Je, ni sahihi kumpa hela Mama mkwe ambaye bado hujamuoa mtoto wake?

Je, ni sahihi kumpa hela Mama mkwe ambaye bado hujamuoa mtoto wake?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Naomba nijibiwe kwa hekima kidogo.

Ni binti naweza sema ni mchumba wangu japo kwetu hajulikani, yeye anakaa na mama yake ni mtumishi.

Tunafahamiana na mama yake tu hatujawahi kuonana japo jambo lililofanya nijuane na mama yake kwa kipindi hicho ni kibaya sana na hatua aliyochukua ni mbaya sana ambayo kila siku inanipa sonona nikifikiria.

Imepita miaka sasa sijawahi kuwasiliana nae, japo dogo siku zote ana push agenda ya Mimi kuwasiliana na mama yake huwa namkatalia.

Leo kanisumbua nimtafute mama yake, nikaamua kumpigia lakini kaniomba hela kidogo amepata shida fulani.

Mimi kwangu sioni ubaya kuombwa hela, kwenye familia yangu hakuna mtu anaeweza kuniomba hela na hawajawai (wanao uwezo kunizidi)..

Swali linakuja je, ni sawa kutoa hela kwa mama mkwe ambae hujamuoa binti yake?..

Kwa wazoefu tu
 
Haya watu KAZI wanakuja kukupa majibu.
20220914_003720.jpg
 
Hiyo ni warning light.

Mama mkwe hana hata aibu ya kuomba omba hela kwa mpenz wa mwanae.

Je ukiwa mume itakuwaje?

Ndoa za zamani zilikuwa na misingi mingi sana mama mkwe alikuwa hata hawezi kuongea na mume wa mwanae
Hii ndio ninayoijua Mimi, lakini hii ya kwangu ni tofauti sana, kila nikimwambia huyo binti kwamba mama ake atanijua official nikienda kujitambulisha but yeye analazimisha sana.
 
Nitasema generally..

Mimi.
Kabla sijamuoa, kibinaadamu, alishika mimba, ilifanyika busara ya ujumbe wa kwetu kwenda kwao. Mimi sikwenda. Siku yakwanza kukutana na mama mkwe ilikua ni hospitali binti alipojifungua, tulipata chumba private kwenye ile wodi ya wazazi. Mama mkwe hakuweza kukaa mimi nikiwepo ndani ya kile chumba. Ilikua nikiingia mimi yeye anatoka. Nilipogundua nikawa nampa muda yeye kwasababu alikua anamsaidia mzazi na kichanga. Nikienda nyumbani kuwaona, nikishamsalimia ataondoka sebuleni, hapo ni wataniagia.
Hapo nimejaribu kukupa picha ya mama mkwe na mume wa binti wanavyokua, ukiacha umjini mjini.

Mama mkwe:
Sijui kwa mila nyingne, ila ukiuacha huu umjini mjini, mama mkwe na mume wa binti hawana ukaribu wa kiasi hicho. Ni desturi kwa mume kutoa chochote kwa mama mkwe ila hii ya kuomba inakua na ukakasi flani

Wewe:
Hapa tusameheane kidogo.
Wewe bado ni mtoto (kifikra) usie na ukomavu. Sijui una umri gani lakini una immaturity ya hali ya juu. Hivi hatakama kakosea, hili ni lakuja kulianika hapa..!!? Labda ni mama wakileo mwenye hali flani ambae uwezo wa kujiongeza na kujizui upo kwa kipimo flani kiasi cha kuomba hela kwa mkwe, tena mtarajiwa. Lakini wewe mkwe mwenyewe, umeombwa trillion ngapi mpaka uombe ushauri hapa. Ni kweli akili yako haitoshi kupembua hili..!!?

Kwani ungemwambia "mama sina ila nipe siku mbili tatu nikuaangalizie" ingekuaje? Au ungempa halafu ukae nae kwa akili ingekuaje? Au ungesema kwa busara kua huna, halafu ukaendelea na maisha kimya kimya ingekuaje? Tujifunze kukomaa.
Nilisema unisamehe na hapa nasema uniwie radhi.
 
Back
Top Bottom