Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Nashukuru pia nimepata mwongozo
Ila naomba kuuliza, kuwekeza kwenye huu mfuko inakulazimu kukaa mda gani ili kujitoa? Ni lazima uanzie miaka 10? Au mwekezaji anapewa nafasi ya kuchagua mda wa kuwekeza?
Lini kujitoa (au kuuza vipande vyako) ni uamuzi wako tu. Hakuna cha miaka 10 wala miezi 10. Siku yoyote ukiamua unajaza fomu na unapata fedha zako ndani ya siku 3 - 10 za kazi, kutegemea aina ya mfuko wao ulioingia.

Baadhi ya mifuko (mfano Umoja) ina kitu wanaita exit load, yaani rate ya kununua kipande ni pungufu kidogo kuliko rate ya kukiuza. Rate hizi za kuuza na kununua hubadilika (kawaida huongezeka) na hutangazwa pamoja kila siku.

Mifuko mingine (mfano Liquid) haina exit load, yaani rate ya kununua na kuuza ni sawa.

Hata hivyo baadhi ya mifuko hufaa zaidi kwa uwekezaji wa muda mrefu ili kukuza mtaji, wakati mingine ni ya kutunzia fedha kwa muda fulani upendao huku ukipata faida (kubwa kuliko benki).

Ukiweza kufika ofisini kwao utapata maelezo kuhusu mifuko yao mbalimbali na utaweza kuamua mfuko wa kujiunga nao kulingana na lengo lako. Mtu anaweza kujiunga na hata zaidi ya mfuko moja.

Pia baada ya kujiunga mtu anaweza kuhamisha fedha kutoka mfuko wao moja kwenda mwingine, wenyewe wanaita kuswitch, iwapo lengo lake linabadilika.
 
Mimi nilifanikiwa kufungua Akaunti na nikaweza kujaribu Kununua vipande.Je, vile vipande nilivyonunua kwa njia hii ya simu inakuwa ya aina gani ya uwekezaji wa mfuko wa UTT?
Ili kununua vipande ni lazima ulikwishachagua mfuko. Maelezo ya kina kuhusu mfuko uliochagua kuanza nao waweza kuyapata website ya utt.

Ukipenda kuutaja hapa labda wadau wengine watakupa maelezo zaidi.
 
Mimi baada ya kufanikiwa kufungua Akaunti kwa kutumia app ya UTT ,nikaenda moja kwa moja kwenye sehemu buy units.Sasa kwenye sehemu hiyo ya buy units kuna option ya Kununua kwa kutumia makampuni ya simu na hakuna option ya kuonesha mfuko gani .Ila baadae nikafanikiwa Kununua units na msg nikapata kwenye simu yangu kuwa nimeweza Kununua units kwa Tsh 813.0316
Ili kununua vipande ni lazima ulikwishachagua mfuko. Maelezo ya kina kuhusu mfuko uliochagua kuanza nao waweza kuyapata website ya utt.

Ukipenda kuutaja hapa labda wadau wengine watakupa maelezo z
 
Mimi baada ya kufanikiwa kufungua Akaunti kwa kutumia app ya UTT ,nikaenda moja kwa moja kwenye sehemu buy units.Sasa kwenye sehemu hiyo ya buy units kuna option ya Kununua kwa kutumia makampuni ya simu na hakuna option ya kuonesha mfuko gani .Ila baadae nikafanikiwa Kununua units na msg nikapata kwenye simu yangu kuwa nimeweza Kununua units kwa Tsh 813.0316
Huo wa bei hiyo ni mfuko wa umoja. Huu hasa unafaa kwa anayelenga kuwekeza kwa muda mrefu ili afaidi ukuaji wa mtaji (japo huzuiliwi kutoka any time).

Naamini unaijua investor account number, ambayo ndio utakuwa unaitumia kununua vipande vingine kaongezea.

Ni vizuri ukiendelea kununua vipande kuongezea uwekezaji wako mara kwa mara. Kama ni mfanya kazi waweza hata kupanga kiasi fulani kila mwezi ukanunulia vipande vya ziada. Ukifanya hivi baada ya miaka kadhaa utafurahia uwekezaji huu.
 
Investor Account Number ninaijua mkuu.Nashukuru sana Uzi huu wakuu na Mungu awajalie.
 
Huo wa bei hiyo ni mfuko wa umoja. Huu hasa unafaa kwa anayelenga kuwekeza kwa muda mrefu ili afaidi ukuaji wa mtaji (japo huzuiliwi kutoka any time).

Naamini unaijua investor account number, ambayo ndio utakuwa unaitumia kununua vipande vingine kaongezea.

Ni vizuri ukiendelea kununua vipande kuongezea uwekezaji wako mara kwa mara. Kama ni mfanya kazi waweza hata kupanga kiasi fulani kila mwezi ukanunulia vipande vya ziada. Ukifanya hivi baada ya miaka kadhaa utafurahia uwekezaji huu.
Mkuu naomba unijuze ni wastani WA interest rate Kwa mwezi kutokana na mifuko hii

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Interest rate hubadilika, lakini kwa uzoefu wangu wa muda mrefu ni zaidi ya 11% kwa mwaka, ambayo ni bora kuliko kuziacha pesa benki.

Ni wazi rate hii ni kidogo sana ukilinganisha na biashara ya mafanikio - lakini kwa tusioweza au tusiopenda kufanya biashara, utt ni mahali sahihi kusave akiba.
 
Asante Sana ndugu yangu ,

Vipi mfuko mzuri ni upi ?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Asante Sana ndugu yangu ,

Vipi mfuko mzuri ni upi ?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mifuko yote ni mizuri na interest rate zao karibu zinalingana. Mfuko mzuri wa kujiunga nao inategemea malengo yako.

Kwa mfano kama unataka kuwekeza akiba kwa muda mrefu, huku ukiiongezea pole pole nayo ikijikuza taratibu - Umoja itakufaa.

Lakini iwapo una pesa nyingi za kuweka kwa muda fulani na unaweza kuzitoa anytime, Liquid inakufaa. Hii ni mbadala mzuri wa fixed deposit za benki, ila yenyewe haina fixed time.

Iwapo umepata fedha nyingi na unataka zikae mahali ule polepole, kwa mfano viinua mgongo vya wastaafu - bond fund inakufaa.

Ukitaka kuweka akiba kusomeshea watoto baadaye - kuna watoto fund

nk.

Naamini ukienda ofisini kwao watakupa maelezo ya kina zaidi, maana mimi natumia tu personal experience.
 
Mkuu asante Sana

Napenda kuuliza tena kuwa Mwezi Jana BOT walipunguza interest rate Kwa Bonds za muda mrefu kuanzia miaka 25.

Vipi hii haina athari kushuka Kwa rates za riba Kwa mifuko ya Utt amis

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu asante Sana

Napenda kuuliza tena kuwa Mwezi Jana BOT walipunguza interest rate Kwa Bonds za muda mrefu kuanzia miaka 25.

Vipi hii haina athari kushuka Kwa rates za riba Kwa mifuko ya Utt amis

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mkuu,

Pamoja kwamba mie sio mtaalamu wa uchumi, lakini kushuka kwa riba za treasury bonds lazima kutaathiri pia mapato ya utt, kwa vile wataendelea kuwekeza huko.

Hivyo yamkini ya rate za utt kushuka kiasi ipo. Lakini naamini pia kwa vyovyote rate za utt zitaendelea kuwa bora kuliko za benki savings au fixed deposits.

Hivyo naamini si vibaya kuendelea na utt.
 
Lini kujitoa (au kuuza vipande vyako) ni uamuzi wako tu. Hakuna cha miaka 10 wala miezi 10. Siku yoyote ukiamua unajaza fomu na unapata fedha zako ndani ya siku 3 - 10 za kazi, kutegemea aina ya mfuko wao ulioingia.

Baadhi ya mifuko (mfano Umoja) ina kitu wanaita exit load, yaani rate ya kununua kipande ni pungufu kidogo kuliko rate ya kukiuza. Rate hizi za kuuza na kununua hubadilika (kawaida huongezeka) na hutangazwa pamoja kila siku.

Mifuko mingine (mfano Liquid) haina exit load, yaani rate ya kununua na kuuza ni sawa.

Hata hivyo baadhi ya mifuko hufaa zaidi kwa uwekezaji wa muda mrefu ili kukuza mtaji, wakati mingine ni ya kutunzia fedha kwa muda fulani upendao huku ukipata faida (kubwa kuliko benki).

Ukiweza kufika ofisini kwao utapata maelezo kuhusu mifuko yao mbalimbali na utaweza kuamua mfuko wa kujiunga nao kulingana na lengo lako. Mtu anaweza kujiunga na hata zaidi ya mfuko moja.

Pia baada ya kujiunga mtu anaweza kuhamisha fedha kutoka mfuko wao moja kwenda mwingine, wenyewe wanaita kuswitch, iwapo lengo lake linabadilika.
Uko vzr sana mkuu, big up kwa moyo huo, umekuwa teacher hpa, nilijiunga baada ya kuwa inspired na ww.
 
Sema tu utt sina uhakika kama wanapita humu bt walistahili kabisa kukulipa for what you're doing.
 
Back
Top Bottom