Faida za mifuko ya utt hazitofautiani sana. Hivyo nadhani mfuko uchaguao utokane hasa na lengo lako.
Iwapo hiyo 1m kwa mfano, au kiasi chochote, unataka ikae utt kwa mwaka au kwa kipindi fulani, halafu uje kuwithdraw na kutumia, mfuko unaokufaa zaidi ni Liquid. Hata usipojua ni kwa miezi mingapi fedha zitakuwa huko sio shida.
Bond inawafaa zaidi waliopata fedha nyingi na wanaziweka utt ili faida yake itumike kuwalipa kiasi fulani kila mwezi. Ukiweka say 100m kwa mfano, utapata kila mwezi a bit over 1m, huku ile 100m yako nayo ikiongezeka kutokana na salio la faida linalobaki baada ya monthly payment.
Kwa hiyo katika bond sehemu kubwa ya faida unagawiwa monthly (au wengine huchagua kila miezi 6), na sehemu ndogo ya faida inayobaki hukuza mtaji.
Umoja hasa ni kwa ajili ya wapendao kusave kwa ajili ya future. Yaani kutokula faida au mtaji siku za karibuni. Unawafaa sana vijana na watu wa umri wa kati wapendao kusave kwa ajili ya uzeeni. Waweza kuingiza huko kiasi kila mara. Mfano wangu mimi nilianza na Umoja nikawa natumbukiza huko kila mara. Nilipostaafu nikaswitch kuingia mfuko wa Bond, ambako sasa napata kitu kila mwezi.
Naona by default anayeingia utt kama hajaspecify mfuko atakao wanamwingiza Umoja.