Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

mkuu mfuko wa liquid fund sina uzoefu nao, unaweza kunielezea jinsi unavyofanya kazi? Na ni mzuri kuzidi bond fund? Hauna masuala ya kupanda na kushukaa kwa hela Yako?
Nipe tips za mfuko wa liquid fund.
Asante.
 
mkuu mfuko wa liquid fund sina uzoefu nao, unaweza kunielezea jinsi unavyofanya kazi? Na ni mzuri kuzidi bond fund? Hauna masuala ya kupanda na kushukaa kwa hela Yako?
Nipe tips za mfuko wa liquid fund.
Asante.
Mfuko wa liquid hauna tofauti kubwa na mfuko wa bond ambao sera yake ni kutoa gawio. Benchmark ya mfuko wa liquid ni kuwekeza kwenye treasure bills za siku 35 hivyo haunathiriwi sana na soko la hisa kama Umoja fund. Kwa mwaka jana riba ilikuwa 14% ingawa kwa kawaida range ni
12% Hadi 14% Wanaouendesha wana mechanisms nzuri ya kuhakikisha unakuwa stable na ndio maana wanawekeza kiasi kikubwa Cha fedha kwenye treasure bills ambazo zinauhakika uhakika 100% kulipwa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hivi hesabu zimekaaje nikisema nikope bank,mfano 25m alafu niende kuwekeza UTT? ntapata hasara au faida?
Hapo inategemea umekopa kwa % ngapi na mkopo wenyewe ni workers salary loans au unapeleka marejesho. Wataalamu wanasema sio vema kukopa ili kufanya uwekezaji huu lakini inawezekana pia. Unaweza kuweka principle kwamba kila fedha unayoipata kiasi fulani unawekeza.Mambo ya msingi vipande vya UTT vinaonezeka thamani na pia hutengeneza compound interest

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Labda nitoe mfano hai.Mfano nimekopa milioni 32 mkopo wa miaka saba,alafu nikawa nakatwa 582k.Hii milioni 32 nikienda kuwekeza UTT ntakuwa naingiza 320k kwa mwezi,wakati nakatwa marejesho ya mkopo 582k. LAKINI kwenye faida nayopata UTT ya 320k kwa muda wa miaka saba ambao ndio mkopo unaisha ntakuwa nimeingiza 26,880,000,hii faida ukijumla na 32m nilizowekeza nakuwa jumla na 58,880,000. WAKATI huo huo kwenye marejesho ya mkopo ya 582k kwa miaka saba ntakuwa nimewapa bank 48,888,000......hizi hesabu za kwenye makaratasi,je kwenye application zipo sawa?
 
Hapo unatengeneza faida kwa compound interest mfano: Liquid fund interest ni 12% hadi 14% tuchukue wanatoa 12%
1st year= 12/100×32,000,000/= unapata 3,840,000/=ongezeko Kwa mwaka ambao unajumlosha na mtaji wako wa 32,000,000 unapata 35,840,000/=
2nd year= 12/100×35,840,000= unapata 4,300,800 hii faida unajumlosha na mtaji wako tena wa 35,840,000 unapata 40,140,800/=
3rd year= unaendelea Hadi miaka 7 hapo ukumbuke pia thamani ya vipande inakua pia na % inaweza kufika 14%

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Asante sana mkuu nimekuelewa vyema,lakini naomba nieleweshe zaidi kuhusu hiyo compound interest.Mimi nilijua faida pekee inayopatikana UTT ni kupitia ongezeko la thamani ya vipande,nilijua kwamba faida ya asilimia 12 inakokotolewa na kuingizwa kama thaman ya vipande.Wakati naanza kuwekeza thaman ya kipande ilikuwa 314,mpaka sasa kipande kimefika kwenye 325. Unataka kuniambia ukiacha thamani ya vipande kuongezeka,kuna gawio lingine litakuja?.........Kuhusu hiyo compound interest niliwahi kuwapigia UTT kuwauliza hawakunipa jibu la kueleweka,nafanyaje ili niianze kuiona? nafanyaje ili nianze kuipata? au kwa pesa yangu kukaa tu na kuingia mwaka wa pili automatic inaanza kuingia? Kwa sasa nina miezi sita,nimejiunga na mfuko wa liquid.
 
sasa tofauti kubwa ya bond na liquid fund ni ipi?? maana kwa maelezo haya bado sijaona tofauti. au minimum depost amount liquid fund ni ndogo kuliko bond fund.
 
Mkuu tunakuomba huku uje kutupa madini.
 
Mkuu tunakuomba huku uje kutupa madini.
Bond Fund unawekeza kwenye hati fungani za serikali kwa kiwango Cha 90% au zaidi rasilimali za mfuko na 10% au chini ya 10% mfuko unawekeza katika rasilimali zenye ukwasi kama vile Treasury bills, hatifungani za makampunu na aina nyingine kwa kiwango kisichosidi 5% ya rasilimali za mfuko. Bond Fund ina mpango wa kukuza mtaji, kugawa gawio Kila mwezi au miezi sita au mwaka yaani fedha zinaingia kwenye account yako. Meneja wa mfuko anapofanya uwekezaji anaweza kunegotiate kupata punguzo kidogo anaponunua government Bonds sababu wakati mwingine hununua Bonds kwa wingi na kupata faida kubwa ya ongezeko la thamani , hivyo faida inaweza kuwa kubwa kuliko hata wewe mwenyewe kuwekeza kwenye bonds za serikali kuu Moja kwa Moja. Liquid fund wenyewe lengo ni kukuza mtaji na mfuko huu unawekeza kwenye masoko ya fedha tu na benchmark yake ni Treasury bills za siku 35. Hivyo mifuko yote yaani Bond Fund na Liquid fund ni mizuri. Liquid fund ni mzuri sababu una ukwasi mkubwa unaweza kuuza vipande kwa haraka na kupata fedha. Bond fund ni mzuri lakini ikiwa umechagua mpango wa gawio ina maana ukuaji wa mtaji unapungua kidogo. Ushauri: Unaweza kuwekeza kwenye mifuko yote miwili yaani Bond fund na Liquid fund

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ubarikiwe sana sana. ..kama hautojali kuna swali hapo juu post namba 351 nalo naomba jibu. Samahani kwa usumbufu lakini.
 
Mnajichanganya huko watawapigia calculation na formula za kisanii wakusumbue, tumieni FIXED ACCAUNT
 
Nmefanikiwa na mm kujiunga na UTT kupitia App
Kwa mfuko kwa umoja fund
Ingawa bado cjafka ofcn kwao hope ntaenda Kujaza form
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…