Je ni sahihi kiusalama Kiongozi Mkuu wa Nchi (Rais) kuombewa akiwa kashikwa mabega

Nadhani swali sahihi lingekuwa, ni sahihi mke wa mtu kuombewa kashikwa mabega na mchungaji mwanamme?
 
Mkuu,

Si sahihi kwa kiongozi wa nchi isiyofuata dini yoyote kufungua kanisa.

Hii ni violation ya kanuni muhimu ya Separation of Religion and State.

Tuanzie hapo kwanza.
 
Nadhani swali sahihi lingekuwa, ni sahihi mke wa mtu kuombewa kashikwa mabega na mchungaji mwanamme?
Boss hoja ilihusu Rais kama Mkuu wa taasisi sensitive ya Urais ambaye usalama wake ni muhimu kwa watanzania wote na sio kama mama wa familia yake
 
Mkuu,

Si sahihi kwa kiongozi wa nchi isiyofuata dini yoyote kufungua kanisa.

Hii ni violation ya kanuni muhimu ya Separation of Religion and State.

Tuanzie hapo kwanza.
Kwangu nadhani akialikwa na muda ukaruhusu anaweza kwenda kufungua au kufanya shughuli yoyote kwenye dhehebu au dini yoyote hata kwa wasio na dini kama anavyoenda kwenye gatherings za machief so kwa hapo na kwa kiongozi wetu hakuna shida. Hoja hii itakuwa na nguvu ikitokea kiongozi achague dhehebu flani tu alafu imani zingine azitenge
 
Anaweza kwenda lakini huo ndio mwanzo wa kuchanganya dini na siasa.

Mwanasiasa atatumia dini kupumbaza watu wasimbane, na viongozi wa dini watatumia wanasiasa kujitajirisha na kupiga deals.

Na watu wa dini tofauti wataona wamebaguliwa.

Tayari Waislamu Zanzibar wanasema Samia anawapendelea sana Wakristo anawapa hela sana anatembelea sana makanisa. Habari hizi zishaanza kuleta mgawanyiko wa kidini.

Rais angeweza kuepuka yote hayo kwa kutojiingiza makanisani.
 
Acha uwongo weka picha tujiridhishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…