Je, ni mwanzo wa mwisho wa Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini?

Je, ni mwanzo wa mwisho wa Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Ni dhahiri kwamba Waitara "ameshauona mwisho" kabla ya kuufikia.

Leo amefanya mahojiano na waandishi wa habari akilalamika kwamba serikali imeweka mipaka ya hifadhi ya Serengeti bila kumshirikisha, Waitara alikuwa akilia kwa kwikwi na akijiapiza kwa kidole.

Anadai Chadema wamepita jimboni "wakamtwanga vilivyo" na anadai kwamba Mkuu wa Mkoa alim-fix akaenda kuongea kwa wananchi kwamba watashirikishwa, lakini alipotega mgongo, serikali ikamtupa mkono. Amekuwa akiendesha vita ya "msituni" dhidi ya viongozi wa serikali, bila shaka anapata wakati mgumu katika ubunge wake.

Waitara ni moja ya wabunge walionunuliwa katika mnada wa hadhara ili ajiunge CCM enzi ya jiwe, kwa Sasa haoni pa kwenda, labda ACT Wazalendo, ni kama CCM wanamtema kimtindo.

Baadhi ya wanaomfahamu, wameshauri atafute dereva na asiwe anatembea peke yake, anaweza kupata ajali kubwa sana kutokana na msongo wa mawazo kuelekea 2025.
 
Huyu biashara ishaa kwisha!
20220910_173608.jpg
 
Atakuwa alilewa,tunamkumbuka na kauli yake akiwa naibu waziri miundombinu "wewe barabara inakuhusu nini?,kunywa bia".
Alikuwa honeymoon ya kisiasa, akifaidi ulinzi wa Jiwe, Sasa saiti pagumu, shamba Lina mwamba wa mawe
 
Machozi yakiendana na kauli za Mura Mura Poti Poti! Wanataka kutugaragaza ....

Hii inaitwa kulia 'KiKurya' kwa kuonesha kuguswa na mazuri au mabaya, ni kawaida kwa kanda hii.
 
Ukiona mtu mzima analia, ujue ubunge umekwenda

Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshasema majimbo ya ubunge 2025 mengi yatakwenda CHADEMA na hili la Mwita Waitara ni moja ya majimbo yaliyo tayari kwa mabadiliko.

Tutaona vilio vingi zaidi toka kwa wabunge waliopita kwa kubebwa na mbeleko ya uchafuzi wa uchaguzi 2020
 
11 November 2022
Tarime, Tanzania

Wachimbaji wadogo wasusa mkutano, wanyanyuka na kutoka ukumbini, walalamika tumeumizwa sana na kufilisiwa


Walaani vitendo vya kufilisi wachimba wadogo wa Nyamongo.

Mgodi mkubwa wa Barrick pia upo katikati ya makaazi ya watu vipi wao wachimbaji wadogo wana pigwa vita na kamishna wa Madini kuwa wanachimba katika makaazi ..... wamkumbuka John Pombe Joseph Magufuli ...
Source : Nyamwaga online TV


16 December 2022

Mbunge Mwita Waitara (CCM) awatoa hofu wananchi wa Komarera Tarime



Akumbushia wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya tangu kuzaliwa CCM yaliyofanyika kitaifa mkoani Mara alieleza malalamiko ya wananchi wa Komarera kuhusu fidia.

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia CCM Bw. Mwita Waitara almaarufu Chief amesema mambo yapo katika mchakato mzuri wa kufanyiwa tathmini na hivyo wananchi watoe ushirikiano.

Wale ambao wamepata fidia mbunge (chief) Mwita Waitara kuwa wale waliopokea basi watapitiwa na vyombo vya usalama na pia magreda kubomoa ...

Source : Nyamwaga online TV
 
Back
Top Bottom