Lini kujitoa (au kuuza vipande vyako) ni uamuzi wako tu. Hakuna cha miaka 10 wala miezi 10. Siku yoyote ukiamua unajaza fomu na unapata fedha zako ndani ya siku 3 - 10 za kazi, kutegemea aina ya mfuko wao ulioingia.
Baadhi ya mifuko (mfano Umoja) ina kitu wanaita exit load, yaani rate ya kununua kipande ni pungufu kidogo kuliko rate ya kukiuza. Rate hizi za kuuza na kununua hubadilika (kawaida huongezeka) na hutangazwa pamoja kila siku.
Mifuko mingine (mfano Liquid) haina exit load, yaani rate ya kununua na kuuza ni sawa.
Hata hivyo baadhi ya mifuko hufaa zaidi kwa uwekezaji wa muda mrefu ili kukuza mtaji, wakati mingine ni ya kutunzia fedha kwa muda fulani upendao huku ukipata faida (kubwa kuliko benki).
Ukiweza kufika ofisini kwao utapata maelezo kuhusu mifuko yao mbalimbali na utaweza kuamua mfuko wa kujiunga nao kulingana na lengo lako. Mtu anaweza kujiunga na hata zaidi ya mfuko moja.
Pia baada ya kujiunga mtu anaweza kuhamisha fedha kutoka mfuko wao moja kwenda mwingine, wenyewe wanaita kuswitch, iwapo lengo lake linabadilika.