Je, ni magaidi wenyewe ndio wanajifungamanisha na uislam au waandishi wa habari ndio wanaoufungamanisha ugaidi na uislam

Je, ni magaidi wenyewe ndio wanajifungamanisha na uislam au waandishi wa habari ndio wanaoufungamanisha ugaidi na uislam

Amejimaliza wapi na ndiyo anawafyeka magaidi wa Hamas kwa speed ya 5G.
Kwa upeo wako unaweza kuona hivyo ila wenye uelewa wa sheria na mambo ya kimataifa wanona kama kajimaliza na kaiangamiza israel akiwemo former mp wa israel ehud barak
Sasahivi ukiwa jew nje ya israel huna amani na unatengwa hata kwenye michezo na mambo ya kimataifa
Kiongozi wa nchi amekuwa kama kibaka wa manzese na amepewa status ya criminal na hadi nchi za ulaya zimeapa kumkamata sasa utaenda vipi kwenye mikutano ya kimataifa
Hadhi ya taifa la israel imeharibiwa na inaonekana kama kikundi cha wahuni tu mbele ya jumuia ya kimataifa hadj waisrael wenyewe wanaandamana kupinga sera za nchi yao
European union inafikiria kuiwekea vikwazo israel
Ndio maana nasema wenye akili wameshaona isael kapoteza na ndio maana tunasema mungu ana njia zake za kumuangamiza mtu taratibu bila ya yeye kujua
 
Dunia ina Waislam 1.8 bilion ambao kila siku wanasali kuilaani Israel lakini Allah wala hajibu maombi yao kamwacha Israel aendeleze kichapo kwa waumini wake....kuna shida mahali siyo bure
Hata farao na hitler walijidanganya hivyo hivyo ila muda ni mwalimu mzuri , na mungu hapangiwi anafanya kila kitu kwa wakati anaotaka yeye
 
Si sahihi, uislamu unakataza kwenda kinyume na amri za Mungu, mtume na serikali yenye mamlaka kutoka kwa wananchi, yeyote anayefanya uhuni kwa kisingizio cha uislamu huyo ana personal interest na hicho anachokifanya, kuhusu baadhi ya ayah za quran zilizoamrisha kupigana ziliteremka madina zenyewe zililenga kuwapa ruhusa waislamu wa wakati huo kujihami na kulipa kisasi kwa maovu waliyofanyiwa pasipo na sababu za msingi kutoka kwa watu wa Makkah ambao walikuwa waabudu masanamu wenye chuki binafsi dhidi ya muhammad na wafuasi wake, na ndio maana kwa sasa hakuna nchi ya kiislamu inayolingania kwenye jihad kwa sababu waislamu wa dunia ya leo wako mbali na manyanyaso kutoka kwa wasio waislamu, lakini tumeshuhudia matukio kadhaa ya kibaguzi dhidi ya uislamu wakati huo huo viongozi wa mataifa mengi ya kiislamu wameishia kulaani kwa maneno na sio mapigano kwa sababu kwa sasa hakuna hoja ya msingi ya kupigana, kinachoendelea gaza na Israel ni vita ya uhuru wa kitaifa na maslahi ya kisiasa, kadhalika katika maeneo mengine duniani kuna makundi yanayozozana kimaslahi na si kidini.

Uislamu unaamrisha amani na upendo kwenye jamii.
Tatizo ni pale vikundi hivyo ya kigaidi vinavyojitambulisha kama wafia Uislam vinapofanya mauaji wapo Waislam wanavishabikia hata huku jukwaani wamo.
 
Kuna Propaganda mpya dhidi ya Waislamu.

Wako wanaofurahia propaganda hizo.

Wako wanaoamini propaganda hizo.

Wako wanaolipwa kwa kuandaa propaganda hizo.

Propaganda hivi zimaendezwa kwaa media kupitia waandishi

Lakini wapo waandishi waliotaka kujua ukweli wa ugaidi. Kuwa ni magaidi wenyewe ndio wanaojinasibisha na Uislam au ni waandishi wenziwao ndio wanaoufungamanisha Uislam na Ugaidi.

Mmoja wa waandishi hao ni AZORY. Hata hivyo alipotaka kutekeleza jukumu hilo alipotezwa na watu wasiojilikana. Kila mmoja unaelewa ni nani wasiojilikana kuwa ni watu waliosikiliza amri kutoka juu.

Hata hivyo limejitokeza akina Azory wa Bandia. Wameweza kukusanya uchunguzi na kuzungumzia ugaidi wa waislam.

Kundi hilo linauzungumzia ugaidi kwa ustadi zaidi ya waongoza muvi za BOLLYWOOD wa na wasimulia muvi wa kule tandale.

Cha ajabu wameyafanya yote na hatimae kuanza kusambaza kwenye mitandao.

Hata hivyo kikundi hiki kinafanya yote haya kama kwamba tz ni sehemu salama kwao kujificha kwa kutengeza na kusambaza uongo uliotengezwa huku wakikingiwa kifua.

Waislam nchini wanaitahadharisha SERIKALI izingatia zaidi maslahi ya Taifa katika kuiendea na kuishughulikia dhana ya ugaidi nchini.

Kuna waandishi hao ambao jf inawalinda wameendelea kuandika makala zinazozungumzia ugaidi wa Waislamu nchini na kwa nchi za jirani.

Kuna waraka wenye anuani ya Njua ya Kibiti kwenda kwenye laana Cabo Delgado.

Moja ya suala linalojitokeza katika makala hiyo ni Uislamu na ugaidi, ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi lakini kwa hakika yeye (Mwandishi) ndiye anayehusisha Uislamu na Ugaidi.

Tunawashauri viongozi wazingatie zaidi maslahi ya Taifa katika suala hili la ugaidi, kwani sasa zimeanza kuibuka propaganda mpya za ugaidi zinazo wanasibisha Waislamu.

Tunaishauri serikali ifute kabisa sheria ya ugaidi na badala yake itumie shera ya uhalifu ambao ipo ili kuwapumzisha na kuwaondolea waislam wasiwasi wa operasheni zinazoibuka baada ya kuanza kwa propadanga hizi ili niweze kuhalalisha uovu wa baadhi ya watendaji wa serikali waovu, wavuta bangi waliopandikizwa chuki kupitia propaganda hizi dhidi ya Waislamu.

Tunaikumbusha Serikali kwamba, Taifa la Tanzania limejengwa juu misingi mitatu ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.

Na huu mpango mpya wa propaganda zenye uongo uliotengenezwa si ktk misingi sahihi ya kuendesha serikali.

Waraka huu umesomwa na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwa waislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.

Ameeleza kuwa mwaka 2002, wakati wa mchakato wa Sheria ya Ugaidi, Wabunge walisema maneno mazito Bungeni, na kufafanua kuwa Tanzania hakuna ugaidi na Sheria hiyo ya Ugaidi inawalenga zaidi raia Waislamu.

Akasema, hivi sasa matokeo ya utekelezaji wa Sheria hiyo yanaonekana wazi kwani wanaokamatwa na kutuhumiwa kwa ugaidi wengi wao ni Masheikh na Waislamu wa kawaida.

Lakini la kusikitisha zaidi ni kwamba hata kesi zake mahakamani zinakwama kusikilizwa na Waislamu wakabaki wafungwa mahabusu wa muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu makala hayo Sheikh Ponda, anasema ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi, lakini makala hiyo ipo wazi kuwa yeye ndiye anayehusisha Uislamu na ugaidi.

Akifafanua Sheikh Ponda, amesema Mwandishi wa Makala hiyo amewataja Waislamu wasomi wa Vyuo vya Kiislamu kama Magaidi huku Misikiti, Madrasa, Asasi kama vile vituo vya Yatima na Shule za Kiislamu amevitaja kuwa ni vituo vya Kigaidi.

Aidha amesema, katika makala yake hiyo ameyataja mataifa kadhaa aliyodai kuwa yanayoelekea kusambaratika kutokana na hicho alichokiita ni ugaidi.

Sheikh Ponda amemtanabahisha mwandishi huyo kuwa uandishi wake unatakiwa azingatie maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusu suala hili zito linalohusu uhai wa watu na mustakbali wa Taifa, badala ya kuja na uchambuzi wa taarifa bandia za Intelijensia.

Kwani taarifa sahihi anazo Azory.
 
Kwa hiyo vile unavyoona ndege za Israel zikiwalenga wagonjwa mahistipalini, watoto na wanawake ktk kambi za wakimbizi wao si magaidi

Tulionao wamarekani waliofanya kama hivyo wao si magaidi.

Na wale vibaka wanaokaamatwa na kuchomoka moto. Iwapo waliomchoma moto ni wakristo itakuwa sahihi tukisema ukristo ni ugaidi.

Turudi kwa kikundi cha lord resistance army kule uganda je wao ni magaidi?

Ktk mauwaji yaliyotokea Rwanda taarifa sahihi ni kuwa raia watutsi waliokimbilia kanisani askofu wa kanisa aliwapigia wanajeshi wa kihudu na wanajeshi walikwenda kanisani na kuwatoa uhai. Je ukristo si ugaidi

Swali langu ni jepesi. Ugaidi ni nini hasa. Kila muislam anapofanya uhalifu, uhalifu huo ndio ugaidi.

Au waandishi wa habari za ugaidi ndio wanaonasibisha uislam na ugaidi.
 
Uliona wap dini inawafundisha waumini wake karete na Judo?...ni uhayawani mtupu....mbaya zaid wanashauriana wazaliane wengi ili wawe wengi Nchini na kuweza kuweka utawala wa kiuslamu...wasichikijiua elimu ya kushawishi hawana zaid tu ya kulalamika kwa kila jambo na kuongeza mzigo kwny familia kwa kigezo Cha kuwa wengi
 
Tatizo ni pale vikundi hivyo ya kigaidi vinavyojitambulisha kama wafia Uislam vinapofanya mauaji wapo Waislam wanavishabikia hata huku jukwaani wamo.
Huenda wao wakawa ni majuha kuhusu misingi ya 'jihad' na sifa zake na vipi inatakiwa kuwa au sababu za kuwepo kwake,,,,!!!

Ndio maana haijawapo kusikika kutoka kwa prominent and most influential muslim scholars wa Tanzania au popote pale duniani wanaohamasisha jihad in the universe kwa sasa!!!

Hao wanaoshabikia hayo mapigano hawana tofauti na mashabiki wa kisiasa waliofeli kiasi cha kuomba itokee vita au coup d'etat.
They are not patriots
 
Huenda wao wakawa ni majuha kuhusu misingi ya 'jihad' na sifa zake na vipi inatakiwa kuwa au sababu za kuwepo kwake,,,,!!!

Ndio maana haijawapo kusikika kutoka kwa prominent and most influential muslim scholars wa Tanzania au popote pale duniani wanaohamasisha jihad in the universe kwa sasa!!!

Hao wanaoshabikia hayo mapigano hawana tofauti na mashabiki wa kisiasa waliofeli kiasi cha kuomba itokee vita au coup d'etat.
They are not patriots
Hamna jihad hapo ni utapeli yaani mtanzania akapigane somalia ni jihad gani? Jihad watu wanalipwa ? Jihad ambayo wanapigana kweny makazi ya watu ?

Hao ni matapeli nchi za kiislamu huwakuti wananyongwa mapema.
 
Islam is a religion of conquest. Sehemu yoyote walipo wanataka complete control ya taasisi na mifumo yote ktk nchi.
Wakristo walikuwa wanafanya kbla ya milenia mpya na walimwaga damu nyingi sana.
bado dini yao haija-mature kwasababu ktk Abrahamic religions ynyewe ndio changa. They will evolve eventually
 
ni magaidi wenyewe ndio wanajifungamanisha na dini ili kupata cheap labour ya wapiganaji wa bure wa kuwalipa wali maharage tu baada ya kuwafanyia brainwash vijana wasio na ufahamu wowote kuhusu imani ya dini yao zaidi ya mihemuko tu. makundi ya kigaidi yapo yajifungamana na Ukristu mfano Lord Restichance Arm la Jo seph Konny na la Ant baraka la central africa,yapo yaliyojifungamana na uislam eg boko,alqaeda,alshahb nk.makundi yote haya hayapiganii dini bali maslai ya kidunia thus viongozi wake wote wanaishi maisha ya kifahari ya wanawake pombe na anasa huku wapumbavu wa chini wakiwabrainwashed kwa sababu wao ni vipofu hawajui lengo la kundi.Makundi yote haya yanafanya matendo kinyume na mafundisho ya dini mfano kuua watu wasio na hatia,kufanya biashara haramu ili kupata pesa za kuendesha kundi mfano kuuza madawa ya kulevya,kuuza viungo vya binadamu baada ya kuwaua mateka,usafirishaji haramu wa binadamu,uuzaji wa silaha kuuza wanawake kwenye madanguro nk,je dini ngani imeruhusu haya.Kwann vijana wa kiislamu ni wengi wanasapoti makundi haya ishu ni hapa ni elimu na uelewa kuhusu falsafa ya makundi haya ndo hawana.
 
SEMA NINI BRO,
NINYI MNA POOR THINKING AND REASONING CAPACITY.
UMEELEWA NILICHO ANDIKA?
Nimekufahamu hivi. wasomi wengi na maprof wengi tz ni waislam na wameifanya kuwa maskini. ingalikuwa wakiristo ndio wasomi wengi tz tz ingalikuwa kama Ulaya.
 
Back
Top Bottom