Je ni sahihi kumlipia nauli mfanyakazi wako mpya?

Je ni sahihi kumlipia nauli mfanyakazi wako mpya?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Katika pita pita zangu mtandaoni, nikakutana na kijana anatafuta kazi.

Nikamfanyia usaili kwa njia ya mawasiliano, ikaonekana nikimpachika sehemu fulani itakuwa si mbaya, ili yeye apate nami pia nipate.

Baada ya maongezi mengi, nikamshauri aende akaripoti kituo cha kazi ambacho kipo mkoa mwingine.

Ndipo akanijulisha kuwa ana mke, na anajaribu kuangalia namna ya kumuacha.

Mi kwa sababu ni muelewa, nikamwambia kama inawezekana nenda naye tu kwa sababu sehemu ya kukaa si tatizo; Wote tukakubaliana.

Baada ya muda, akanijulisha yeye atangulie kwanza, nami nikamkubalia.
Baada ya dakika 15 kupita, ananiambia nauli sina, unanisaidiaje?

Sikumjibu, nikaona hayuko makini na kazi.

Je, wanamna hiyo, yuko sawa kudai nauli?​
 
Watu wa mtandaoni ni matapelo usikubali kumtumia hela mwambie akope akifika eneo la kazi hyo hela utaituma kwa muhusika

Au tafuta dereva wa gari linalofika site mpe oda ya kumleta Hadi eneo la kazi husika
 
Umesema
katika pita pita zako mtandaoni et?

Mpaka unaomba ushauri hapa inaonekana una wasiwasi na huyo kijana

Kuna mawili pengine hana kweli nauli au anataka kukutapeli

Mwambie aazime nauli sehemu aki ripoti kazini pesa itarudishwa
Na hiki ndicho nilichomuambia
 
Watu wa mtandaoni ni matapelo usikubali kumtumia hela mwambie akope akifika eneo la kazi hyo hela utaituma kwa muhusika

Au tafuta dereva wa gari linalofika site mpe oda ya kumleta Hadi eneo la kazi husika
Uko sahihi, wengi hawaaminiki.
 
Uko sahihi, ila nahisi kama atatumia nauli yake au atakopa itakuwa ni ishara ya uhitaji wa kazi.
From your perspective inaweza kuwa sawa, but sometimes usiweke kutafuta logic sana kwenye haya mambo.

Just humanity. Siamini mtu anaetaka kazi na kama umemfanyia intavyuu na akakidhi vigezo vyako anaweza kushindwa kuwaza option uliyoisema. It is rough out there - inaweza ikawa ndiyo chance yake kupata mishe. Hebu step back usiiangalie kama employer to employee. Iangalie kama human to human. Kunaweza kukawa na sababu nyingi zinazomfanya akuambie hivyo. Maoni yangu tu.
 
Back
Top Bottom