Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Hongera mkuu, kama alivyosema mwamba mmoja hapo juu, ukipata buku kumi tupia kule, ishirini kule, sahau kwa mda then njoo utashangaa hazina yako itakavyoongezeka.
Purse as per George classon in his classic richest man in Babylon [emoji23]
 
Mkuu big up sana kwa madini, hata Mimi naweza kusema...bila kupitia hivyo vitabu viwili ulivyovitaja, inawezekana nisingeifungia hata huu uzi, hakika ni vitabu Bora sana as far as personal finance in concerned. Paying yourself first...lo..mkuu safi sana.

Ahsante sana tumejifunza mengi mno.
Pamoja sana kiongoz, maarifa mengi ujue yamefichwa kwenye makaratasi na mbaya zaidi watz wengi hatunaga kasumba ya kusoma vitabu, kwakweli ni vitabu vinavyoelimisha sana, TIBA SABA ZA POCHI TUPU[emoji23]
 
[emoji1] sure, bt hazina yako usije ukampa mfyatua matofali aende kununua vito vya dhahabu itapotea.
Naam exactly,..seek advice from those who were competent through their own experiences to give it. And you said brickmakers? About brick making they give good advice [emoji122]. Ni kitabu Cha zamani,.ila ni kizuri na kinafaa sana
 
Huu uzi nimeusubscribe kabisa niendelee kupata madini. Iko hivi nimepata kazi fulani ya muda kidogo, nimejifikiria naona biashara za kawaida is not my call sehemu pekee ninayoweza pata faida ni kupitia hizi mutual funds.
Malengo yangu ni kutenga nusu ya mshahara niuwekeze kwa sababu naweza sema sina majukumu mengi, sina mtoto, silipi kodi ya chumba, ni vitu vidogo vidogo ninavyoweza kujibana mwenyewe. Naona ni bora niwekeze huku.
Wakuu naomba muendelee kutupa madini zaidi na zaidi tujifunze. Natanguliza shukrani wakuu!!
 
Mifuko yote ni mizuri na interest rate zao karibu zinalingana. Mfuko mzuri wa kujiunga nao inategemea malengo yako.

Kwa mfano kama unataka kuwekeza akiba kwa muda mrefu, huku ukiiongezea pole pole nayo ikijikuza taratibu - Umoja itakufaa.

Lakini iwapo una pesa nyingi za kuweka kwa muda fulani na unaweza kuzitoa anytime, Liquid inakufaa. Hii ni mbadala mzuri wa fixed deposit za benki, ila yenyewe haina fixed time.

Iwapo umepata fedha nyingi na unataka zikae mahali ule polepole, kwa mfano viinua mgongo vya wastaafu - bond fund inakufaa.

Ukitaka kuweka akiba kusomeshea watoto baadaye - kuna watoto fund

nk.

Naamini ukienda ofisini kwao watakupa maelezo ya kina zaidi, maana mimi natumia tu personal experience.
Inamaana kama ukiweka Pesa sawa Mfano 1mil kwenye Liquid na Umoja.Baada ya Mwaka Umoja itakua na pesa nyingi kuliko Liquid?
 
Mkuu
Hizo nukta ni desimali. Hivyo bei (net asset value per unit) ziko katika mamia na sio malaki.

Mifuko ina bei mbalimbali kwa vile ilianza kwa nyakati tofauti.

Umoja ndio ulikuwa mfuko wa kwanza kuanzishwa kwa bei ya sh 100 kwa kipande, ambayo imekua taratibu hadi hiyo zaidi ya 800 sasa. Ukuaji huo ndio kinachovutia wawekezaji.

Mfuko wa Liquid ulianza baadaye sana kulinganisha na umoja, nao ukaanza na bei ya 100. Bei yake pia inaendelea kukua.

Mfuko wa bond ukiufuatilia kukua kwa bei yake ni polepole zaidi. Hii ni kwa sababu mwekezaji wake analipwa kila mwezi (au kila miezi sita kama amechagua hivyo), hivyo sehemu kubwa ya faida kuliwa reguraly badala ya kukuza uwekezaji.

Hizo bei hazimaanishi mfuko moja una faida kuliko mwingine, la hasha. Kuchagua kwako mfuko kuendane tu na lengo lako la kuwekeza.
Mkuu ina maana Kwenye Liquid pesa inarudi na kuingizwa kwenye mtaji?
 
Samahani kiomgozi ameuliza mfano kama anazo Sh 5ml awekeze wapi ndiyo kuzuri, sasa kwenye majibu yako hapa naona umeanza kusema awekeze kwenye Mfuko wa Umoja ndiyo nzuri kisha ukarudia tena kama ana Sh 5+ ml awekeze Bond account.
Hapa naomba twende taratibu Kwa Sh 5ml Umoja atapataje na akiweka Bond itakuwaje?
Umoja atapata benefit ambayo ni 12% - 16% kwa mwaka, ila Bond anapewa hio percentage na kila mwezi ana dividend za 50,000 which is more profitable kuliko ikikaa umoja
 
Mimi nilifanikiwa kufungua Akaunti na nikaweza kujaribu Kununua vipande.Je, vile vipande nilivyonunua kwa njia hii ya simu inakuwa ya aina gani ya uwekezaji wa mfuko wa UTT?
wakati unachagua account ulichagua account gani? mara nyingi ni umoja kama hukuangalia vizuri, ila pia unaweza nunua vipande kama vya 10,000 alafu vikisoma kwenye simu angalia vipande hivyo linganisha na bei ya vipande katika soko ili ujue aina ya mfuko uliowekeza au fika officini kwao sukari house ujue na kama hujaupenda utatoa pesa kuhamishia mfuko mwengine
 
Mkuu ina maana Kwenye Liquid pesa inarudi na kuingizwa kwenye mtaji?
Unaweza kusema hivyo. Inavyotokea ni kwamba kwa mfano unaponunua thamani ya kipande ni sh 110. Kila siku thamani iabadilika kidogo. Baada ya mwezi kipande hicho chaweza kuwa na thamani, mathalan ya sh 111. Ukuaji huo huendelea hadi siku utakayotoa fedha yako utt kwa kuwauzia wenyewe utt vipande vyako. Utauza kwa thamani current, sio ile ya 110 uliyonunulia.

Liquid ni mbadala mzuri na wenye manufaa kuliko fixed deposits za benki, na ilianzishwa haswa kuwafaa walio na fedha wanataka kuziweka mahala kwa muda fulani kabla ya kuzitumia. Wakati huo zipate faida.

Advantage ya liquid muda wa kuwithdraw mtaji wako ni uamuzi wako, ofcourse na rate mostly ni nzuri zaidi kulinganisha na bank accounts.
 
Inamaana kama ukiweka Pesa sawa Mfano 1mil kwenye Liquid na Umoja.Baada ya Mwaka Umoja itakua na pesa nyingi kuliko Liquid?
Faida za mifuko ya utt hazitofautiani sana. Hivyo nadhani mfuko uchaguao utokane hasa na lengo lako.

Iwapo hiyo 1m kwa mfano, au kiasi chochote, unataka ikae utt kwa mwaka au kwa kipindi fulani, halafu uje kuwithdraw na kutumia, mfuko unaokufaa zaidi ni Liquid. Hata usipojua ni kwa miezi mingapi fedha zitakuwa huko sio shida.

Bond inawafaa zaidi waliopata fedha nyingi na wanaziweka utt ili faida yake itumike kuwalipa kiasi fulani kila mwezi. Ukiweka say 100m kwa mfano, utapata kila mwezi a bit over 1m, huku ile 100m yako nayo ikiongezeka kutokana na salio la faida linalobaki baada ya monthly payment.

Kwa hiyo katika bond sehemu kubwa ya faida unagawiwa monthly (au wengine huchagua kila miezi 6), na sehemu ndogo ya faida inayobaki hukuza mtaji.

Umoja hasa ni kwa ajili ya wapendao kusave kwa ajili ya future. Yaani kutokula faida au mtaji siku za karibuni. Unawafaa sana vijana na watu wa umri wa kati wapendao kusave kwa ajili ya uzeeni. Waweza kuingiza huko kiasi kila mara. Mfano wangu mimi nilianza na Umoja nikawa natumbukiza huko kila mara. Nilipostaafu nikaswitch kuingia mfuko wa Bond, ambako sasa napata kitu kila mwezi.

Naona by default anayeingia utt kama hajaspecify mfuko atakao wanamwingiza Umoja.
 
Umoja atapata benefit ambayo ni 12% - 16% kwa mwaka, ila Bond anapewa hio percentage na kila mwezi ana dividend za 50,000 which is more profitable kuliko ikikaa umoja
Mimi nimewekeza Umoja, nikifikisha kiasi fulani cha pesa nitawekeza kwenye Bond.Nakumbuka kuna mdau alisema unaweza kubadilisha mfuko.
 
wakati unachagua account ulichagua account gani? mara nyingi ni umoja kama hukuangalia vizuri, ila pia unaweza nunua vipande kama vya 10,000 alafu vikisoma kwenye simu angalia vipande hivyo linganisha na bei ya vipande katika soko ili ujue aina ya mfuko uliowekeza au fika officini kwao sukari house ujue na kama hujaupenda utatoa pesa kuhamishia mfuko mwengine
Ni Umoja mkuu, niliangalia bei.Maana kila siku najitahidi kudunduliza na massage zinazokuja ni bei ya vipande vya Umoja.
 
Faida za mifuko ya utt hazitofautiani sana. Hivyo nadhani mfuko uchaguao utokane hasa na lengo lako.

Iwapo hiyo 1m kwa mfano, au kiasi chochote, unataka ikae utt kwa mwaka au kwa kipindi fulani, halafu uje kuwithdraw na kutumia, mfuko unaokufaa zaidi ni Liquid. Hata usipojua ni kwa miezi mingapi fedha zitakuwa huko sio shida.

Bond inawafaa zaidi waliopata fedha nyingi na wanaziweka utt ili faida yake itumike kuwalipa kiasi fulani kila mwezi. Ukiweka say 100m kwa mfano, utapata kila mwezi a bit over 1m, huku ile 100m yako nayo ikiongezeka kutokana na salio la faida linalobaki baada ya monthly payment.

Kwa hiyo katika bond sehemu kubwa ya faida unagawiwa monthly (au wengine huchagua kila miezi 6), na sehemu ndogo ya faida inayobaki hukuza mtaji.

Umoja hasa ni kwa ajili ya wapendao kusave kwa ajili ya future. Yaani kutokula faida au mtaji siku za karibuni. Unawafaa sana vijana na watu wa umri wa kati wapendao kusave kwa ajili ya uzeeni. Waweza kuingiza huko kiasi kila mara. Mfano wangu mimi nilianza na Umoja nikawa natumbukiza huko kila mara. Nilipostaafu nikaswitch kuingia mfuko wa Bond, ambako sasa napata kitu kila mwezi.

Naona by default anayeingia utt kama hajaspecify mfuko atakao wanamwingiza Umoja.
Mimi mkuu Uzi huu umenisaidia sana sana
 
Hio ya kuswitch nimeipenda
 
Mkuu weww ni MTU mwema Sana naamini mungu atakunyooshea njia kwenye mambo yako!

Umenipa Darasa kubwa Sana.

Barikiwa.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom