Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

sisi ni special bhana regardless..

tatizo letu sisi tunajiona tupo sahihi kwa kila kitu hata kama sio, unakuta mwanaume kaoa mwanamke sahihi ila mwanamke hajaolewa na mwanaume sahihi ndo changamoto zisizokua na kichwa wala miguu zinajitokeza and sikuiz imekua common sana. Unakuta mwanaume anajificha kwenye kichaka cha "nataka mwanamke mpambanaji sio goalkeeper" ili kukwepa majukumu
Ukisikia Mwanaume anayedai kwamba anataka Mwanamke mpambaji asiye Goalkeeper, huyo mweke kwenye group la Magasho.

Hakuna mwanaume hapo,

Hicho hakipaswi kuwa kipaumbele cha kuchagua mwanamke
 
Ningelikuwa mimi ndo huyo kijana kamwe nisingekufuata tena nikisimama kiuchumi kwasababu hufai kuwa mke kama utamkimbia mwenzako kisa kayumba kiuchumi
Kweli kabisa. Tunajua wanawake ni wale wale tu. Almost wote wana tamaa, lakini kiukweli ni bora nikutane na mwanamke mwingine nikiwa nishafanikiwa kuliko kurudi kwa ambae aliondoka wakati nina hali mbaya
 
Mimi ni msichana nina miaka 26 nina mtoto mmoja ambae nimezaa na huyu mwanaume kiukweli nina changamoto ambayo nahisi kukataa tamaa iko hivyo mwaka 2019 nilikuta na huyu mwanaume nilimkuta akiwa anaishi mwenyewe kapanga chumba nikaingia nae kwenye mahusiano mwaka huo huo nikabeba mimba alikataa mwisho akibali akanitambulisha kwao nikajifungua yeye wakati huo ameajiliwa kiwandani..

Mwaka 2022 akaacha kazi kiwanda na kuchukua NSSF yake milioni 3 akanipa milioni moja nifungue biashara hela yake iliobaki alichafua kula starehe na rafiki zake ikapelekea hela yake kuisha na kuwa jobless maana kazi hana ikawa mimi ndo baba na mama wa kulisha familia kwa kutengemea biashara yangu mpaka ikafa biashara yenyewe maana mahitaji mengi kuliko faida ya biashara nikawa mama wa nyumbani na yeye hana kazi maisha magumu nikarudi kwetu na mwanangu yeye akawa anakuja ukweni kula na kuondoka hela hatoi maana hana kazi…

Mimi nikapambana nikachukua mkopo nikafungua biashara yangu huku nikimuhudumia yeye na mwanae kula nikasema ngoja nimtafutie kazi kila nikimtafutia kazi anakataa kufanya nikachoka mwisho akakubali kufanya japo mshahara wa kawaida huduma kutoa kawaida tu mimi ndo responsible wa vitu vingi akaacha kazi hiyo sehemu kwasababu ambazo hazina maana now hana kazi mimi ndo namlisha ndani haamki wala kuumiza kutafuta kazi anasema hataki kazi ngumu za viwanda kazi ni kulala tu ndani na kupiga simu za kufanya udalali ambazo hazina faida kodi imeisha wala hajisumbui naomba ushauri nimuache uyu mwanaume au maana nikiendelea kumlemaza naona najiumiza sana hajalishi anajali kiasi gani ila sio muajibikaji najikuta naumia kupambania familia mwenyewe nisaidie kimawazo ninaweza kujinyonga

Aise ! baba yangu yupo kama huyo mmewako.

mama anapambana anafanya biashara kwakujihangaikia.

mzee anabeba pesa kwenda kuhonga michepuko yake.

yaani baba ndiye huongoza kumpiromosha mama kiuchumi.

nihatari sana kua na mme wa kihivyo.

ni wajinga sana mzee wangu namchukiaga sana familia haiendelei maana kila kipato kikipatikana anakibeba kwakua yeye ndo mkuu.

ni wajinga hawafai atakuja kukuonyesha huko uzeeni nakwambia.

{ yaani mke ndo ailishe familia ? . halafu mtu wa kiume anasema hataki kazi ngumu ?. } nisikufariji hapo ondoka.

huyo mtu ni hatari sana nina mfano wa baba yangu ni uchafu siyo mme huyo.
 
Haibadilishi maana ya kuwa kuna wanaume ni wapumbavu na wavivu tu haijalishi nini, tumekutana nao na tunaishi nao! hii ya kugeneralize ndio inawashinda kutoa ushauri kwenye cases kama hizi! mnaanza kujiweka kwenye special groups kwahiyo mlitaka nani awatafutie?
Ni huzuni kwakweli Seran
 
Aise ! baba yangu yupo kama huyo mmewako.

mama anapambana anafanya biashara kwakujihangaikia.

mzee anabeba pesa kwenda kuhonga michepuko yake.

yaani baba ndiye huongoza kumpiromosha mama kiuchumi.

nihatari sana kua na mme wa kihivyo.

ni wajinga sana mzee wangu namchukiaga sana familia haiendelei maana kila kipato kikipatikana anakibeba kwakua yeye ndo mkuu.

ni wajinga hawafai atakuja kukuonyesha huko uzeeni nakwambia.

{ yaani mke ndo ailishe familia ? . halafu mtu wa kiume anasema hataki kazi ngumu ?. } nisikufariji hapo ondoka.

huyo mtu ni hatari sana nina mfano wa baba yangu ni uchafu siyo mme huyo.
Unakuta mama ndio analipa ada hapo! Na wa kuitwa vidume humu bado wanatetea huo upunga! Kweli humu watu wana shida kisaikolojia!
 
Je ni kweli mke ni ubavu wa mme?,je huyo ni chaguo lako,je Mungu uumpa mtu amfananae?je ni sahihi na haki kama yeye ndo angekuwa anakulisha wewe akukatae kwa sababu ni golkipa
 
Nyie mnataka usawa wa kijinsia at the same time muendelee kupata benefits alizokua anapata mwanamke nyakati za mfumo dume. Kitu ambacho ukikileta kwenye uhalisia unaona hakuna mtililiko wa kimantiki. Mnachokitaka ili kiwe practicable mwanamke unatakiwa uolewe na mwanaume tajiri. Bahati mbaya hatuna matajiri wa kutosha kuweza kuwaoa hata 3% tu ya wanawake wote.

Unavyotaka usawa wa kijinsia kuna mambo mawili lazima uyaelewe. Kwanza, haki sawa inakuja na wajibu sawa. Yaani kama wote mna kipato basi mtashirikiana kulipa bill za nyumbani au kama mmoja wenu ndie mwenye kipato basi atawajibika.

Pili, suala la kifanikiwa ni randomly, sio gender based kama zamani, kwamba kwa sababu fursa zote alipewa mwanaume basi huyo ndie anaetakiwa kuja kwenye mahusiano na financial contributions. Kwahiyo mnatakiwa ku-normalize suala la kusettle na mwanaume uliemzidi kipato au hana kipato kabisa.

Kutaka haki sawa halafu kuwa frustrated na inevitable outcomes zake ni wazi pale beijing hamkujua/hamkuelewa mnachoenda kukipigania
Nimependa sana hii.😂😂😂

Wanawake wajifunze kunormalize kuwa swala la mafanikio halina jinsia. Anaweza kuanza kufanikiwa mwanaume au mwanamke yeyote atakaeanza kufanikiwa atatakiwa kubeba mwenzake kwa 100% bila kulalamikia jinsia, hayo ndio matokeo ya kikao cha Beijing.😂😂😂😂

Mamamamaeeeee
 
viwanda kazi ni kulala tu ndani na kupiga simu za kufanya udalali ambazo hazina faida kodi imeisha wala hajisumbui naomba ushauri nimuache uyu mwanaume au maana nikiendelea kumlemaza naona najiumiza sana hajalishi anajali kiasi gani ila sio muajibikaji najikuta naumia kupambania familia mwenyewe nisaidie kimawazo ninaweza kujinyonga
Sio yule mwanetu aliekuja kuomba kazi huyu kweli?
 
Hivi mnawezaje kulisha mwanaume asiyejishughulisha?
Km wewe ulivyoweza kumlisha mwanaume asiejishughulisha akiwa tumboni mwako na wenzio wanaweza kufanya hivyo hivyo wanalisha kisichojishughulisha kikiwa tumboni, hivi mtoto mwanaume akiwa tumboni hua anakunya na kukojoa humo humo?
 
Nimependa sana hii.😂😂😂

Wanawake wajifunze kunormalize kuwa swala la mafanikio halina jinsia. Anaweza kuanza kufanikiwa mwanaume au mwanamke yeyote atakaeanza kufanikiwa atatakiwa kubeba mwenzake kwa 100% bila kulalamikia jinsia, hayo ndio matokeo ya kikao cha Beijing.😂😂😂😂

Mamamamaeeeee
Wanataka usawa wa kijinsia at the same time waendelee kuhudumiwa. Wakati hata ilo suala la mwanamke kuhudumiwa na mwanaume ni mfumo dume ambao wao wenyewe wanaupinga
 
Kinachoshangaza ni kwamba humu unatafuta huruma na sio msaada,! Malalamiko yako hayatoi historia ya maisha yenu ya nyuma kipindi anafanya kazi kiwandani wkt huo wewe huna kazi! Kuyumba kupo kwenye maisha na huyo yupo kwenye hatua ya mpito, hivi unajiskiaje kuyaona madhaifu yake kwa wkt huu akiwa kwenye changamoto kisha ukatumia udhaifu huo kumnyanyasa na ukaamua kumuacha harafu baada ya muda Mfupi akafanikiwa? Unaonaje ukitumia nguvu kubwa kumshauri kuliko kulalamika? Nadhani ni busara zaidi mpe nafas ajiteteee kuliko kuweka mazingira ili uje kuskia mumeo anauza ua lake ili akulidhishe kwa lazima, kama nia ya utafutaji anayo mpe muda atafanikiwa lakini atunze uanaume wake asipende Sana kazi raini watampiga pasi.
 
Wanataka usawa wa kijinsia at the same time waendelee kuhudumiwa. Wakati hata ilo suala la mwanamke kuhudumiwa na mwanaume ni mfumo dume ambao wao wenyewe wanaupinga
Hii imekaa vema sana. Inafikirisha sana hii kitu.
 
Back
Top Bottom