Je, ni magaidi wenyewe ndio wanajifungamanisha na uislam au waandishi wa habari ndio wanaoufungamanisha ugaidi na uislam

Je, ni magaidi wenyewe ndio wanajifungamanisha na uislam au waandishi wa habari ndio wanaoufungamanisha ugaidi na uislam

Kuna Propaganda mpya dhidi ya Waislamu.

Wako wanaofurahia propaganda hizo.

Wako wanaoamini propaganda hizo.

Wako wanaolipwa kwa kuandaa propaganda hizo.

Propaganda hivi zimaendezwa kwaa media kupitia waandishi

Lakini wapo waandishi waliotaka kujua ukweli wa ugaidi. Kuwa ni magaidi wenyewe ndio wanaojinasibisha na Uislam au ni waandishi wenziwao ndio wanaoufungamanisha Uislam na Ugaidi.

Mmoja wa waandishi hao ni AZORY. Hata hivyo alipotaka kutekeleza jukumu hilo alipotezwa na watu wasiojilikana. Kila mmoja unaelewa ni nani wasiojilikana kuwa ni watu waliosikiliza amri kutoka juu.

Hata hivyo limejitokeza akina Azory wa Bandia. Wameweza kukusanya uchunguzi na kuzungumzia ugaidi wa waislam.

Kundi hilo linauzungumzia ugaidi kwa ustadi zaidi ya waongoza muvi za BOLLYWOOD wa na wasimulia muvi wa kule tandale.

Cha ajabu wameyafanya yote na hatimae kuanza kusambaza kwenye mitandao.

Hata hivyo kikundi hiki kinafanya yote haya kama kwamba tz ni sehemu salama kwao kujificha kwa kutengeza na kusambaza uongo uliotengezwa huku wakikingiwa kifua.

Waislam nchini wanaitahadharisha SERIKALI izingatia zaidi maslahi ya Taifa katika kuiendea na kuishughulikia dhana ya ugaidi nchini.

Kuna waandishi hao ambao jf inawalinda wameendelea kuandika makala zinazozungumzia ugaidi wa Waislamu nchini na kwa nchi za jirani.

Kuna waraka wenye anuani ya Njua ya Kibiti kwenda kwenye laana Cabo Delgado.

Moja ya suala linalojitokeza katika makala hiyo ni Uislamu na ugaidi, ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi lakini kwa hakika yeye (Mwandishi) ndiye anayehusisha Uislamu na Ugaidi.

Tunawashauri viongozi wazingatie zaidi maslahi ya Taifa katika suala hili la ugaidi, kwani sasa zimeanza kuibuka propaganda mpya za ugaidi zinazo wanasibisha Waislamu.

Tunaishauri serikali ifute kabisa sheria ya ugaidi na badala yake itumie shera ya uhalifu ambao ipo ili kuwapumzisha na kuwaondolea waislam wasiwasi wa operasheni zinazoibuka baada ya kuanza kwa propadanga hizi ili niweze kuhalalisha uovu wa baadhi ya watendaji wa serikali waovu, wavuta bangi waliopandikizwa chuki kupitia propaganda hizi dhidi ya Waislamu.

Tunaikumbusha Serikali kwamba, Taifa la Tanzania limejengwa juu misingi mitatu ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.

Na huu mpango mpya wa propaganda zenye uongo uliotengenezwa si ktk misingi sahihi ya kuendesha serikali.

Waraka huu umesomwa na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwa waislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.

Ameeleza kuwa mwaka 2002, wakati wa mchakato wa Sheria ya Ugaidi, Wabunge walisema maneno mazito Bungeni, na kufafanua kuwa Tanzania hakuna ugaidi na Sheria hiyo ya Ugaidi inawalenga zaidi raia Waislamu.

Akasema, hivi sasa matokeo ya utekelezaji wa Sheria hiyo yanaonekana wazi kwani wanaokamatwa na kutuhumiwa kwa ugaidi wengi wao ni Masheikh na Waislamu wa kawaida.

Lakini la kusikitisha zaidi ni kwamba hata kesi zake mahakamani zinakwama kusikilizwa na Waislamu wakabaki wafungwa mahabusu wa muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu makala hayo Sheikh Ponda, anasema ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi, lakini makala hiyo ipo wazi kuwa yeye ndiye anayehusisha Uislamu na ugaidi.

Akifafanua Sheikh Ponda, amesema Mwandishi wa Makala hiyo amewataja Waislamu wasomi wa Vyuo vya Kiislamu kama Magaidi huku Misikiti, Madrasa, Asasi kama vile vituo vya Yatima na Shule za Kiislamu amevitaja kuwa ni vituo vya Kigaidi.

Aidha amesema, katika makala yake hiyo ameyataja mataifa kadhaa aliyodai kuwa yanayoelekea kusambaratika kutokana na hicho alichokiita ni ugaidi.

Sheikh Ponda amemtanabahisha mwandishi huyo kuwa uandishi wake unatakiwa azingatie maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusu suala hili zito linalohusu uhai wa watu na mustakbali wa Taifa, badala ya kuja na uchambuzi wa taarifa bandia za Intelijensia.

Kwani taarifa sahihi anazo Azory.
BOTH ARE TRUE
 
Dunia ina Waislam 1.8 bilion ambao kila siku wanasali kuilaani Israel lakini Allah wala hajibu maombi yao kamwacha Israel aendeleze kichapo kwa waumini wake....kuna shida mahali siyo bure
kweli shida ipo. shida kwamba waislam wameambiwa wakiristo wasiwafanya marafiki na wandani wao, walipowafanya marafiki ndio hayo yanatokea. au nimekufahamu vibaya?
 
una uhakika gani kwamba boko harama ni waislamu? Unajua kwamba isis wanajifanya ni waislamu ila cha ajabu hata kusali tu hawajui ? Acheni kuamini kila kitu mnachoambiwa na mzungu tumieni akili zenu
Unajua kwamba waislamu duniani kote wakisali wanaelekea kibla ila angalia hawa mazuzu wa isis wakisali huku kila mtu akielekea anapojua yeye, ujinga mtupu
Pole sana maalim
 
Si lazima kukubali. Ukweli kwamba ukifa nje ya uislam wewe ni moto. huo ndio ukweli
Kwa hiyo watakaoiona pepo.ni.waislam tuuu eeeeeeeeh.Wakati mwingine usiwe unaruhusu watu kuuona ujinga wako.Ni Fedheha.Ungezaliwa China kwa mujibu wako unekuwa condemned to hell?Puuzi kabisa wewe
 
Yale matoto ni terror breds future terrorists.

NO MERCY MAAMAEE
Ukiandika kama mkristo sishangai maana bible na tanakh vinawaamrisha kuuwa watoto ambao hawana hatia what peaceful religions anyway let me back up with some verses.

2 wafalme 2:23-24

(23)Elisha aliondoka Yeriko, akaenda Betheli. Alipokuwa njiani, wavulana fulani walitoka mjini wakaanza kumzomea wakisema, “Nenda zako, nenda zako mzee kipara!”

(24)Elisha aligeuka akawatazama na kuwalaani kwa jina la Mwenyezi-Mungu. Dubu wawili majike wakatoka mwituni, wakawararua wavulana arubaini na wawili miongoni mwao.

1 samweli 15:3

Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.
 
Anyway speaking from fact ..

ulisikia wapi magaidi wana sema "praise the lord uku wakiwa na panga" au "Halllelujah" uku wana mtutu..


sina maana muslim ni ma gaidi hapana ... maana ata wa kristo wana vigund uko west africa .. ila wengi wapewe


siku sikia "Allah Akhabar" kwa public afu kaa apo apo you will understand wat we talking about ,[emoji23][emoji23]


"it is what it is "

nothing personal .. free view
Kesho naenda kujaribu hii pale kariakoo nakuwa na begi kubwaaa na kipaza Sauti nasema Allah Akhabar tuone itakuwaje 😂 😂 😂
 
Hakuna muislamubaliyechinja mtu yoyote kusa dini ni watu wanaojifanya waislamu
Incharge,

Waislamu wengi si wote wapo emotional sensitive ukijaribu kupingana nae au kumtania kuhusu dini yake.

Mbona yalishatokea huko miaka ya nyuma mpaka watu wakauana.
 
Huenda wao wakawa ni majuha kuhusu misingi ya 'jihad' na sifa zake na vipi inatakiwa kuwa au sababu za kuwepo kwake,,,,!!!

Ndio maana haijawapo kusikika kutoka kwa prominent and most influential muslim scholars wa Tanzania au popote pale duniani wanaohamasisha jihad in the universe kwa sasa!!!

Hao wanaoshabikia hayo mapigano hawana tofauti na mashabiki wa kisiasa waliofeli kiasi cha kuomba itokee vita au coup d'etat.
They are not patriots
Well said
 
kweli shida ipo. shida kwamba waislam wameambiwa wakiristo wasiwafanya marafiki na wandani wao, walipowafanya marafiki ndio hayo yanatokea. au nimekufahamu vibaya?
Uko sahihi mkuu

Waombaji 1.8 bil hawajapata majibu kwa dua zao. Bado Wazayuni, Manaswara na Wacomminist wa China wanadominate ulimwengu
 
Hizi mada zinagusa imaninza watu. Hivi Osama, Sadam na Aboubakar Baghdad yule jamaa wa IS na sisi waislam wa huku Tandare nani anafata misingi ya Imani yake?
Benjamin Nyetanyau na mkristo anayejiita muisrael kiimani wa hapa Masasi nani anafuata Imani yake kweli kweli?
Ndiyo maana hata mtu akiipinga Israelkwa utashibwake bado Imani yake itamfunga na mwingine hivyo hivyo ktk uislam. Maana yake huwezi kuwa mkristo ukawazidi wayahudi kwa haki ya Sheria wala huwezi kuwa muislam ukawazidi Saudia, Afghanistan, Iraq au Iran kwa ujanja.
Ndiyo maana wakristo magaidi wapi na wanaua na wakristo wachache ndo wanapinga the same to Islam na Buddhist
 
kwa hiyo nembo ni mtu kusema Mungu ni mkubwa ? basi kwa kiarabu ndio muislamu .

Nataka kuona hapa kundi la kigaidi limeenda Mecca kuhij ndio nitaamini , hawa hata kule hawafiki 😀 😀 😀
Wanaoenda Kuhiji Mecca Muongozo wao sio Quran, Hadith, na Miratul Rasul??
 
Back
Top Bottom