Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Jiulize unaweza kutoa nyonyo nje mbele ya baba au baba mkwe wako ukanyonyesha mtoto.Kama unaweza ni haki kama huwezi then jiheshim
 
View attachment 3077317

Katika mwili wa mwananke kifua ni sehemu nyeti na haipaswi kuonwa na watu wengine zaidi ya mwenye mamlaka tu, yaani Mume.

Lakini tunaona baadhi ya wanawake wakinyonyesha watoto wao hadharani bila kuficha au kusitiri vifua vyao, mfano katika vyombo vya usafiri au sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

Ni haki ya mtoto kupatiwa maziwa pale atakapo hitaji, lakini sidhani kama sababu hii ndyo inahalalisha mwanamke kutoa ziwa mahali popote.

Kwa walio na dini au wasio na dini wote wanafahamu kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti na haipaswi kuonekana hovyo.

Je, ni sahihi kunyonyesha mahali popote kwa kisingizio cha kumpa mtoto haki yake?
Labda unawaza kizungu. Kiafrika hakuna shida sehemu ya siri ni kwenye uchi tu ndio maana toka enzi Waafrika wanapatunza sana kwenye uchi uwe wa mwanamke ama mwanaume. Ila wazungu wanaona sehemu ya siri kwa mwanamke ni matiti ndio maana wao kuacha uchi wazi ni kawaida yao.
 
Kwa huku mijini inategemea mtu na mtu na ndio sababu wengi wakitembea na watoto basi lazima atakuwa na mtandio ikitokea mtoto ametaka kunyonya basi anajifunika ni wachache wenye kujiacha wazi hasa eneo lenye watu wengi.

Japo hii ni tofauti sana na kule vijijini yaani mama akiwa ananyonyesha basi uthamani wa kifua unapotea tena kwa sisi waswahili huwa hatujali wala nini.
 
Ni sahihi ikiwa tu huyo mnyonyeshaji ndiye anayemiliki UCHAWI DUNIANI...

Vinginevyo ,macho ya "waja" mmmh..

Watu wanatembea na mauchawi yao...atapigwa mtu MWANGENI aione dunia chungu.....

Si vyema na busara kabisa kwani likirogwa NYONYO analotumia mtoto ni vipi usalama utapatikana kwa maziwa anayonyonya mwana?!!!

Humkuti mwanamke anayefahamu "tenets" za maisha akalitoa NYONYO hadharani...

Peace & Love [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
yani mtoto awe ananjaa ashindwe kunyonyeshwa kisa mambo yenu!
 
Kwa huku mijini inategemea mtu na mtu na ndio sababu wengi wakitembea na watoto basi lazima atakuwa na mtandio ikitokea mtoto ametaka kunyonya basi anajifunika ni wachache wenye kujiacha wazi hasa eneo lenye watu wengi.

Japo hii ni tofauti sana na kule vijijini yaani mama akiwa ananyonyesha basi uthamani wa kifua unapotea tena kwa sisi waswahili huwa hatujali wala nini.
Mijini Ni wachache sana wanao funika vifua vyao, wengi tunaona wanajichia bila kujali heshima zao.
 
Ni sahihi ikiwa tu huyo mnyonyeshaji ndiye anayemiliki UCHAWI DUNIANI...

Vinginevyo ,macho ya "waja" mmmh..

Watu wanatembea na mauchawi yao...atapigwa mtu MWANGENI aione dunia chungu.....

Si vyema na busara kabisa kwani likirogwa NYONYO analotumia mtoto ni vipi usalama utapatikana kwa maziwa anayonyonya mwana?!!!

Humkuti mwanamke anayefahamu "tenets" za maisha akalitoa NYONYO hadharani...

Peace & Love [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wengi hawafahamu hilo Mkuu, wanadhani kila sehemu inafaa kuachwa wazi mahali popote.

Wanaogopa uchawi kwa kuwafunga watoto wao hirizi kiunoni lakini wanaacha vifua vyao wazi bila kujua madhara yake.
 
Ukimwona mwananamke anayenyosha hivyo, elewa kuwa amekosa alternative na mtoto kazidiwa njaa, Wewe mwenye jicho lionalo Kwa tamaa usimwangalie. Wanaume Wengine hata wakiwaangalia wanawake kwenye tukio Hilo hata hawawazii hilo, hujifikiri Kwa kumpongeza mwanamke kwa ujasiri wa kumjali mtoto.
 
Kwa kawaida maziwa ni mojawapo ya Sehemu za siri, mmama anaponyonyesha anatakiwa kukaa mbali na watu, au wanaume
Mtoto akipata njaa kwenye bus au SGR mpo tayari kumsubiri mama akatafute kichaka anyonyeshe
 
FB_IMG_1724477018308.jpg
 
Back
Top Bottom