Je, ni sahihi mke wangu kuniambia kila Mwanaume anayemtongoza?

Je, ni sahihi mke wangu kuniambia kila Mwanaume anayemtongoza?

Lugha ya mwili ya mkeo inasababisha atongozeke kiurahisi, na hii ni hatari sana mzee baba, kwa kifupi mkeo yupo hivyo( anaingilika), sio kosa lake anapaswa kusaidiwa ni sababu ya mazingira , makuzi na malezi yake aliyopitia

Mfundishe na msaidie abadili lugha ya mwili wake inayojumuisha jinsi anavyofikiri, mawazo, hisia, muonekano, mwendo wake na hata mavazi pamoja na anavyowasiliana na wenzake( mawasiliano ya mwili wake kwa wenzake) na zaidi lazima aishi na kuwajibika kama mke wa mtu anayejiheshimu, akiwa ana msimamo hatasumbuliwa.

Pia kwepa na epuka kuingilia mawasiliano na bosi wake itakuletea stress sana hatimaye utakufa kwa presha bure ila umwambie yeye ndiye anapaswa kuwajibika kwa kuwa na udhaifu wa kuingilika kiurahisi na sio wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah, mwanamke anavyojiweka ndio jinsi ambavyo watu wanaweza kuwa na courage ya kumfuata au kutomfuata. It depends, kama ni mtu wa kujichekelesha ovyo na kujirahisisha kwa kila mtu ni rahisi sana kuingilika na watu kumpiga mistari.Mwambie abadilike awe very focused na kilichompeleka ofisini kuliko kuwa fused na watu ambao inturn ndio wanamletea usumbufu wa kumtaka kimapenzi.

Ninachokiona mwanamke wa mtoa mada ni aina ya wanawake wanaopenda sana attention ya watu kuliko kuwa confident na self-centred. Mke hajiamini anapenda approval ya watu katika kila afanyacho na hii ndio inapelekea asiwe na standards. Anazoeana sana na kila mtu halafu hana standards/msimamo ndio maana anatongozwa ovyo. Hii sio nzuri kwa afya ya mahusiano maana swala la kuliwa mke soon halikwepeki kama akiendelea na tabia hio. Actually sio tabia ya mke, ni aheri aonekane anajiskia kuliko kujirahisisha halafu atongozwe ovyo na kila mtu.
 
Ukiwa umejaaliwa kipawa cha uongozi huwezi kunyanyasa watu walio chini yako kwa cheo chako, hapo hakuna boss ni fala mmoja tu, mtafutie gep, weekend hii umuonye, akiendelea njoo tena uombe ushauri, tutakwambia nini cha kumfanya huyo khabith
 
Kama kweli hutaki abanduliwe muachishe kazi...Ukishindwa basi mwambie bosi atumie kinga!
 
Ukiambiwa hivyo unadanganywa, usiseme kuwa anakwambia kila kitu sio kweli! Akikuambia ujue hajampenda, wale ambao anawapa Huwa Hawasemi au hawataji Kamwe! Utaonyeshwa meseji Feki, calls Feki, hadi nanihii Feki lakini zile zenye uhalisia hutakaa uzione.

The way forward, relax, tafuta pesa, jenga maisha yako! Usipende kudanganywa!! Ukija kuujua ukweli utaumia Sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Angekuwa demu sawa... Mke mzee babaa acha utanii etii!! Mke wangu agongwe me ntuliee eti naatafuta pesaaa...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji15][emoji15][emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu cha Muhimu kuliko vyote ni MKEO AWE NA MSIMAMO MKALI...!!

Usidhani kuwa hapo ofisini ni yeye tu anatongozwa aisee...wanaume tuna uchu sanaa yani Anatongozwa mpaka mwenye Mimba ndo mkeo asitongozwee... Yeye apunguze hizo story pengne anakwambia ujisikie wivu na umjali zaidi.. Sidhani kama ni boss tu ndo anamtongozaa wapo wengine wengi tu.. So Kutongozwa ni nature ya mwanamke ilaa kukataa Ni UWEZO WA WANAWAKE WACHACHE SANAAA omba mkeo awe mmoja wa haooo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Otherwise umeliwaaaaaa yani ukute ashaanza kumla kwenye meza za ofisi tayarii...mkeo anavunga tu hapoo[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni utoto na uendawazimu kukasirika, kisa mkeo anatongozwa?!! Tambua kwamba wanawake kutongozwa ni jambo la kawaida sana, haijalishi ameolewa au hajaolewa, na pia kwa wanaume wengi kutongoza ni jambo pia la kawaida haijalishi mwanaume anayetongoza ameoa au hajaoa. Si leo wala si kesho wanawake wataendelea kutongozwa na wanaume wanaendelea kutongoza, hii ni kanuni ya asili. Kwani WEWE hutongozi au kwasababu hujasema hapa? Ni utoto na uendawazimu kukasirika, kisa mkeo anatongozwa!?

Sawa, inakera kutambua bosi wake mkeo anamtongoza, lakini pia inakera mkeo kukuambia kwamba bosi wake anamtongoza!? Atakuambia wangapi? Inakera kwasababu, mbona hasemi wengine wanaomtongoza, madukani, sokoni, barabarani? n,k. Mkeo akikupa idadi ya wanaomtongoza kwa siku, wiki hadi mwezi si utachanganyikiwa kabisa??!! Unahitaji hekima, tena kwenye hili mkeo anahitaji hekima zaidi kuliko wewe! Tambua mkeo ni mwanamke ni binadamu kama wengine, hivi alishawahi kukuambia wanaume anaovutiwa nao? Unadhani mkeo hajui jinsi ya kuwakatalia wanaume? wangapi alishawakataa na wewe wala hujui chochote?

Yaonekana ndoa yenu bado changa na hizi ni changamoto ambazo mnabidi wewe na mkeo mjifunze, sio kila anayekutongoza umwambie mumeo au mkeo. Yawezekana mkeo hana uzoefu au hajafundwa vema kukabiliana na changamoto za ina hii.

Ushauri ufanyeje
Usitaharuki na endelea kuishi kwa upendo na mkeo na umuunge mkono ili 'aweze kuikabili changamoto hiyo'. Anachofanya bosi si sahihi lakini hilo lisikutoe wewe kwenye mstari, baki na mkeo kwa mapenzi ya heshima zote. Muulize mkeo anataka wewe umsaidieje au ufanyeje ili kutatua changamoto hii, tafuta njia ya kistaarabu ili bosi wake ajue kwamba wewe unajua kwamba yeye (bosi) anamnyemelea mkeo. Kwasababu mwisho wa siku bosi asifanikiwe azma yake lakini pia kibarua cha mkeo nacho kisiote nyasi.

Kama unahitaji msaada zaidi nitafute inbox
 
Back
Top Bottom