Lugha ya mwili ya mkeo inasababisha atongozeke kiurahisi, na hii ni hatari sana mzee baba, kwa kifupi mkeo yupo hivyo( anaingilika), sio kosa lake anapaswa kusaidiwa ni sababu ya mazingira , makuzi na malezi yake aliyopitia
Mfundishe na msaidie abadili lugha ya mwili wake inayojumuisha jinsi anavyofikiri, mawazo, hisia, muonekano, mwendo wake na hata mavazi pamoja na anavyowasiliana na wenzake( mawasiliano ya mwili wake kwa wenzake) na zaidi lazima aishi na kuwajibika kama mke wa mtu anayejiheshimu, akiwa ana msimamo hatasumbuliwa.
Pia kwepa na epuka kuingilia mawasiliano na bosi wake itakuletea stress sana hatimaye utakufa kwa presha bure ila umwambie yeye ndiye anapaswa kuwajibika kwa kuwa na udhaifu wa kuingilika kiurahisi na sio wewe.
Sent using
Jamii Forums mobile app