana ni ngumu kuwa perfect kwa asilimia mia moja, hiyo ni kwa utashi wetu ila kwa kilichoifanya asili yetu chenyewe ndo kinaona tupo sahihi!.

Tufanye tunayoyaweza kwa usalama hilo ndo lakuzingatia zaidi.
Mfalme Suleiman yeye tu alkua na wanawake 700 na michepuko 300 imagine, na kati ya hao wanawake zake walikua na sifa za kila aina ambazo kila mwanaume anataka mwanamke wake awe nazo..
 
Back
Top Bottom